Wamekosa hoja wamekuwa viroja!

Wamekosa hoja wamekuwa viroja!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
3,156
Reaction score
3,628
Habari wanajamvi!

Ndivyo unavyo weza kusema, Wamekosa hoja wamekuwa viroja. Duniani hakuja wahi kuwa na kaburi la ukweli, ukweli siku zote ni mchungu. Ukweli hupendwa na wenye kukumbatia haki tu basi. Ukweli hata ukinong'ona hupaa kama moto wa nyika wakati wa kiangazi kikali.

Naam, Mtu wa Mungu Zakary Kakobe kanena ukweli mtupu siku ya sikukuu ya Noel. Ule ni ukweli tena ukweli mtupu.

Vijana legelege wasaka vyeo na wazee waoga wameamua kumvaa Kakobe huku wakijua watashindwa kabla ya vita kuanza. Vijana wengi ndani ya ccm ni wajinga na wasaka vyeo! Daima huelekea upepo unako vumia. Huwa hawatumii akili. wana waza vyeo na maisha rahisi hata kama kufanya hayo ni kuhatarisha Amani ya Nchi. Wazazi wao nao wako taabani kifikra ndio maana 'mwenzao' anawageuza kama senene kwenye kaangio la moto.

Wange tamani wote tuwe wajinga. Wakituambia bomoa nyumba ya Mbowe, tubomoe bila kuhoji.
wakituambia msiende kumuombea Lissu kanisani wote tukubali bila kuhoji kulikoni?
Kakobe kawa mbeba maono! Kasema kwaniaba yetu. Amekataa kuwa mjinga, ameita beleshi ni beleshi na siyo kijiko kikubwa.
Anae taka kuombewa ni sharti awe na hofu ya Mungu. Awe mkweli, asiwe mtu wa visasi wala upendeleo.Aheshimu wakubwa na wadogo na awe na Lugha ya upole.
Hongera kakobe, hakika unastahili kukaa madhabahuni.
 
Natamani na namuomba mungu anijalie uzima,na ninawaombea Wana CCM wote uzima,ili siku upinzani ikichukua dola wawepo wote, na katiba mpya waisome vzl sijui wataficha nyuso zao wapi, na sijui watakuwa wageni WA Nani maana watalia na kuabika Dunia nzima, japo siku haijulikani lakini itakuwa mda si mrefu,
 
Mwenyekit wa wakazi mkoa wa Bashite. Cccccm
 
Natamani na namuomba mungu anijalie uzima,na ninawaombea Wana CCM wote uzima,ili siku upinzani ikichukua dola wawepo wote, na katiba mpya waisome vzl sijui wataficha nyuso zao wapi, na sijui watakuwa wageni WA Nani maana watalia na kuabika Dunia nzima, japo siku haijulikani lakini itakuwa mda si mrefu,
Ahahahahaaaaa
Na amini wote watakuwepo tu
 
Natamani na namuomba mungu anijalie uzima,na ninawaombea Wana CCM wote uzima,ili siku upinzani ikichukua dola wawepo wote, na katiba mpya waisome vzl sijui wataficha nyuso zao wapi, na sijui watakuwa wageni WA Nani maana watalia na kuabika Dunia nzima, japo siku haijulikani lakini itakuwa mda si mrefu,
wale hawana aibu! Watakuambia walikuwa wanasaka maisha.
 
hakika ni vijana wote walioko CCM hawatumii akili. Wao huangalia matumbo yao tu basi.

Nimeipenda hii"Wanagezwa geuzwa kama SENENE kwenye kikaangio"

Maana ni kweli kabisa wanageuzwa kwa maneno yasiyo na tija wala umuhimu
 
Amani nadhani ina lindwa hivi kwamba asiwepo wa kusema
 
Na mhurumia huyu Kakobe kitakacho mpata
Acha woga wa kilofa

Kwa huyu baba ubaya,mtu useme au usiseme ni yale yale

Kakobe sema baba tusaidie na wengine tuliofungwa midomo kwa lazima Mungu yuko nawe hizi chimbilili ndogo ndogo zisikutishe
 
Acha woga wa kilofa

Kwa huyu baba ubaya,mtu useme au usiseme ni yale yale

Kakobe sema baba tusaidie na wengine tuliofungwa midomo kwa lazima Mungu yuko nawe hizi chimbilili ndogo ndogo zisikutishe
Kwangu mimi Kakobe amefungua njia ya watukuto kuogopa kusema ukweli. Mmoja hawezi kushinda walio wengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom