Lowassa si muumini wa
Janteloven, anatufaa
urais?
Johnson Mbwambo Toleo la 380 19 Nov 2014
Lowassa Urais 2015
Johnson Mbwambo
mbwambojohnson@yahoo.com
reply
reply
More information about text formats
Text format
WAFALME wa mataifa huwatawala watu
wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili
wa watu (friends of the people). Lakini
isiwe hivyo kati yenu; bali yule aliye mkuu
kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote,
na aliye kiongozi lazima awe kama
mtumishi.
Wiki iliyopita niliyakumbuka tena maneno hayo ya
Yesu Kristo katika Biblia (Luka 22;25-26)
nilipokutana na watu wanaoshabikia mbio za
Edward Lowassa waliofurahishwa na matokeo ya
utafiti wa asasi ya Twaweza yanayoonyesha
kuwa mtu wao huyo ndiye anayeongoza mbio
hizo ndani ya CCM.
Kwa hakika, wiki nzima ya jana gumzo kuu
sehemu mbalimbali nchini ni matokeo ya utafiti
huo wa Twaweza. Wako waliofurahishwa nayo na
wako waliyoyabeza kwa hoja kwamba
yalipikwa.
Waliofurahishwa nao, wakiwemo baadhi ya
waandishi wa habari niliokutana nao, wanadai
kuwa matokeo hayo ya Twaweza yanathibitisha
kuwa eti Edward Lowassa ni Mtu wa
Watu (Man of the People). Hao ndiyo
walionifanya niyakumbuke maneno hayo ya Yesu
Kristo.
Niseme tu hapa kwamba walioisoma riwaya ya
mwaka 1966 ya hayati Chinua Achebe ya A Man
of the People (Mtu wa Watu), watanielewa
nikisema hapa kwamba si kila mtu wa watu ni
mtu wa watu kweli!
Watanielewa nikisema ya kwamba, kati ya hao
wanaoitwa watu wa watu wapo pia watu wa
watu wa sampuli ya Mh. Nanga kama
ilivyosimuliwa na Chinua Achebe katika riwaya
yake hiyo ya A Man of the People.
Niende mbali zaidi kwa kusema ya kwamba, hata
hao waandishi wa habari waliofurahishwa na
matokeo hayo ya utafiti wa Twaweza kuhusu
Lowassa miongoni mwao wapo wa aina ya
James wa gazeti la Daily Chronicle; kama
ilivyosimuliwa na Achebe katika riwaya yake
hiyo.
Labda niwe muwazi zaidi kwa kusema kwamba,
binafsi, mpaka sasa sijakutana na wafuasi wa
Lowassa, wakiwemo waandishi wenzangu, ambao
wanamshabikia kiongozi huyo kwa sababu ya
kuvutiwa na vision yake (kama anayo) ya namna
ya kuikomboa nchi hii.
Kwa hakika, wengi niliokutana nao wala hata
hawajui mtu wao huyo (Lowassa) anaelemea
mrengo gani katika siasa za duniani hii kulia
au kushoto, kati kushoto au kati kulia.
Wao hilo haliwasumbui. Wanachojali tu ni mtu
wao huyo (Lowassa) aingie Ikulu ili nao
wanufaike kwa kuteuliwa katika nafasi
mbalimbali za uongozi kama vile u-DC, u-RC,
ujumbe wa bodi za mashirika ya umma, ubunge
wa kuteuliwa, ubalozi, ukatibu mkuu wa CCM nk!
Hisia zangu ni kwamba hata kwa wagombea
urais wengine ndani ya CCM hali ni hiyo hiyo.
Yaani wanazungukwa na wafuasi na wapambe
ambao hawajali kujua sera zao, vision zao,
mirengo yao ya kisiasa nk; bali wanachojali ni
kukamata tu Ikulu na kuanza kugawiana vyeo na
njia za ulaji!
Wala hakuna wanaojali kuhoji kama wagombea
urais wao hao wana mkakati wowote mpya
unaotekelezeka wa namna ya kulitokomeza
tatizo kuu linaloitafuna Tanzania ya sasa, na
ambalo sasa limekuwa kansa sugu - tatizo la
kukithiri kwa ufisadi na mmonyoko wa maadili.
Huko nyuma nilishawahi kusema kwamba, hata
mtu akiniamsha usingizini saa nane usiku na
kuniuliza ni tatizo gani moja kuu linaloiangamiza
Tanzania yetu kwa sasa, nitamjibu kuwa ni
ufisadi na kuporomoka kwa maadili.
IPTL ufisadi, ununuzi vipaza sauti bungeni
ufisadi, biashara meno ya tembo ufisadi,
ugawaji vitalu vya uwindaji ufisadi, ujenzi
maabara ufisadi, uuzaji UDA na mashirika
mengine ya umma ufisadi, zabuni za
halmashauri ufisadi, uchimbaji madini
ufisadi, vyeo, chaguzi na nyadhifa ufisadi,
manunuzi ya umma ufisadi, utoaji ajira
ufisadi, huduma za jamii kama elimu na afya
ufisadi, utoaji haki mahakamani ufisadi, ujenzi
wa barabara ufisadi, utoaji ardhi za vijiji kwa
wawekezaji - ufisadi; yaani ni ufisadi, ufisadi,
ufisadi! Hata dini siku hizi ni ufisadi mtupu!
Ninaposema ufisadi ni tatizo kuu la Tanzania kwa
hivi sasa maana yangu ndiyo hiyo.
Ni kweli kuwa tuna matatizo mengi kuanzia ya
ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma
duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji
safi na salama kwa watu wetu, demokrasia
changa, utawala dhaifu, nk, lakini, kwa mtazamo
wangu, bado tatizo kuu linabaki kuwa ni ufisadi
kuporomoka kwa maadili.
Naamini hivyo kwa sababu, juhudi zote
zinazofanyika na zitakazofanyika baadaye
kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira, elimu duni,
kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu
duni nk, zinakwazwa na zitakwazwa na
kutamalaki kwa ufisadi katika kila nyanja ya
maisha yetu.
Huo ndiyo ukweli. Kwa hiyo, adui wetu mkuu wa
zama hizi ni ufisadi.
Na ndiyo maana, binafsi, nampima Lowassa kwa
kigezo hicho, na sio wingi wa shule za sekondari
za kata ambazo alisimamia kujengwa wakati
akiwa waziri mkuu!
Kwangu mimi, tuhuma za ufisadi aliohusishwa
nao katika kashfa ile ya Richmond ambayo
kwayo alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu nazipa
nafasi kubwa katika kumpima kama anafaa kuwa
rais wetu mpya ajaye kuliko kuangalia idadi ya
shule za sekondari za kata alizosimamia
kujengwa nchini.
Hata kama nitaiweka tuhuma hiyo ya Richmond
pembeni, na kujiuliza iwapo katika maisha yake
yote ya kisiasa na nafasi alizoshika aliwahi
kuibeba ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, napata
kigugumizi kutoa jibu la ndiyo.
Yaani sikumbuki ni lini Lowassa amewahi
kukemea ufisadi nchini! Na kama miujiza itatokea
na CCM kumteua awe mgombea urais wake,
nitashangaa kama kwenye mikutano ya kampeni
ataibeba ajenda ya vita dhidi ya ufisadi!
Atathubutu?
And yet, ufisadi na kutoweka kwa maadili ndiyo
tatizo kuu linaloitafuna nchi yetu kwa sasa. Kwa
maneno mengine ni kwamba, bila kuchukua kwa
makusudi hatua za kujenga utamaduni wa
kuuchukia ufisadi sawa na ule wa Janteloven wa
nchi za Scandnavia, hatutafika popote
kimaendeleo.
Hatutafika popote kimaendeleo hata kama
tutampata rais mchapakazi kama Lowassa
mwenye uwezo wa ajabu wa kusimamia ujenzi
wa sekondari mbili mpya kila mwezi katika kila
wilaya nchini! Kama si muumini wa Janteloven,
hatufai.
Dk. Kitila Mkumbo katika chambuzi zake za hivi
karibuni, kwenye gazeti hili, kuhusu wasaka urais
aliandika ya kuwa Lowassa ni mchapakazi lakini
mwenye nakisi ya uadilifu!
Kama kweli Lowassa ni mchapakazi wa kiwango
cha hali ya juu, ni jambo lenye ubishi
linalojadilika. Lisilo na ubishi, hata hivyo, ni
ukweli kwamba Lowassa ana nakisi kwenye
kipimo cha uadilifu labda kama kashfa ya
Richmond au ile ya kusimamia uuzaji wa mali za
AICC haina maana yoyote kwa anayebisha.
Na kama ana nakisi katika kipimo cha uadilifu
(rejea vuguvugu lile la CCM la kumvua gamba
yeye, Rostam na Chenge), huhitaji kuwa msomi
wa elimu ya kurusha maroketi kujua kwamba
Lowassa na Janteloven ni mbali kwa mbali
angalau mpaka sasa.
Ndiyo maana sitachoka kusema ya kuwa, kama
atachaguliwa mwaka 2015 kuwa rais mpya wa
Tanzania, kamwe hatawezi kuupiga vita ufisadi
na kujenga nchini mwetu utamaduni wa ki-
Janteloven kwa sababu si muumini wa
utamaduni huo.
Na bila kuujenga utamaduni huo nchini na
kuukomesha ufisadi uliotamalaki kila kona ya
maisha yetu, siioni nchi yetu hii ikijinasua kutoka
kwenye dimbwi la umasikini ilikozama, na wala
siioni haki ikitendeka kwa wanyonge na masikini.
Janteloven ni nini? Janteloven ni utamaduni wa
kuuchukia ufisadi. Utamaduni huo asili yake ni
Denmark. Wenyewe wanauita utamaduni huo The
Jante Law au kwa ki-Denishi Janteloven.
Ni Janteloven hiyo ambayo kwa miaka kadhaa
sasa imeifanya Denmark ishike nafasi ya kwanza
katika nchi 10 bora duniani ambazo ufisadi ni wa
kiwango cha chini mno, kwa mujibu wa vigezo
vya Transparency International (TI); yaani
Corruption Perception Index.
Sheria ya Jante au Janteloven (ki-Denishi) au
Jantelagen (ki-Swedish) ni sheria ambayo
haikuandikwa popote ambayo asili yake ni kitabu
cha mtunzi wa kale wa Denmark aliyeitwa Aksel
Sandemose.
Mwaka 1933 Sandemose aliandika kitabu cha
riwaya kinachoitwa A Fugitive Crosses His
Tracks (En Flyktning krysser sitt spor) ambacho
kimezisaidia nchi za Scandnavia hadi leo
kuuchukia ufisadi.
Riwaya hiyo ya Sandemose inahusu maisha ya
jamii katika kijiji kinachoitwa Jante ambako
walijiwekea utamaduni wa kuheshimu kanuni 10
ambazo kwa pamoja zinaunda hicho kinachoitwa
The Jante Law.
Kimsingi, kanuni hizo zinazounda The Jante Law
zinazungumzia saikolojia ya kuuchukia ubinafsi;
saikolojia ya kuuchukulia utajiri uliopatikana kwa
njia zisizo halali kuwa hauna maana (un-worthy)
na si sahihi na haukubaliki (in-appropriate).
Katika riwaya hiyo, wakazi wa Jante waliovunja
sheria ya Jante (ambayo kama nilivyosema,
haikuandikwa popote) walitiliwa shaka na
kuchukiwa. Mathalan; kama raia wa Jante
aliweza kujenga jumba kubwa ghafla, alitiliwa
shaka na inapobainika kwamba alilijenga kwa njia
za dhuluma za aina yoyote, alichukiwa na jamii
nzima.
Kwanza unatiliwa shaka, na ikibainika ni kweli
mafanikio yako ni ya kifisadi, unachukiwa na jamii
nzima. Mambo mawili yalikuwa muhimu kwa raia
wa Jante inapotokea mtu akapata mafanikio ya
haraka kwanza shaka (suspicion) na kisha
chuki (hostility).
Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba Sheria ya
Jante (kama ilivyo katika riwaya ya Sandemose),
ilisaidia kujenga utamaduni wa kuuchukia ufisadi
katika nchi ya Denmark miaka nenda rudi, na
ndiyo maana haishangazi ripoti za TI
zinaionyesha Denmark kuwa ni nchi yenye
kiwango cha chini mno cha ufisadi duniani.
Leo hii, nikitafakari kuhusu Tanzania yetu, na
jinsi tulivyozama katika ufisadi kuanzia kwenye
siasa hadi kwenye miradi ya maendeleo nchini,
kuanzia majumbani kwetu tunakoishi hadi kwenye
nyumba zetu za ibada, nashindwa kuamini
kwamba ipo siku nasi Tanzania tutaitwa Nchi
Iliyoendelea (A Developed Nation).
Na ni kwa sababu ya kiu hiyo ya kutaka kuiona
siku moja nchi yetu ikiitwa A Developed Nation
sitamuunga mkono hata mara moja mgombea
urais mwenye virusi vya kukumbatia ufisadi na
mafisadi!
Daima nitawaunga mkono wagombea urais
wanaonipa matumaini ya kuwa watasimamia
nchini mwetu ujenzi wa saikolojia ya kuuchukia
ufisadi (Janteloven).
Nasema hivyo, kwa sababu, kama nilivyoeleza
mwanzo, hilo ndilo tatizo mama linalotukwaza na
litakalotukwaza na kuturudisha nyuma katika
mipango yote mizuri ya maendeleo
itakayopangwa baadaye.
Nihitimishe kwa kusema kwamba hata hao
wagombea wengine wa CCM wanaochuana kwa
karibu na Lowassa; yaani kina Membe, Pinda,
Sumaye, Makamba, Wassira, Magufuli, Sitta nk,
simuoni hata mmoja ambaye ni muumini
kikwelikweli wa Janteloven. Simuoni hata mmoja
anayemkaribia japo kidogo Mwalimu Nyerere au
Sokoine au Thomas Sankara wa kule Burkina
Faso kabla wana wa shetani hawajamuua.
Hakuna hata mmoja. Na hapo ndipo
ninapokubaliana tena na mwalimu wangu wa
somo la uraia, Profesa Kitila Mkumbo ya
kwamba, waadilifu ndani ya mduara wa sasa wa
CCM wa wataka urais, hawapo.
Na kwamba kama CCM watataka kutumia kigezo
cha uadilifu kumpata mgombea urais wake
kwenye uchaguzi wa mwakani, basi hawana budi
watoke nje ya boksi kumpata mwana CCM
MWADILIFU na muumini wa Janteloven ambaye
hayumo katika mduara wa sasa wa utawala, na
asiye na chembe ya kashfa ya ufisadi hata ya
kusingiziwa tu!
Naamini watu wa namna hiyo bado CCM inao.
Kumbuka: Si kila mtu wa watu ni mtu wa watu.
Tunao pia kina Mh. Nanga wa riwaya ya A Man
of the People ya Chinua Achebe ndani ya nchi
yetu.
Najua wapo wajinga watakaofikiri kuwa
ninayaandika haya kwa kuwa labda najiona kuwa
mimi ni mtu mwadilifu. La hasha. Wengi wetu ni
waathirika wa namna moja au nyingine ya huu
mmomomyoko wa maadili ninaouzungumzia;
nami pia nikiwemo.
Ninachomaanisha, hata hivyo, ni kwamba
tulioathirika tukae pembeni tusigombee uongozi
wa juu wa umma, na badala yake tuwaachie
waadilifu; maana hao wanaweza kutufikisha
mahali pazuri katika safari hii ndefu na ngumu ya
kushamirisha utamaduni wa Janteloven katika
nchi yetu.
Tafakari.
My note:moja ya vitu vinavyozuia Maendeleo ni rushwa kwann bado bado watu wanaiunga mkono ccm ni kutaka kurahisisha maisha Kwa kujipendekeza au kutokujua fikiria,chukua hatua.