Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Wambura Mtani aondoka RFA baada ya miaka 22

Wakati anatoka kazini clouds fm alipata ajali. Hakuomba Ho2. Alizikwa kwao Kilimanjaro.
Sio kweli hakufariki wakati anatoka kazini clouds

Huyu ni miongoni ya waliopunguzwa clouds n kina perfect clispine

Kutokana na msongo wa mawazo alikuwa anakunywa sana ndio sababu ya ajali

SO alipata ajali akiwa jobless
 
Nguli wa utangazaji kutoka kituo cha Radio Free Africa (RFA) Wambura Mtani ameondoka katika kituo hicho alicho hudumu kwa miaka 22.

Mtani ni mkongwe aliyekuwa amebaki kwenye Radio hiyo baada ya watangazaji wengine nguli kuondoka humo na wengine walifariki kama vile Jumaa Ahmed Baragaza (R.I.P) Zuberi Msabaha (R.I.P), Prince Baina Kamukulu (R.I.P), Fred Fidelis aka Fredwaa (R.I.P) ambaye baadae aliondoka.

Binafsi nitamkumbuka kwa mazuri yake hapo na akapambane kutafuta changamoto mpya.
The nikka is back ,naanza sasa kumsikiliza hapa Je Huu ni Ungwana.

Alianza na Makabila Alhmis.

Safi sana nitakuwa nasikiliza kipindi chake cha Je huu ni Uungwana maana nilikiacha kukisikiliza.
 
Mzee King Kong, kumbe tulikua pamoja alhamis nilikua nimechill na mama watoto kitandani tunasikiliza hicho kipindi cha Millenium.
Faustine Stephano X Wambura Mtani
Hahaha si unajua mimi ni mzee wa chaka 2 Chaka ,amsha popo porini lazima nitune RFA hakuna kulala mpaka Asubuhi.
 
Daah ktk kukua kwangu nikiwa najitambua nilkua nasikiliza sana RFA jumapili ndo sibanduki kwny redio...kweli siku hazigandi na watu wengi wamedondoka hapo mjengoni 🥲🥲
 
inaonesha wa mara ya kwanza walikuwa wanavumilia ila baadaye wakashindwa uvumilivu.
Mwaka kama sio 2012 waliondoka kwa mkupuo Fredrick Bundala, Kid Bwoy, Irene Tilya na mwingine wa kiss fm baadaye wakafuata akina Ezden the rocker, fredwaa na rahab. Akaja Azam akakomba kibao akina Yahya Mohamed, Hassan Mvula, Steve Moyo, Baruan Muhuza nk.

Kutoka hapo RFA haijarudi kwenye mstari.
Yahya Mohamed sasa hivi kaula ni Mkurugenzi wa habari na maudhui kama sikosei Azam...mzee wa kata wese
 
Husna Mlanzi amekufa lini tena?
Kuna miaka kama mitano au minne alikufa kwa ajali
Screenshot_20261022-211113_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom