Ghafla bila kutarajia, nimejikuta naangalia kipindi cha Shajara kupitia TBC1, kilichokuwa kinaongelea ngoma ya kabila la Wamasaia inayoitwa esotho (samahani kama nimekosea neno hilo). Sikuwahi kuisikia hii ngoma na kama nimewaelewa vizuri, ngoma hii inahusisha yafuatayo.
-Ngoma hii wanacheza watoto na vijana kuanzia miaka 8 na kuendelea, na huchezwa kipindi ambacho wanyama wana malisho ya kutosha.
-Lengo lake (sina hakika kama ni rasmi) ni kuwapa nafasi ya kujifunza kufanya ngono!!
-Morani mmoja anaweza kupendwa na wasichana hadi kumi....na wote atafanya nao ngono peke yake...Na kumetolewa ushahidi kwamba kama Morani huyo kapata lishe ya kutosha (maziwa na nyama) anaweza kufanya ngono na wasicha hadi 5 kwa usiku mmoja. Wanajikusanya kwenye boma moja na hawaoneani wivu!
-Msichana alihakikisha anaenda kwenye kundi ambapo mchumba wake hayupo
-Madhara yake kwa ni pamoja na msichana kupata mimba ila kwa siku za karibuni, ngoma hii inaongeza uwezekano wa kuambukizana ukimwi. Inasemekana hakuna matumizi ya kondomu katika ngoma hii!
Inawezekana yapo mengine mengi ila hii ni uthibitisho mwingine kwamba nchi yetu ina utajiri wa tamaduni ambazo tunaweza kuzifanyia mabadiliko chanya na kuzitumie kiuchumi. Bahati mbaya watu wanaangalia baadhi ya tamaduni ambazo zilikuwa na nia nzuri kwa mtazamo hasi!
Hapa mmenigusa kwa kweli..
Kabla sijasema chochote, Mimi ni mmasai tena yule wa asili kabisa. Kwetu Ngorongoro.
Kwanza nashukuru kwa mtoa mada na nakupongeza vilevile kwa kuwa karibu na masuala ya utamaduni wa nchi yetu.
Naomba nikusahihishe kidogo.
Siyo
Esotho ni
Esoto. Esoto siyo Ngoma bali ni utamaduni tu. Esoto maana yake ni Makutano ya morani na
intoyie(wasichana) bila kujali umri wa msichana. Nini maana ya msichana kwa kimasai?? ...Ni wale wote ambao hawajaingia jandoni, kama ambavyo mnajua kwamba wamasai mpaka watoto wa kike wanafanyiwa tohara. Lakini msichana akishaingia tu jandoni basi anatengwa kwenye kundi hili la kwenda kujumuika huko Esoto.
Kwa hiyo esoto inahusisha vijana kwa kiume yaani morani kama ulivyosema na hawa mandito yaani wasichana. Huko wanaenda kucheza ngoma mbalimbali. Pia siyo siri Ngono ipo kwa wingi. Hapa ndipo wasichana wengi wa kimasai wanapopoteza usichana wao.
Lakini kiasili Esoto haikuwa ni chanzo cha watoto wa kike kupata mimba ingali bado wadogo. Msichana kwa mila ya kimasai kupata mimba wakati bado hajafanyiwa tohara, ni jambo la aibu sana kwake na familia yake pia. Zamani msichana akishafanya kosa kama hili, anaweza hata kutengwa na jamii kabisa. Walichokuwa wanafanya kuonyesha ukali juu ya hili suala la mtoto kupata mimba ni kwamba mtoto yule(msichana) anapelekwa porini pamoja na ndama jike halafu wanafungwa kwenye mti. Wanaachwa kwa usiku mmoja halafu kama msichana ndo kachukuliwa na wanyama wakali basi inakula kwake na ndama anarudishwa home. Vilevile kama ni ndama ndo kaliwa basi mtoto atapona na kurudishwa nyumbani. Hiyo ilikuwa zamani sana. Kwa sasa kitu kama hicho hakuna wakuu.
Esoto baada ya milipuko ya magonjwa nayo imeanza kufifia sana japo bado ipo katika baadhi ya maeneo. Na kama mkuu ulivyosema ni kweli esoto huwa inafanyika nyakati za usiku hasa wakati wa masika ambapo kuna watu wana shibe kwao na kwa mifugo vilevile. Huwa ni kama vile mkulima anapotoka shambani na kwenda pengine baa kujiburudisha baada ya kazi nzito japo si nzuri sana. Hapa (esoto) ndo mahali ambapo vijana wa rika moja yaani morani hukutana na kuenjoy na wasichana wao. Wanaenjoy ngoma na ngono pia.
Hayo ni kwa uchache mkuu. Ukitaka nirudi nitarudi kadiri ya maswali yenu..
Yapo mengi ya kueleza kama nitapata nafasi.