Wamama zangu wa Sokoni waunda lugha yao!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Wamama wafanya biashara sokoni ni kundi moja maalumu lenye tabia za kipekee sana. Wanapenda kutembea pamoja kwenye kundi moja; hasa wakienda na kutoka makazini kwao. Kama itawalazimu kupanda daladala kwenda na kurudi sokoni, hupanda wote kwa pamoja, na ni kundi linaloogopewa sana na makondakta. Hawa wamama ni wakali na wenye makelele sana na hupenda lugha za matusi mazito. Ni katika mazungumzo yao yaliyojaa matusi nimenasa lugha yao yenye maana maalumu. Tazama lugha hiyo hapa chini na maana yake:
Kupiga chabo= mke kumkatalia mumewe unyumba kwa kusingizia yuko kwenye siku zake.
Kuangalia oil=Mume kutaka kuhakikisha kama kweli mkewe yuko kwenye siku zake kwa kuiona hedhi yenyewe.
Kupaka mhogo parachichi= kufanya mapenzi kinyume na maumbile
Kula aiskrim= kunyonya uume
Kunawa mtoni= kunyonya uke
Kuvua gamba=kutoa mimba
Kuomba kura= kutongoza
Kufungua bomba la bamia=kutoa mbegu za kiume wakati wa kufanya mapenzi
Kuendesha semina ya uvccm=mtu mzima kufanya mapenzi na msichana wa shule
ATM ya chenji=kondakta.
Kuweka mzigo booking= kuachana na mpenzi wako.

Hawa wamama nakutana nao sana kwenye daldala katika shughuli zangu kati ya KIA (Kilimanjaro International Airport) na Moshi mjini. Katikati ya vituo hivi viwili kuna masoko ya Kwa Sadala na Bomang'ombe




 
Mbona safari ile ni fupi sana, uliwezaje kusikia maneno yote hayo!
Ninadaka neno moja na kukaa nalo. Pia napenda kukufahamisha tabia moja ya hawa wamama. Wanazungumza haraka haraka sana na kubadili mada kila sekunde; wanazungumza kama wanashindana vile. Hapo ndipo nawafaidi. NI kweli KIA mpaka Kwa Sadala ni pafupi lakini vituo vipo vingi.Daladala ikisimama kupakia na kushusha lazima wamama walalamike kwamba wanachelewa na kutoa tusi moja kali.Wakati wote huo, harddisk yangu inafanya kazi ya 'kusave' information.
 
mmh nahisi na mkeo ni mama sokoni sa ulijuaje tafsiri ya hayo maneno?

Wala Ummu! Mke wangu sokoni anapafahamu akienda kununua mahitaji ya nyumbani kwa hiyo hanisaidii kwenye tafsiri. Tafsiri naipata mwenyewe kwenye context ya mazungumzo ya hao akina mama. Ntakupa mfano: Mama Upendo atamsalimia rafiki yake Mama Amani na kumwuliza:"Vipi mwaya, ulimaliza mzigo jana?" Mama Amani atajibu:"Mzigo uishe saa ngapi kwani nilifanya kazi? Mkata ushuru noma sana yule kisirani yule. Kazi kunifatafata tu, mara oo twende tukapate kinywaji mara oo sijui nini. "Ukizubaa tu Mama Amani imekula kwako" anadakia mwanamke mwingine na kuendelea,"Yule mtoza ushuru ndo staili zake za kuomba kura" "Kuomba kura kwangu? Mavi yake! Amwache mkewe nyumbani aje kunitongoza? Hapati kitu hapa mshenzi sana"
Kwenye hayo mazungumzo mtu unagundua kwamba kuomba kura maana yake ni kutongoza mwanamke.Kwahiyo Ummu ndivyo ninavyotafsiri gumzo lao kwa kuchuja matusi mazito sana kiasi nikitoa mifano mingine nitashushiwa ban la mwaka 2012!
 
Back
Top Bottom