samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Lakini si umeelewa? kiswahili kinakua hata hilo neno kuparanganyika zamani lilitumiwa na watu wa kutoka sehemu za Musoma zaidi lakini lilipozoeleka likawa moja ya neno la kiswahili.Asante kwa taarifa, Samahani sio mahali pake lakini sahihisho la lugha. Hili neno sintofahamu ni neno la kiswahili au unaungana mkono wa baadhi ya watu wanaoharibu kishwahili? Kwa nini usitumie neno mtafaruku, kuparaganyika, wasiwasi, kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.
Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
Lakini si umeelewa? kiswahili kinakua hata hilo neno kuparanganyika zamani lilitumiwa na watu wa kutoka sehemu za Musoma zaidi lakini lilipozoeleka likawa moja ya neno la kiswahili.
yaliytokea tunisia ndio yanaanza leo tanzania nawasihi ndugu zetu wamachinga wa Mwanza muongoze jahazi sisi tupo nyuma yenu
Nimeelewa na ndio maana nimesema asante kwa taarifa, hapo nilikuwa natoa angalizo. Sikatai neno kupagaranyika linaweza kuwa limetokana na matumizi ya watu wa musoma kama ambavyo maneno mengi ya kiswahili yalivyochukuliwa toka lugha nyingine ( kutohoa). Lakini huwezi kutumia neno sintofahamu ukiwa na maana ya wasiwasi au huko sio kutohoa ni kitu kingine kabisa .
Pili kuzoeleka kwa neno sio lazima kuwa neno hili litatoholewa, ili liingie kwenye msamiati Bakita lazima walikubali na kwa hili neno sidhani kama watakubali kulikubali kwenye maana hiyo mnayotaka tuifahamu. Ndio maana maneno kama lisaa lilitumika likazoeleka kalini bakita wakasema hapana sasa hilo nenohaliktumini kabisa.
Kusahihishana ni kuendeleza kiswahili fasihi, ukiona mtu amekosea usisite kumsahihisha ukikaa kimya tutaendelea kutumia maneno yanayozoeleka lakini yasiyokubalika na hivyo hayatotoholewa na bakwata.
Unajua maana ya watu 1m au unawadhania.ni kweli mimi nilikuwa rock city ndani nikasitukia watu kama 1 m wanaandamana huku wakiwa na malungu wakielekea jiji lakin kila sehemu wakifika wanalusha mawe kwenye maduka ndo maana maduka walifunga. Lakini zali limesababishwa na manspaa kwasababu kunamaeneo ya makoloboi wamachinga walikuwa wamepimiwa maeneo hayo lakin baada ya hapo wamachinga walianza kujenga vibanda sasa ilikuwa ni mbele ya maduka ya watu, wenye maduka walipoona wamezibwa wakaenda kwa mkulungezi wakamwambia wao hawataweza kulipa kodi kwa sababu hawauzi, wamekingwa na mamachinga. Mkulungenzi akawaamulu wamachinga waondolewe mara moja. Kwahiyo ndo walikuwa wanaandamana kupinga kitendo hicho huku wakitishia kuchoma moto maduka yote ya makoloboi. Lakini hali imeturia baada ya polisi kuzagaa mji mzima
Asante kwa taarifa, Samahani sio mahali pake lakini sahihisho la lugha. Hili neno sintofahamu ni neno la kiswahili au unaungana mkono wa baadhi ya watu wanaoharibu kishwahili? Kwa nini usitumie neno mtafaruku, kuparaganyika, wasiwasi, kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.
Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
Mkuu hata hilo hapo kwenye Bold sidhani kama lina tofauti sana na alilotumia jamaa nadhani zote ni Slang au unaweza kunipa maelezo zaidi....kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.
Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
Duh! Hivi mkoje ! Sasa mtu kaleta mada ya wamachinga mwanza, alafu watu wanapindisha mada kiswahili kiswahili. Kha