Mkurugenzi jiji Mwanza, Das Nyamagana, mtendaji Pamba, Mwanasheria Jiji, Afisa Biashara na Diwani Chadema wapiga tena mamilioni ya Shule Pamba.

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Mkurugenzi jiji Mwanza, Das Nyamagana, mtendaji Pamba, Mwanasheria Jiji, Afisa Biashara na Diwani Chadema wapiga tena mamilioni ya Shule Pamba.

Siku mbili baada ya kuandika habari kuhusu upigaji wa pesa katika eneo la shule ya Pamba, sasa watumishi hao wa umma na diwani huyo wa Chadema wameweka wazi bila kuficho namna wanavyopiga pesa za umma.

Baada ya habari hiyo kuandikwa kupitia ukurasa huu, jana viongozi hao kupitia wafanyabiashara hao waliokuwa soko kuu na Mwadeco walishusha makontena mengine.

Jana mankotena matatu yaliyoshuswa na, kuwekwa katika ukuta wa shule hiyo, karibu na geti la kuingia na kutoka shuleni hapo.

Kontena hizo tatu zilizowekwa hapo kila moja imeingia katika eneo hilo kwa gharama ya Tsh. Milioni 6.

Kwa hesabu za kawaida kontena zote tatu zimewekwa eneo hilo kwa Tsh. Milioni 18 ambazo zote zimeingia mifukoni mwa watu sita.

Makontena mawili mengine ambayo yatawekwa katika eneo hilo lililopo karibu na ukuta wa shule mahali palipoandikwa "Eneo la kupumzika mtendaji wa Pamba kwa ajili ya kuzungumza na wageni" yataingia muda wowote.

Makontena hayo mawili yenyewe kutokana na eneo kuwa dogo, yametozwa Tsh. Milioni 5 kila kontena moja.

Kwa kontena zote ambazo zimewekwa kwa siku hizi mbili, hizo za Tsh. Milioni 18 pamona na hizi za Tsh. Milioni 10 zote zina jumla ya Tsh. Milioni 28.

Licha ya watu hao kupiga pesa za zinatokana na eneo la shule, hakuna hata senti moja inayoingia kwenye mfuko wa shule hiyo iliyopo katikati ya jiji hili.

Viongozi hao wameshindwa kuona aibu, kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, chakusikitisha pesa kama hizo zinazoingia mifukoni mwao zingesaidia hata kujenga madarasa.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa, mchezo wa kuuza maeneo haya, unaongozwa na Kiomoni Kibamba (Mkurugenzi Jiji) na Katibu Tawala Nyamagana, ambao wamemtanguliza Afisa Mtendaji wa Pamba Bw. Mugisha akishirikiana na Diwani wa Nyamanaro Chadema.

Diwani huyo wa Nyamanoro yeye ni mtafuta wateja (wafanyabiashara) ambao wenye uwezo wa kutoa pesa bila kutoa taarifa ya namna wanavyouziana eneo hilo.

Inaelezwa kuwa baada ya wizi wao kubainika wameanza kujinasua na kujitoa kimasomaso kwamba pamoja na wao kuuza maeneo hayo hakuna kiongozi atakaye wafanya chochote.

Viongozi hao wanajinasibu kuwa, kabla ya kuuza maeneo hayo, walijipanga na kuwaweka sawa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali hivyo hawawezi kuchukuliwa hatua yeyote.

Habari iliyoandikwa siku mbili zilizopita

DAS Nyamagana, Afisa Mtendaji Pamba, Diwani Chadema wapiga Tsh. Milioni 45 za shule ya Pamba

Pesa hizo zinatokana na kuuza eneo la wazi la shule kwa wafanyabiashara wakubwa

Katibu Tawala wilaya ya Nyamagana, Yonas Alfred, Afisa Mtendaji wa kata ya Pamba Jonas Mugisha na Diwani wa Kata ya Nyamanoro, Abubakar Kapera wanashirikiana kuuza eneo la shule ya sekondari Pamba kwa wafanyabiashara wakubwa jijini Mwanza.

Wafanyabiashara wanaouziwa eneo la shule hiyo ni wale ambao walikuwa na maduka katika soko kuu la Mwanza na wale waliokuwa jengo la Mwadeco.

DAS huyo na wenzake wanauza eneo hilo la shule ambalo lipo mbele ya geti la kuingia na kutoka shuleni hapo kwa wafanyabiashara ambao huingiza kontena hizo nyakati za usiku.

Jinsi wanavyouza eneo hilo ni kwamba wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa wanauziwa eneo kuanzia Tsh. Milioni tatu hadi sita ili waweke makontena.

Wengine wanaoweka vibanda vidogo vya chuma wanauziwa kuanzia Tsh. Milioni moja hadi milioni Tatu kitendo ambacho wafanyabiashara wengine wameanza kugoma na kuomba kurudishiwa pesa zao.

Kontena kubwa ambazo zimewekwa eneo hilo la shule ya sekondari ya pamba zipo kontena sita huku vibanda vidogo vya chuma vipo 20.

Kwa hesabu za kawaida kontena hizo zote sita, zimeingiza kiasi cha Tsh. Milioni 20 huku vibanda vidogo vimeingiza Tsh. Milioni 25.

Jumla ya pesa zote ni Tsh. Milioni 45 ambazo zimeingia mifukoni mwa watu hao watatu licha ya watu wengine wakifichwa ambao ni mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, Mwanasheria wa Jiji Bi. Maliam na Afisa biashara wa Jiji.

Kutokana na wafanyabiashara hao kuvamia eneo hilo na kuweka makontena yao kwa usaidizi mkubwa wa viongozi hao, taarifa zinasema tayari bodi ya shule ya Pamba imekutana.

Bodi hiyo ya Pamba imekutana jana na leo na kufanya kikao, wakihoji kwanini eneo lao la shule kuvamiwa na wafanyabiashara bila kushirikishwa na kwamba eneo hilo limekuwa likitumiwa na wanafunzi katika shughuli mbalimbali.

Bodi hiyo inadai kwamba kabla ya kukutana walipeleka malalamiko yao kwa mkurugenzi wa Jiji la Mwanza lakini hakuna hatua zozote ambazo zilichukuliwa na kuwalazimu kuandika barua kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Bodi hiyo inasema barua ambayo imeandikwa kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, pia itaandikwa nyingne kwenda ngazi ya kitaifa kwa msaada zaidi.

Hapo chini ni picha za kontena zilizoshushwa jana

Attachments

  • IMG20191017165321.jpg
    IMG20191017165321.jpg
    243.6 KB · Views: 3
  • IMG20191017165317.jpg
    IMG20191017165317.jpg
    194.2 KB · Views: 3
  • IMG20191017165706.jpg
    IMG20191017165706.jpg
    285.1 KB · Views: 3
Hizi details zote unazotoa wewe zinaonekana kama una uchungu fulani juu ya hilo jambo, mwandiko wako haufichi hisia zako pole sana.
 
Lipumbavu litakuwa limekosa mgawo!
 
Back
Top Bottom