Wamachinga wasababisha sintofahamu jijini mwanza

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kuna taarifa kua wamachinga jijini mwanza wamegoma kugama katikati ya jiji la mwanza ni hivi sasa polisi wana randaranda jijini humo tayari kwa kuwaondoa kwa nguvu endapo wataendelea kugoma kuondoka kwa hiari yao. Inasemekana tayari wafanya biashara wengine wamefunga maduka yao kukwepa vurugu ambazo zinaweza kutokea. Mwenye habari zaid kutoka mwanza atujuze chanzo: mkazi mmoja wa mwanza..
 
Ofisi za Halmashauri ya jiji sasa hivi zimezungukwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) huku kukiwa na idadi kubwa ya askari wa kutuliza ghasia. Nahofia Tunisia ya Tanzania isije anzia Mwanza.
 
Asante kwa taarifa, Samahani sio mahali pake lakini sahihisho la lugha. Hili neno sintofahamu ni neno la kiswahili au unaungana mkono wa baadhi ya watu wanaoharibu kishwahili? Kwa nini usitumie neno mtafaruku, kuparaganyika, wasiwasi, kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.

Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
 
Hawa ndugu zetu wangekuwa handled carefully na kuacha siasa nje ili waweze kuendelea kujikimu!
 
Asante kwa taarifa, Samahani sio mahali pake lakini sahihisho la lugha. Hili neno sintofahamu ni neno la kiswahili au unaungana mkono wa baadhi ya watu wanaoharibu kishwahili? Kwa nini usitumie neno mtafaruku, kuparaganyika, wasiwasi, kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.

Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
Lakini si umeelewa? kiswahili kinakua hata hilo neno kuparanganyika zamani lilitumiwa na watu wa kutoka sehemu za Musoma zaidi lakini lilipozoeleka likawa moja ya neno la kiswahili.
 
yaliytokea tunisia ndio yanaanza leo tanzania nawasihi ndugu zetu wamachinga wa Mwanza muongoze jahazi sisi tupo nyuma yenu
 
Lakini si umeelewa? kiswahili kinakua hata hilo neno kuparanganyika zamani lilitumiwa na watu wa kutoka sehemu za Musoma zaidi lakini lilipozoeleka likawa moja ya neno la kiswahili.

Nimeelewa na ndio maana nimesema asante kwa taarifa, hapo nilikuwa natoa angalizo. Sikatai neno kupagaranyika linaweza kuwa limetokana na matumizi ya watu wa musoma kama ambavyo maneno mengi ya kiswahili yalivyochukuliwa toka lugha nyingine ( kutohoa). Lakini huwezi kutumia neno sintofahamu ukiwa na maana ya wasiwasi au huko sio kutohoa ni kitu kingine kabisa .

Pili kuzoeleka kwa neno sio lazima kuwa neno hili litatoholewa, ili liingie kwenye msamiati Bakita lazima walikubali na kwa hili neno sidhani kama watakubali kulikubali kwenye maana hiyo mnayotaka tuifahamu. Ndio maana maneno kama lisaa lilitumika likazoeleka kalini bakita wakasema hapana sasa hilo nenohaliktumini kabisa.

Kusahihishana ni kuendeleza kiswahili fasihi, ukiona mtu amekosea usisite kumsahihisha ukikaa kimya tutaendelea kutumia maneno yanayozoeleka lakini yasiyokubalika na hivyo hayatotoholewa na bakwata.
 
Bakwata??!! Anyway kama alivyosema quinine kiswahili kinapanuka. It is now moving from one to one function to one to multiple function kwa maana kwamba neno moja linakua na maana zaidi ya moja. Anyway tuendelee na mada ya wamachinga.
 
Hapo juu ulimaanisha BAKITA? Maana Bakwata ni kwa ajili ya Waislaam.

Umeomba tusahihishane na nimeanza. Asante kwa maelezo ya hapo juu....
 
ni kweli mimi nilikuwa rock city ndani nikasitukia watu kama 1 m wanaandamana huku wakiwa na malungu wakielekea jiji lakin kila sehemu wakifika wanalusha mawe kwenye maduka ndo maana maduka walifunga. Lakini zali limesababishwa na manspaa kwasababu kunamaeneo ya makoloboi wamachinga walikuwa wamepimiwa maeneo hayo lakin baada ya hapo wamachinga walianza kujenga vibanda sasa ilikuwa ni mbele ya maduka ya watu, wenye maduka walipoona wamezibwa wakaenda kwa mkulungezi wakamwambia wao hawataweza kulipa kodi kwa sababu hawauzi, wamekingwa na mamachinga. Mkulungenzi akawaamulu wamachinga waondolewe mara moja. Kwahiyo ndo walikuwa wanaandamana kupinga kitendo hicho huku wakitishia kuchoma moto maduka yote ya makoloboi. Lakini hali imeturia baada ya polisi kuzagaa mji mzima
 
Unajua maana ya watu 1m au unawadhania.
 
Asante kwa taarifa, Samahani sio mahali pake lakini sahihisho la lugha. Hili neno sintofahamu ni neno la kiswahili au unaungana mkono wa baadhi ya watu wanaoharibu kishwahili? Kwa nini usitumie neno mtafaruku, kuparaganyika, wasiwasi, kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.

Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu

unajua angalau kuna maneno ya kiswahlil yasiyo rasmi lakini yanafanana na maana zake hili la sintofahamu ni upuuzi wa hali ya juu, nasikia kichefuchefu kulisikia, mtanisamehe waungwana.
 
kimuyemuye na hofu. Tusiharibu kiswahili.

Nimekuwa nikisikia mara nyingi redio one wakitumia neno hili sintofahamu
Mkuu hata hilo hapo kwenye Bold sidhani kama lina tofauti sana na alilotumia jamaa nadhani zote ni Slang au unaweza kunipa maelezo zaidi....
 
Duh! Hivi mkoje ! Sasa mtu kaleta mada ya wamachinga mwanza, alafu watu wanapindisha mada kiswahili kiswahili. Kha
 
Gazeti moja la mwanza limeandika kandoro atofautiana na mkurugenzi wa jiji (kabwe) inaonekana kandoro alikubali wamachinga kufanya shughuli zao eneo la makoroboi ambalo liko maeneo ya mjini lakin mkurugenzi kachomoa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom