WAMA ya Mama Salma ni NGO au kitengo cha CCM?

WAMA ya Mama Salma ni NGO au kitengo cha CCM?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,243
Reaction score
44,520
CCM ni sawa mwembe ambao hurushiwa mawe kutokana na matunda yake - mama salma kikwete
Mke+wa+Rais+Mama+Salma+Kikwete+akiwanadi+wagombea+Ubunge+Jarome+Bwanausi+%28+LILUNDI%29+,MARYAM+KASEMBE+%28MASASI%29+MTWARA.JPG

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete (katikati) akiwanadi wagombea Ubunge wa jimbo la Lilundi,Bw. Jarome Bwanausi na wa jimbo la Masasi, Bi.Maryam Kasembe mkoani Mtwara juzi.

Hawa+ni+baadhi+yawagombea+Udiwani+wa+Jimbo+la+Masasi+%28MTWARA%29+wakinadiwa+na+Mke+wa+Rais+Mama+Salma+Kikwete-27-9-2010.JPG

Baadhi ya wagombea Udiwani wa Jimbo la Masasi,Mtwara wakinadiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete katika mkutano uliofanyika juzi jimboni humo.

(Kutoka kwa Michuzi Blog)

My Take:
Ninaelewa Ridhiwani anapofanya kampeni anafanya kama kiongozi wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (japo kimsingi anampigia kampeni babake kwani wapo viongozi wengine wa vijana ambao wana nafasi ya juu kuliko yeye na hawapati nafasi na ujiko kama wa wake). Sina tatizo sana na Ridhiwani kufanya hivyo.

Lakini mama Salma naye ni kiongozi ndani ya CCM nadhani ni mjumbe wa CCM wa nafasi fulani sikumbuki! Lakini katika hizi kampeni kila anakoenda anatambulishwa kama kiongozi wa Taasisi ya wa Kina Mama (WAMA). Nina maswali:

a. Taasisi hii ni kitengo cha Ikulu (Ofisi ya First Lady)?
b. Taasisi ni NGO iliyoanzishwa kwa sheria ya NGOs? Kama ndiyo je NGOs nyingine zina haki ya viongozi wake kumpigia mgombea wanayemtaka au chama wanachotaka kampeni? Sema kwa mfano TASWA au LEAT wanaweza kuanza kupiga kampeni waziwazi za chama au mgombea wanayemtaka?
c. Gharama za mama Salma zinalipwa na CCM (kama Kinana alivyotaka tuamini) au zinalipwa na WAMA au na Serikali?
d. Kama mama Salma anafanya hivyo kama kiongozi wa CCM kwanini wanatumia ujiko wa WAMA?
e. Yumkini WAMA ni chombo kimojawapo cha CCM?
 
Habari ndo hiyo MMK hakuna chenga wala nn! WAMA=IKuLu=CCM, NGOs zingine zijaribu kupiga kampeni waziwazi uone zitakazofanyiwa!
 
WAMA ni CCM na CCM ni Serikali so WAMA ni serikali. Anatumia kote kote. After all JK ndiye mwajili wa wafanyakazi wote TZ anaweza kuwafukuza kama mbayuwayu wakikataa kutii maelekezo yake. Sim mmeona yule DED wa kilimanjaro?
 
Heshima kwako Mzee Mwanakijiji,

Mkuu Mama Kikwete alipofanya ziara mkoani Mara alitumia gari la mkuu wa mkoa ambalo liliwekwa namba za kiraia lakini wakasahau kufuta namba zilizochorwa kwenye vyioo vya gari.

Mama Kikwete anapigania maslahi ya mumewe na familia yake. Bado anatamani aendelee kufaidi misafara mikubwa na ving'ora vya polisi hana ajenda ya kuwakomboa watanzania bali familia yake.
 
hakuna swali hapa, WAMA ni ccm na alishasema mwenyewe salma kwamba wama haiwezi kufanya kazi chini ya chama kingine, sasa mnataka kujua nini tena?
 
Nadhani kuna mtu anahitaji kufungua kesi dhidi ya WAMA kushiriki siasa.
 
Ameyasema hayo akichangia hoja ya wizara ya maendeleo ya jamii na pia kasema vongozi wote ni wa CCM.
 
Waziri kajikanyaga sana,mwisho nae karopoka WAMA ipo kisiasa
 
Huo ndo ukweli, WAMA inatumika kwa maslahi ya kisiasa zaidi! Ndo maana body memba wote ni mainterahamwe..
 
waziri mwenye amethibitisha kuwa mama salma kikwete eti hufanya siasa kwa kumsaidia mume wake kikwete aibu kubwa sana kwa serikali ya ccm
 
wagalatia mbona mna wivu na WAMA? mbona Enzi za Mama Mkapa na EOTF mliufyata kimyaaa
 
Kuna tofauti kubwa sana namna mama ana mkapa alivyobehave kama FL na jinsi anavyofanya salma kikwete. Full uswahili kwa gharama za walipa kodi (serikali).
 
wagalatia mbona mna wivu na WAMA? mbona Enzi za Mama Mkapa na EOTF mliufyata kimyaaa

Familia ya Mkapa ili kuwa familia iliyo elimika na ya kistarabu. Wewe uliona wapi mama Mkapa akiitumia EOTF katika masuala ya kisiasa kumsaidia mumewe? Kwanza Mkapa mwenyewe hakuwa anahitaji msaada wa familia kufanya kazi zake na zaidi alitenda kazi za kirais kuliko zile za kichama ndio maana Deni la nje lilikuwa linalipika na Hazina yetu ilikuwa inaweka akiba.
Sasa WAMA imekuwa kama UWT na inatumia fedha wakati mwingine za serikali.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
1400391073456.jpg

Anaabudiwa kuliko Rais
Ana nguvu ambazo Katiba haizitambui.
 
Nashangaa kibaraka msajili ana kazi gn!tunaomba jibu wama ni chama cha siasa au ni kabranchi kaunyonyaji.
 
Back
Top Bottom