Escaper
JF-Expert Member
- Nov 11, 2018
- 1,780
- 3,241
Linapokuja suala la kuingizwa mjini haijalishi wewe ni born town au wakuja ni "timing" tu.
Kuna kipindi michezo ya kulizana pesa ilikua mingi sana, nakumbuka kuna mwaka katika mishe mishe zangu za town nikakuta kikundi cha watu kimekusanyika basi nikaona sio tabu ngoja nosogee..
Ile nafika nakuta kuna mchezo unachwezwa, mkanda wa suruali unazungushwa harafu unachomeka peni kisha mkanda unakunjuliwa ,peni ikiwa ndani ya mkanda unakula Bingo/pesa.
Sasa baada ya kuusoma mchezo kila nikicheki kuna mdada anakula tu pesa nikauliza bei gani jamaa akasema weka elfu 2 unapata elfu 4.
Kazi ikaanza kila nikichomeka peni hola! nikichomeka hola!
Aisee nilipigika hela kinoma, mbaya zaidi niliagizwa mzigo wa duka la maskani, nikawa nimepaniki pale nikidai kuwa hela sio zangu basi liliibuka njemba moja pale lina mbavu hatari ikanibidi tu nisepe
ila sitasahau ile siku katika maisha yangu na kamwe siwezi sogea kwenye mikusanyiko.
Hivi kuna mikoa hii michezo ya kuingizana chakike bado ipo?? Wewe ushawahi pata kadhia ya kupigwa hela kizembe kwa aina yoyote ile ...Tiririka !