Ukitaka kumchinja ng'ombe halafu akafanikiwa kukurupuka basi wote mliokuwa hapo mtafute pa kwenda hasa yule aliyeshika kisu.
Nawashangaa watu wanavyogombea kuchinja. Hawamjui ng'ombe vizuri. Yule ni nyati, tofauti ni kwamba anafugika.Mkeshaji ushawahi kukumbana na hii adhma nini maanake unavyoongea kwa hisia na msisitizo,poleeeeeee kama ulikutana na hicho kivumbi maanake najaribu kupiga picha ila sipati picha ulivyokuwa unaupangua upepo,Haaaahaaaaahaaaaa[joking}
Nawashangaa watu wanavyogombea kuchinja. Hawamjui ng'ombe vizuri. Yule ni nyati, tofauti ni kwamba anafugika.
Ukitaka kumchinja ng'ombe halafu akafanikiwa kukurupuka basi wote mliokuwa hapo mtafute pa kwenda hasa yule aliyeshika kisu.
Mkeshaji ushawahi kukumbana na hii adhma nini maanake unavyoongea kwa hisia na msisitizo,poleeeeeee kama ulikutana na hicho kivumbi maanake najaribu kupiga picha ila sipati picha ulivyokuwa unaupangua upepo,Haaaahaaaaahaaaaa[joking}
Kama ndo hivyo sirudii tena kulilia kuchinja
Hapo ukifanikiwa kuchomoka lazima uwe rasta(jah rastafarai)
Wakuu msiombe kukutana na dhahama hiyo,kuna siku tuko msibani tunataka kuchinja,basi akakurupuka,ilikuwa mshikemshike almanusra utokee msiba mwingine ndani ya msiba...
Endeleeni kulilia kuchinja na mjifunze na riadha pia!
Haaaaaaahaaaaaaahaaaa nacheka kama vile mazuri naomba tu unisamehe mkuu maanake napiga pichwa kichwani naona watu kibao msibani kila mtu akitafuta njia yake wallahi nashindwa kuhimili kicheko,hata hivo poleni sana mkuu.
Yaani ulivyocheka wewe najikuta na mimi nikicheka nikikumbuka tukio lile,ilikuwa mshikemshike kila mtu akitafuta njia yake hakuna cha wanawake wala wanaume, halafu alikuwa akimwandama jamaa mwenye kisu.Kilichomuokoa jamaa ilikuwa ni kurukia juu ya mpera wa pale kwenye ile nyumba, basi alipomkosa ndio akaanza kuandama kila mtu anayemuona mwisho akatokomea maporini....
Daaaaahhhh basi ilikuwa bonge la patashika kuwahi kutokea,sasa mkuu unamaanisha wewe ulikimbia hadi ukawa huna habari kabisa na waifu?Je kama ungeona waifu tu ndo anaandamwa na huyo ngo'mbe ungechukua hatua gani?
Bahati nzuri waifu alikuwa ndani akimfariji mjane, ila ingekuwa waifu ndio kaandamwa wala sijui ingekuwaje maana kumsogelea yule ibilisi ilikuwa ni kubeep kifo....