Waliotapeli kwa jina la Dr. Abbas na kuzusha kifo cha Dr. Mwakyembe wakamatwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi watuhumiwa hao ni Innocent Adam Chengula na Tarzan Alfan Mwambengo wanaodaiwa kutumia picha na jumbe za simu zinazomuhusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo kwa lengo la kutapeli pamoja na kuzusha kifo cha Dr. Mwakyembe.

Baada ya upekuzi walikutwa na Kadi za Simu zilizosajiliwa kwa majina yasiyowahusu, pamoja na jumbe zinazosomeka “Kaka naomba niazime Mil 3, Alhamisi nitarudisha”. na Kaka nina mtoto naomba umpatie kazi hapo kwako amesomea Bachelor of Commerce in Accounting"

Watuhumiwa hao wamekutwa na Laptop 1, Simcard 9 zenye usajili wa majina na mitandao tofauti, Moderm 1, Kipaza Sauti 1 na Simu 3. Katika tukio la kuzusha kifo cha Mwakyembe, mtuhumiwa alitumia mtandao wa Youtube na kuweka video ikiwa na maneno "BREAKING NEWS, HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKWEMBE".
53EE8CF0-9F4F-4927-806A-32E2E8F81D22.jpeg

3B76B1DB-2257-407B-8553-D43B4857EB03.jpeg
 
Watuhumiwa hao wamekutwa na Laptop 1, Simcard 9 zenye usajili wa majina na mitandao tofauti, Moderm 1, Kipaza Sauti 1 na Simu 3. Katika tukio la kuzusha kifo cha Mwakyembe, mtuhumiwa alitumia mtandao wa Youtube na kuweka video ikiwa na maneno "BREAKING NEWS, HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKWEMBE".
Kwakuwa ni Mwakyembe wameweza ila akina yakhe wanalalamika kila siku kutapeliwa lakini matapeli hawakamatwi, je wanashirikiana na nani?
 
Watoto wa YOUTUBE noma sana!

Kuna kamoja kaliandika "BREAKING NEWS WALIOMUUA MAGUFULI WAKAMATWA"
..
 
Back
Top Bottom