Waliosoma vyuo Tanzania walipe madeni!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliosoma vyuo Tanzania walipe madeni!!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kamundu, Jun 15, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi nimekuwa nikifuatilia maandamano ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu na nikagundua kuna matatizo makubwa ambayo watu hawayaongelei. Gharama za kumsomesha mwanafunzi mmoja hadi kumaliza shule ni TSH 15,000,000. Tatizo ni kwamba tuna system ambayo serikali haidai pesa baada ya wanafunzi kumaliza shule na hivyo kuchukulia posho kama msaada badala ya mikopo. Shule si bure na wanafunzi inabidi wajue hivyo lakini serikali vilevile inabidi ijue kwamba kutokukusanja madeni si tatizo la wanafunzi wa sasa bali ni tatizo ya serikali kutokana na kushidwa kukusanja au hata kufuatilia madeni. Tuanze na raisi wetu je amelipa deni lake la chuo?? inabidi tuwe na system ambayo watu wanalipa madeni ya shule. Mimi binafsi nina deni hapa marekani la $38,000 na ninalipa $156 kila mwezi kwa miaka 20. Nikipanga kulipa mapema ni sawa lakini si bure na siwezi kukimbia deni kwasababu serikali itakuja kwa mwajiri wangu na kuchukua pesa kila mwezi.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Walipe kutoka wapi wakati hawana ajira?acha kuropoka wewe marekani sio bongo.
   
 3. H

  Haki JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unakompera nchi mbili zenye tofauti kubwa ktk kila kitu.
  Besides, Serikali kwanza inatakiwa ianzishe Credit Bureu ambayo itakuwa inarekodi data zote za WTZ wanaokopa hela kutoka bank. Hii itaweza kuzisadia sana banks kuweza kutrack watu ambao wanakopa hela. Pili, hizi Universities zinatakiwa zijiendeshe wenyewe bila ya kuitegemea sana serikali.Vyuo vikuu vinatakiwa viwe independent institutions. Kwa hiyo Udom, na vyuo vingine vinatakiwa vitatue matatizo yao wenyewe bila ya kuitegemea Serikali. Fikra za Kijamaa zinafanya mpaka maDean wasijue mikakati ya kuendeleza shule, na badala yake wanataka serikali iwasaidie wao na wanafunzi wao. Huu ni ujinga mkubwa uliopo vyuo vikuu nchini. Wake up!!
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Raisi ana ajira je kalipa? kuna watu wangapi wamesoma vyuo vya serikali kwa mkopo na wanakazi je wamelipa. Kama unasoma shule na hutaki kulipa deni basi unasoma kwa msaada na kama ni msaada basi uwezi kudai pesa ya msaada bali ya mkopo. Kwanini NSSF na mashirika mengine yana pesa kama watu hawana kazi??
   
 5. N

  Nguto JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,653
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nani kakwambia hawalipi?
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Walipe nini wakati wakati wabunge wanapewa fedha nyingi za bure kufanyia zinaa tu Dodoma kwanini zisiende mashuleni kulipia wanafunzi?
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Walioiba hela za EPA wakimaliza kuilipa serikali then ndio na mimi nitaanza kulipa hayo madeni ya tuition.
  Mwambie raisi wako akusanye hela za Kagoda kwanza then ndio aje kunidai. Otherwise leave me alone!
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wewe hujui kinachoendelea Tz kaa kimya!unajua wanaotakiwa kulipa madeni ya chuo ni waliomaliza chuo kuanzia mwaka upi?wenye ajira wanalipwa sh ngapi ili waweze kulipa madeni na kujikwamua wao na familia zao kimaisha?we endelea kubeba box huko kwa sababu hujui huku hata kazi ya kubeba box haipatikani.
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  NSSF inapata fedha kutoka kwa wanachama wake. Huwezi kuelewa hali ya TZ kama una mpango wa kukaa huko 20yrs na hata ukielezwa hapa utaendelea kutoelewa kwa sababu unataka kulinganisha TZ na US. Njoo huku uone mwenyewe mkuu hakuna kazi na kama ziko ni za kuhama hama kutoka kampuni hii au shirika hili kwenda lile. Kwa kipindi cha miaka 6 mtu anaweza kufanya kazi zaidi ya mashirika 5 kwa hiyo serikali inashindwa kum-track kwa sababu hakuna system in place ya kufuatilia mkopaji.
   
 11. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Nashindwa kukupata vizuri pointi yako, unataka kuniambia kuwa migomo vyuoni inatokana na serikari kushindwa kukusanya madeni. Tatizo si wanafunzi kugoma ila matatizo yanaanzia kwa viongozi wa serikari mara nyingi fedha za mikopo ya wanafunzi wanazifanyia biashara zao binafsi mpaka mgome ndio mnapewa hivyo kautaratibu hako kemekwisha zoeleka hapa bongo

  Suala la ulipaji wa madeni halipo clear kwani linawabana wale walioajiliwa either sector binafsi au serikarini. kwa mfanya biashara system haipo clear kwake kwani sisi wengine tuliletewa barua na kuambiwa mwezi ujao utakatwa 50000 kwa kipindi cha miezi 92 so utapiga hesabu mwenyewe. ila naunga mkono watu walipe ili wengine wasome pia kwa serikari kama mko fasta kwenye kudai basi na kutoa sio mpaka mtu agome
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Webmaster je ni kwanini una move hii topic? hakuna topic nyingine kama hii na watu kubishana ni kitu kizuri kwani hili swala la elimuni muhimu. Kama una move basi acha message kwamba unaipeleka wapi .
   
 13. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,776
  Likes Received: 7,094
  Trophy Points: 280
  dah mi skujua kama intelligence wanaweza ropoka maneno kama haya, now wanafunzi wa elimu ya juu tunadai nyongeza ya boom, halafu kulipa hatutaki then tusipoongezewa twalalamika, kwa wale wasio na ajira its okay wasipolipa but kwa wenye ajira wasipolipa huo ni usela mavi,

  na tukumbuke katiba mpya inakuja, kipindi tupo socialism(sera ya kijamaa) ilikua ni 100 asilimia walipiwa ikawa tunatransform kuja capitalist waka introduce cost sharing. Sasa moja wapo ya kipengele cha katiba mpya nchi itaingia rasmi kwenye sera za capitalism hii inamaanisha serikali itatoa mkopo kwa wanafunzi ambao ina interest nao kama waalimu madaktari na mainjinia wenzangu na mimi kina bcom na pspa sjui twakimbilia wapi.

  Tujifunze kufanya mema ili serikali ikikosea tuweze kuikosoa vizuri, tukishindana na serikali kufanya vibaya nchi hii tutaipeleka wapi????
   
 14. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  hilo nalo neno mkuu...
   
 15. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nani ka kuambia watu hawalipi? hakuna aliye na deni chuo halafu halipi labda bado hana ajira. hii ni sheria na kama mwairi hatawasilisha anashtakiwa. We nawe unauza sura marekani hakuna chochote au umetaka tu watu wakujue uko marekani? what is marekani bwana? unachokipata huko almost sawa na kipato cha bongo sasa unagain nini huko? huo ni ulimbukeni rudi ujenge taifa lako
   
 16. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Hoja yako ni ya msingi kwa mustakabali wa elimu ya taifa letu. Hata hivyo mimi nionavyo kwa Tanzania sio rahisi kukusanya madeni kutoka kwa wahitimu kwa vile serikali haijui wako wapi na wanafanya nini. Suala la mikopo ya elimu ya juu tulillazimishwa na wazungu ili tuendelee kupatiwa misaada na mikopo katika bajeti ya serikali.

  Kwa kuwa elimu bora ni muhimu sana kwa ustawi wa taifa lolote mimi napendekeza kuwa bodi ya mikopo iliyopo ivunjwe na iundwe bodi ya mfuko wa elimu ya juu ambayo itasimamia na kuratibu vyanzo vya mapato kwa ajili ya elimu ya juu. Hivi sasa tunao watumishi wa umma wapatao 300,000 na sekta binafsi tuchukue idadi hiyo hiyo hiyo, lakini pia kuna wafanya biashara wakubwa ambao wanaweza kuchangia elimu ya juu. Hebu tuchukue idadi ya watu 700,000 tu ambao kama watakubali kutoa TZS 10,000 kila mwezi maana yake ni kwamba tutakusanya TZS 7,000,000,000/= kwa mwezi mmoja pekee, kwa mwaka ni sawa na TZS 84bn/-. Fedha hii pamoja na vyanzo vingine ambavyo bodi itavipata wapatiwe vijana wetu wa vyuo vikuu wasome bure kama vile JK na wenzake walivyosoma kwa kodi na michango ya Watanzania.

  Utaratibu wa sasa eti wa kuwakopesha haufai kabisa kuendelea kutumika, ni wa kibaguzi na hautendi haki kwa kizazi cha sasa.
   
 17. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Sikushauri urudi huku cos ukirudi ajira hakuna bora uendelee kubeba mabox na ucku uwe bar made huko kwa obama huku ukija na elimu yako ya huko na vyuo vya vichochoroni utakuna nazi kitaa hadi mwisho utabaki u know what am say,when I was in america...tena bar baada ya kupewa ofa ya rafiki yako unayemlazimisha alipie tution fee mwenye ajira yake ndogo na mshahara wake mdogo
   
 18. N

  Ngoswe11 Member

  #18
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kutuzingua wewe dah sera gani hizo unatuletea hapa.

  Millioni 15 kitu gani bana mbona unatuzingua! Watu tunakamua shule 2 years ina-cost Million 40 TSH, per year 20Millions excluding accomodations na wanaolipa hizo fedha hawatudai hata senti tano tuwarudishie sembuse hizo Milion 15 kwa miaka 3 au 4. We wa wapi lakini?

  Je na hao mafisadi wanaokula hizo hela? Akina VILAZA kama kawambwa yuko pale kutengeneza dili tu kuiba fedha za umma sasa mtoto wa mkulima ndo alipe sio?

  We vipi bana, kama vipi nenda kalale usituletee habari zako! kama BOOM tulishakula na hatutolipa kamwee hadi mafisadi waondoke! POLEEE kiongozi lakini wafikishie huo ujumbe hao waliokutuma! UMESIKIA enheeee?
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nakatwa wekundu naona mpaka deni likaisha!
  Ila ata sijui izo ela zaenda wapi maana hii serikali siiamini ata kidogo
   
 20. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo la Tanzania kubwa ni hili tunataka kila kitu bure wakati ni masikini je pesa ya shule itoke wapi? Mikopo imeanza sikunyingi kuanzia wakati wa Kikwete kwani pesa ilitoka wapi kama sio deni ambalo Tanzania ilikopa IMF na World Bank kwa Interest za juu ili watu wasome. Kama una system ya watu wanaotaka vitu vya bure hata pale wapatapo mikopo huwezi kuwa na nchi yenye maendeleo hata siku moja
   
Loading...