Waliosimamishwa UDSM wahojiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliosimamishwa UDSM wahojiwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, Jan 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), jana ulianza kusikiliza utetezi wa wanafunzi 40 kwa tuhuma za kuleta fujo na uchochezi uliopelekea mgomo chuoni hapo na kusababisha wanafunzi 13 na wenzao 86 kusimamishwa kwa muda usiojulukana.

  Rais wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso) aliyesimamishwa kwa muda usiojulikana, Simon Kilawa, alisema Baraza la Chuo hicho umeuelekeza uongozi wa Chuo, kuwahoji wanafunzi wote waliosimamishwa na kusikiliza utetezi wao, ili kuona kama kuna

  mwanafunzi anayestahili uamuzi mwingine, tofauti na kusimamishwa na kufukuzwa.

  Kilawa alisema mpaka saa 7:00 mchana jana, ni wanafunzi wawili waliokuwa wamekwisha hojiwa, ingawa utawala ulikuwa umepanga

  kuwahoji wanafunzi 40, na wengine waliobaki walitarajiwa kuitwa mbele ya uongozi wa chuo kwa ajili ya kujitetea leo.


  NIPASHE ilishuhudia wanafunzi wakiwa wamekaa katika vikundi vikundi wakisubiri muda wao ufike ili wajitetee huku akiitwa

  mwanafunzi mmoja mmoja na kutokea mlango mwingine ili pale anapomaliza utetezi wake asipate fursa ya kuonana na wanafunzi wengine.

  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivi karibuni kimekumbwa na vurugu na migomo ya mara kwa mara, hali iliyopelekea uongozi na Baraza la Chuo kuwafukuza wanafunzi 13 na kuwasimamisha wengine 86 kwa muda usiojulikana, wakiwemo viongozi wa Daruso.  CHANZO: NIPASHE

   
 2. h

  hahakiki New Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakati mwingine mkigoma mhakikishe hao mbwa wa kikwete (mkandala, mgaya, na maboko) mnawatia majeraha la sivyo mtakuwa mnapotezewa muda kwa kujifanya mnagoma kwa amani.
   
Loading...