The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,903
- 2,884
Leo magazeti yameripoti juu ya kukosekana kwa fedha za kugharamia mitihani ya moco iliyopaswa kufanyika ambayo ni muhimu sana kwani mitihani hiyo ni kwa ajili ya kuwapima watahiniwa watarajiwa ili kuwapa fursa walimu na wadau wengine wanaohusika kujua wanapaswa kuongeza nguvu eneo gani kukwama kwa fedha hizo kunamaanisha kwamba tunachezea kamali watoto wetu kwa kuwapeleka bora liende.
Kinachorudisha nyuma nchi hii ni uwepo wa watu wanaoshabikia kila kitu hata kama kiuhalisia kitu hicho kina madhara au hakiwezi kuleta ufanisi tunaoaminishwa, wao hujali tu kama kimesemwa na mtawala. Ninyi watu hebu badilikeni mseme ukweli tuisaidie nchi yetu.
Ni muhimu sasa serikali ikaja na mpango kabambe wa kuinusuru elimu yetu na sio hii elimu bure kwani elimu bure ndio kaburi la elimu ya nchi. Kushndwa kupata fedha ya moco ni mwanzo tu tutaona mikwamo mingi sana.