Waliorudi rwanda waandaliwa ardhi....

Waliorudi rwanda waandaliwa ardhi....

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844

Rais Paul Kagame wa Rwanda

WAKATI agizo la Rais Jakaya Kikwete la wakimbizi haramu likiendelea kutekelezwa na kupokewa vizuri na Rwanda, Bodi ya Kilimo ya nchi hiyo (Rab) imetenga zaidi ya hekta 300 za ardhi kwa ajili ya wananchi wanaorejea.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, ambaye ni Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Elizeus Mushongi, alisema hadi jana, wahamiaji haramu 7,814 walikuwa wameondoka mkoani Kagera na ni walioripoti katika vituo vya Uhamiaji mkoani hapa.

Mushongi alisema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wahamiaji wanaoondoka kupitia ‘njia za panya’ ambao ni wengi zaidi.

Alisema katika makundi hayo ya wahamiaji haramu, ambao wanatoka Uganda, Burundi na Rwanda kuna wengine ambao hawataki kurudi kwao na idadi kubwa ya wasiotaka kurudi ni Wanyarwanda.

Kwa mujibu wa Mushongi, Wanyarwanda hao wakati wakijiorodhesha katika vituo, wamekuwa wakisema wanakwenda Burundi na Uganda na hata walioonekana kupita ‘njia za panya’, walikuwa wakienda nchi hizo pia.

Alisema katika kituo vya Murusagamba, walipita Wanyarwanda 35 wakienda Burundi, kituo cha Mutukula, Wanyarwanda 13 wakielekea Uganda, Bugango 22 wakienda Uganda na Kanyigo saba, wakienda Uganda.

Katika kituo cha Kabanga, Warundi 522 walijisajili kurudi kwao na Warundi 10 katika kituo cha Murongo, walisema wanakwenda Uganda. Katika kituo hicho, Wanyarwanda 166 walipita wakienda Uganda.

Rusumo yaongoza

Aliongeza kuwa kituo cha Rusumo kinaongoza kwa kupitisha wahamiaji haramu wengi, waliofikia 4,748 wakienda Rwanda.Kituo cha Murongo kilipitisha wahamiaji 332, Murusagamba 78 na Mutukula 31 na eneo la Mgoma ambalo halina vituo vya Uhamiaji, walijisalimisha 1,734 katika ofisi za vijiji.

Kuhusu silaha zilizosalimishwa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi, alisema silaha 42 zilisalimishwa na wahamiaji hao.

Alisema miongoni mwa silaha hizo, nyingi ni magobori huku akisema Jeshi lake limejipanga kukabiliana na wahamiaji ambao hawajaondoka. Alisisitiza kuwa wahamiaji watakaokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Rwanda yakataa ng’ombe

Mushongi aliendelea kusema idadi ya ng’ombe walioondoka hadi jana ni 1,996 kupitia kituo cha Rusumo huku wengi wakienda Uganda, kwa sababu Rwanda haitaki idadi kubwa ya ng’ombe.

Kitakwimu, alisema kati ya wahamiaji haramu walioondoka kwa hiyari, Wanyarwanda ni asilimia 64, Warundi asilimia 34 na Waganda, asilimia mbili. Alisema msako maalumu haujaanza, lakini unatarajiwa kuanza muda wowote na maandalizi yamekamilika.

Hata hivyo, alitaka wahamiaji hao haramu waendelee kuondoka kwa hiari yao kabla hawajafikishwa kwenye mkono wa sheria. Alisema Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera, imesitisha utoaji vibali kwa muda wakisubiri maelekezo kutoka juu.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe aliwahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa msako wa wahamiaji haramu, na kufichua waliojificha.Alisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria watakaobainika kuficha na kuwakingia kifua wahamiaji hao.

Ardhi iliyotengwa

Ardhi hiyo imetengwa katika wilaya za Nyagatare na Gatsibo kwa ajili ya wafugaji ili mifugo yao ipate malisho, imefahamika. Takribani mifugo 2,000 kwa mujibu wa gazeti la The New Times la Rwanda, wameingia nchini humo kutoka Tanzania tangu Wanyarwanda ambao ni wahamiaji haramu, watekeleze agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuondoka katika mapori mkoani Kagera na kurudi kwao.

Baada ya agizo hilo kutekelezwa, wafugaji na wakulima hao walionesha wasiwasi wao wa kupata maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.

Hata hivyo, Mratibu wa Rab katika Jimbo la Mashariki, Celestin Nyambyi, alisema juzi kuwa mifugo hao watawekwa katika vituo maalumu vyenye karantini kwa hadhari ya usalama.

“Ng’ombe wanaingia nchini kwa idadi kubwa na hivyo kuwapo uwezekano wa kusababisha tishio la kiafya kama hadhari haitachukuliwa … wafugaji wanaorejea watapata mahitaji yote wanayotaka kwa ajili ya kupata makazi ya kudumu nchini mwao,” alisema Nyambyi.

Zaidi ya Wanyarwanda 3,500 wanaoishi katika wilaya za Biharamulo, Ngara, Karagwe na Muleba tangu miaka ya sitini hadi sasa, wamepokewa baada ya kufukuzwa Tanzania, gazeti hilo liliripoti.

Wakizungumza na gazeti hilo juzi, wafugaji hao walilalamikia walichokiita kutendwa vibaya na mamlaka za Tanzania na wenyeji, wakidai kuwa walifukuzwa nchini bila kuzingatia haki za msingi za kibinadamu.

Alex Rurangwa, mfugaji ambaye familia yake ilikuwa na ng’ombe 3,000 wilayani Biharamulo, alisema walinyanyaswa na hawakuruhusiwa kuondoka na ng’ombe hao.

Alishauri Wanyarwanda wengine walioko Tanzania kuondoka kabla hawajapata hasara ya mali na maisha.

“Wanyarwanda wote wanapaswa kuondoka Tanzania. Kuna mazingira yamewekwa ambayo yanaruhusu wakulima kupoteza mali nyingi. Mazingira ya kila mmoja kupora mali za Wanyarwanda ndiyo yameandaliwa,” alidai Rurangwa.

“Wana kila haki ya kutufukuza kutoka nchini mwao, lakini si watupige risasi na kutuibia ng’ombe kama walivyofanya. Nilipoteza ng’ombe 30 kwa kundi lisilojulikana la watu. Walimvizia kaka yangu na kumjeruhi,”alidai.

Mmoja wa wakimbizi waliorejea, Ben Celestin (26), alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya Kirehe juzi baada ya kudai kupigwa mshale mgongoni.

Rurangwa alisema ng’ombe waliorudi nao ndio walikuwa chanzo pekee cha mapato yao, ingawa wanataka kuwabadilisha kwa chanzo kingine cha uzalishaji mali.

“Tumepata hasara kubwa; tunahitaji sasa kubadilisha shughuli ambayo tumekuwa tukiifanya kwa muda mrefu. Tutauza wengi ili kununulia ardhi, nyumba na kuishi maisha ya kudumu. Tunaomba wauzaji wengine waturuhusu tuuze wa kwetu kwanza, kama dharura.”

John Mugisha, mkulima ambaye ng’ombe wake bado wako njiani kutoka wilayani Karagwe, alikuwa na wasiwasi kama wote watafika nchini humo. Alisema vizuizi vya asili kama milima, mito na hifadhi za wanyamapori kwamba vinaweza kuzuia safari ya ng’ombe hao.

“Tuna matatizo. Siku tulizopewa (14) na tulivyotendwa ni ukiukwaji wa haki zetu. Karagwe ni mbali sana na Rwanda. Ng’ombe wetu wako njiani wakijaribu kuvuka mito na mabwawa. Hivyo, nina shaka kama watafika hapa kwa wakati mwafaka,” alisema.

Mume Mtanzania

Roda Mungeriwase (42), mama wa watoto wanane, alidai kuwa kuishi Tanzania siku zote kumekuwa kwa matatizo kwa Wanyarwanda.

“Nililazimika kumwacha baba wa watoto wangu saba ili atunze mali zetu. Mume wangu ni Mtanzania. Wazazi wangu waliingia Tanzania mwaka 1966. Maisha haya ya mashaka yamekuwa sehemu ya maisha yetu,” Mungeriwase alidai.

“Ni hali ya kutisha pale ambapo kwa ghafla tu mtu anajikuta hana mali na nyumba, familia zimesambaratika. Sijui majaaliwa ya mume wangu au jinsi atakavyolea watoto wetu hao saba,” alilalamika.

Mapema, iliripotiwa kuwa makataa waliyopewa Wanyarwanda kuondoka Tanzania yalikuwa Agosti 9. Hata hivyo, kwa mujibu wa wakimbizi waliorejea, Wanyarwanda wote waliokuwa wakituhumiwa kuishi nchini Tanzania kiharamu walitakiwa hadi leo wawe wameondoka nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Gazeti hilo hakuna mahali limezungumzia jinsi Wanyarwanda hao walivyoingia nchini kama walifuata taratibu au walikuwa haramu.

chanzo. http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/15229-waliorudi-rwanda-waandaliwa-ardhi
 
Rais Paul Kagame wa Rwanda

WAKATI agizo la Rais Jakaya Kikwete la wakimbizi haramu likiendelea kutekelezwa na kupokewa vizuri na Rwanda, Bodi ya Kilimo ya nchi hiyo (Rab) imetenga zaidi ya hekta 300 za ardhi kwa ajili ya wananchi wanaorejea.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, ambaye ni Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Elizeus Mushongi, alisema hadi jana, wahamiaji haramu 7,814 walikuwa wameondoka mkoani Kagera na ni walioripoti katika vituo vya Uhamiaji mkoani hapa.

Mushongi alisema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wahamiaji wanaoondoka kupitia ‘njia za panya' ambao ni wengi zaidi.

Alisema katika makundi hayo ya wahamiaji haramu, ambao wanatoka Uganda, Burundi na Rwanda kuna wengine ambao hawataki kurudi kwao na idadi kubwa ya wasiotaka kurudi ni Wanyarwanda.

Kwa mujibu wa Mushongi, Wanyarwanda hao wakati wakijiorodhesha katika vituo, wamekuwa wakisema wanakwenda Burundi na Uganda na hata walioonekana kupita ‘njia za panya', walikuwa wakienda nchi hizo pia.

Alisema katika kituo vya Murusagamba, walipita Wanyarwanda 35 wakienda Burundi, kituo cha Mutukula, Wanyarwanda 13 wakielekea Uganda, Bugango 22 wakienda Uganda na Kanyigo saba, wakienda Uganda.

Katika kituo cha Kabanga, Warundi 522 walijisajili kurudi kwao na Warundi 10 katika kituo cha Murongo, walisema wanakwenda Uganda. Katika kituo hicho, Wanyarwanda 166 walipita wakienda Uganda.

Rusumo yaongoza

Aliongeza kuwa kituo cha Rusumo kinaongoza kwa kupitisha wahamiaji haramu wengi, waliofikia 4,748 wakienda Rwanda.Kituo cha Murongo kilipitisha wahamiaji 332, Murusagamba 78 na Mutukula 31 na eneo la Mgoma ambalo halina vituo vya Uhamiaji, walijisalimisha 1,734 katika ofisi za vijiji.

Kuhusu silaha zilizosalimishwa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi, alisema silaha 42 zilisalimishwa na wahamiaji hao.

Alisema miongoni mwa silaha hizo, nyingi ni magobori huku akisema Jeshi lake limejipanga kukabiliana na wahamiaji ambao hawajaondoka. Alisisitiza kuwa wahamiaji watakaokamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Rwanda yakataa ng'ombe

Mushongi aliendelea kusema idadi ya ng'ombe walioondoka hadi jana ni 1,996 kupitia kituo cha Rusumo huku wengi wakienda Uganda, kwa sababu Rwanda haitaki idadi kubwa ya ng'ombe.

Kitakwimu, alisema kati ya wahamiaji haramu walioondoka kwa hiyari, Wanyarwanda ni asilimia 64, Warundi asilimia 34 na Waganda, asilimia mbili. Alisema msako maalumu haujaanza, lakini unatarajiwa kuanza muda wowote na maandalizi yamekamilika.

Hata hivyo, alitaka wahamiaji hao haramu waendelee kuondoka kwa hiari yao kabla hawajafikishwa kwenye mkono wa sheria. Alisema Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera, imesitisha utoaji vibali kwa muda wakisubiri maelekezo kutoka juu.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe aliwahadharisha wananchi kuwa makini wakati wa msako wa wahamiaji haramu, na kufichua waliojificha.Alisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria watakaobainika kuficha na kuwakingia kifua wahamiaji hao.

Ardhi iliyotengwa

Ardhi hiyo imetengwa katika wilaya za Nyagatare na Gatsibo kwa ajili ya wafugaji ili mifugo yao ipate malisho, imefahamika. Takribani mifugo 2,000 kwa mujibu wa gazeti la The New Times la Rwanda, wameingia nchini humo kutoka Tanzania tangu Wanyarwanda ambao ni wahamiaji haramu, watekeleze agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuondoka katika mapori mkoani Kagera na kurudi kwao.

Baada ya agizo hilo kutekelezwa, wafugaji na wakulima hao walionesha wasiwasi wao wa kupata maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo yao.

Hata hivyo, Mratibu wa Rab katika Jimbo la Mashariki, Celestin Nyambyi, alisema juzi kuwa mifugo hao watawekwa katika vituo maalumu vyenye karantini kwa hadhari ya usalama.

"Ng'ombe wanaingia nchini kwa idadi kubwa na hivyo kuwapo uwezekano wa kusababisha tishio la kiafya kama hadhari haitachukuliwa … wafugaji wanaorejea watapata mahitaji yote wanayotaka kwa ajili ya kupata makazi ya kudumu nchini mwao," alisema Nyambyi.

Zaidi ya Wanyarwanda 3,500 wanaoishi katika wilaya za Biharamulo, Ngara, Karagwe na Muleba tangu miaka ya sitini hadi sasa, wamepokewa baada ya kufukuzwa Tanzania, gazeti hilo liliripoti.

Wakizungumza na gazeti hilo juzi, wafugaji hao walilalamikia walichokiita kutendwa vibaya na mamlaka za Tanzania na wenyeji, wakidai kuwa walifukuzwa nchini bila kuzingatia haki za msingi za kibinadamu.

Alex Rurangwa, mfugaji ambaye familia yake ilikuwa na ng'ombe 3,000 wilayani Biharamulo, alisema walinyanyaswa na hawakuruhusiwa kuondoka na ng'ombe hao.

Alishauri Wanyarwanda wengine walioko Tanzania kuondoka kabla hawajapata hasara ya mali na maisha.

"Wanyarwanda wote wanapaswa kuondoka Tanzania. Kuna mazingira yamewekwa ambayo yanaruhusu wakulima kupoteza mali nyingi. Mazingira ya kila mmoja kupora mali za Wanyarwanda ndiyo yameandaliwa," alidai Rurangwa.

"Wana kila haki ya kutufukuza kutoka nchini mwao, lakini si watupige risasi na kutuibia ng'ombe kama walivyofanya. Nilipoteza ng'ombe 30 kwa kundi lisilojulikana la watu. Walimvizia kaka yangu na kumjeruhi,"alidai.

Mmoja wa wakimbizi waliorejea, Ben Celestin (26), alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya Kirehe juzi baada ya kudai kupigwa mshale mgongoni.

Rurangwa alisema ng'ombe waliorudi nao ndio walikuwa chanzo pekee cha mapato yao, ingawa wanataka kuwabadilisha kwa chanzo kingine cha uzalishaji mali.

"Tumepata hasara kubwa; tunahitaji sasa kubadilisha shughuli ambayo tumekuwa tukiifanya kwa muda mrefu. Tutauza wengi ili kununulia ardhi, nyumba na kuishi maisha ya kudumu. Tunaomba wauzaji wengine waturuhusu tuuze wa kwetu kwanza, kama dharura."

John Mugisha, mkulima ambaye ng'ombe wake bado wako njiani kutoka wilayani Karagwe, alikuwa na wasiwasi kama wote watafika nchini humo. Alisema vizuizi vya asili kama milima, mito na hifadhi za wanyamapori kwamba vinaweza kuzuia safari ya ng'ombe hao.

"Tuna matatizo. Siku tulizopewa (14) na tulivyotendwa ni ukiukwaji wa haki zetu. Karagwe ni mbali sana na Rwanda. Ng'ombe wetu wako njiani wakijaribu kuvuka mito na mabwawa. Hivyo, nina shaka kama watafika hapa kwa wakati mwafaka," alisema.

Mume Mtanzania

Roda Mungeriwase (42), mama wa watoto wanane, alidai kuwa kuishi Tanzania siku zote kumekuwa kwa matatizo kwa Wanyarwanda.

"Nililazimika kumwacha baba wa watoto wangu saba ili atunze mali zetu. Mume wangu ni Mtanzania. Wazazi wangu waliingia Tanzania mwaka 1966. Maisha haya ya mashaka yamekuwa sehemu ya maisha yetu," Mungeriwase alidai.

"Ni hali ya kutisha pale ambapo kwa ghafla tu mtu anajikuta hana mali na nyumba, familia zimesambaratika. Sijui majaaliwa ya mume wangu au jinsi atakavyolea watoto wetu hao saba," alilalamika.

Mapema, iliripotiwa kuwa makataa waliyopewa Wanyarwanda kuondoka Tanzania yalikuwa Agosti 9. Hata hivyo, kwa mujibu wa wakimbizi waliorejea, Wanyarwanda wote waliokuwa wakituhumiwa kuishi nchini Tanzania kiharamu walitakiwa hadi leo wawe wameondoka nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Gazeti hilo hakuna mahali limezungumzia jinsi Wanyarwanda hao walivyoingia nchini kama walifuata taratibu au walikuwa haramu.

chanzo. http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/15229-waliorudi-rwanda-waandaliwa-ardhi

UMOJA WA WANYARWANDA WAKIMBIZI
Brazaville Dar es Salaam Cape townLondon​
Tel. +242069728747 +255755047545 +27795382019 +447413549095
E-mail: <hutubanturace@gmail.com>​

KWA MAANDALIZI YA KUREJEA KWENYE NCHI YETU
RWANDA, JIBU LA MAZUNGUMZO YA KISIASA

MATATIZO MAKUBWA YA WANYARWANDA NI YA KISIASA NA YANAGUSA KILA MUNYARWANDA. UFUMBUZI WAKE NI MAZUNGUMZO YA KISIASA KATI YA WANYARWANDA AMBAO WAKO KWENYE UONGOZI WA RWANDA LEO, WANANCHI, UPINZANI, NA UMOJA WA WANYARWANDA WAKIMBIZI.

KWA MAANDALIZI YA KUREJEA KWENYE NCHI YETU RWANDA: JIBU LA MAZUNGUMZO YA KISIASA.
MAZUNGUMZO KATI YA WANYARWANDA: NJIA PEKEE YA KUONDOKANA NA TATIZO LA KISIASA.
Mazungumzokatiyawanyarwandayanayoandaamazingirayamaelewanokatiyawanyarwanda, ndiyonjiapekeeyakuondokananamatatizoyoteya Rwanda. Viongoziwataifahilo, walitakiwakuzingatianafasihiimuhimunakufikiahatuayakubadilishamutazamowao.
Mdaumefikailiwanyarwandawotetuishipamojakwenyenchiyetu. Rwanda ninchiyetusisiwotenaitajengwatunaumojawawatwa, wahutunawatutsi. Hayomazungumzondiyodhamanayamatokeomazurikwenyemaswalayakisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, nk,katikataifaletu.Wakimbiziwotewakinyarwandawanaotakakurejeakwao, huundiomsimamowao,bilauogawalakubabaisha.
Tangumiaka 19,tukiwanjeyanchiyetu, uongoziwaKagameunajuavizurisanakwambatumeachananafamiliazetu, tumepotezamalizetu; kwambanyumbazetuzimebomolewa au zimechukuliwanawatuwenginenakwambanduguzetuwengiwanasutanakuteswakwenyemagerezabilakesiyoyotebadayakuwatuwamesingiziwa. Hatunaimanitenana Paul Kagame, ndiyomanatunatakiwakuzungumzia kwanza maswalayausalama, namengineyotekablahatujarejea Rwanda.
Paul Kagameanajuavizurisanakwamba, wengimiongonimwawanajeshi wake, au wanachamawa RPF, ambaowamemwagadamuzawanyarwandawengi, wakohurubilahofuyoyote, nahiyohaliinaonyeshajinsiganimahakamazauongoziwa Kigali siyozakuaminika.

MADAI YETU MAKUBWA YANAHUSU VITU VIFUATAVYO:
- Mazungumzokatiyawanyarwanda
- National Reconciliation
- Kutambulikakwavyamavyasiasavyaupinzaniikiwandani au njeya Rwanda bilayakuviingizakwenyekitukinaitwa "forum"
- Kuingizawakimbiziwotewatakaorejeakwaokwenyemaishayakawaida
- Kuachiliahuruwafungwawotewakisiasa
- Mahakamazisizopendeleakwawanyarwandawote
- Kuingizawanajeshiwazamanikwenyejeshi la taifa
- Kuhakikishausalamawawatunamalizao
- Kusomeshawatotowoteambaowazaziwaohawanauwezobilaubaguziwowote
- Uhuruwakujielezanakutoamaoni
- Kuandaamazingiramazuriyauchaguzihuruna transparent kwenyengazitofautitofauti.

NATIONAL RECONCILIATION.

Nationa Reconciliation nikituambachohadileokimeupigachengauongoziwa RPF. Tanguinashikamadarakamwakawa 1994, RPF inaendeleakuenezauongokwamataifakwambainaupakipaombeleumojawakitaifa, wakatimatendoyakeyakisiasanakijeshiyanapelekeakwenyechuki. Viongoziwa RPF hawaachikuonyeshajeurikwambachamahichokimeshindakwamtutuwabundukinakwamanahiyokinatakiwakutawalakimabavu. Ndiyomanawahutuwotewaliyouawana RPF wamesahaulika, wakatiwatutsiwaliyokufawanakumbukwawakatiwote. RPF itadaijekwambakuna reconciliation ikiwawaliyokufawotepandezotehawakumbukwiwote?
Tunasisitizakwamba national reconciliation katiyawanyarwanda, inatakiwakutokananaumojakatiyawanyarwandawote. Ili tufikekwenyeumojahuo, kunavitu 4 muhimuvyakujua:

- Hukumusawakwawatuwapandezotembiliambaowameingizakwenyemachafukotaifa la Rwanda. Aidhakwakuundatuumeyakitaifayakufuatilia, au kwakupanuwa mandate ya ITPR kwaviongoziwaserikaliya Kigali naya RPF waliyohusikakuuawahutundaniya Rwanda nakwenyenchiambazowamekimbilia;
- Hakiyakumbukumbukwawaliyokufawotenasiyotukwaupandemmoja;
- Uchunguziwa kina au utafitikwenyeukwelikuhususababuzamsingikwenyematatizoyanayogonganishawanyarwanda;
- Hudumakwawahangawotebilaubaguzi.
Tunafikiritenatunaaminikabisakwamba "tuumeyakitaifayaukweli, uhuruwamahakamana reconciliation, ambayopekeendiyoyenyeuwezowakurejeshaamanikwenyetaifa la Rwanda, inaitajikasana". Ndiyomanaumojawawanyarwandawakimbiziunaombaviongoziwa Rwanda kuchangamkiaharakatizakuundahiyotuume.
KUINGIZA ASKARI WA ZAMANI (EX FAR) KWENYE JESHI LA TAIFA
Ili matatizoya Rwanda yafikieukomo wake, tunatakiwakukubarianakwambakunasehemuyawanajeshiwazamani(ex FAR)ambaowanaishiukimbizinitakribanimiaka 19 imepita. Kwaajiliyausalamazaidiwataifa la Rwanda, wanajeshihaoambaoniwakimbizi, hawatakiwikubakimisituni. Wanaitajikurejeakwenyenchiyaokwanjiayamazungumzoitakayoandaamazingirayakuwaingizakwenyejeshijipya la taifa.Nikwanjiayamazungumzotukwenyeambayohawowanajeshiwakimbiziwanawezakurejea Rwanda bilakuwanawasiwasi.
MAANDALIZI YA UCHAGUZI HURU NA TRANSPARENT KWENYE NCHI YA RWANDA
Uchaguzihuruna transparent kwenyetaifa la Rwanda ukombalikwasababu Rwanda inatawaliwakimabavunachamakimojaambachondichokinaruhusiwakutoamgombeauraismmoja.
Kwenyenchiya Rwanda wakatiwauchaguzimkuu, wagombeauraiswavyamavyaupinzaniwanabugudhiwa, wanachukuliwakama negative forces, maranyinginewanakamatwanakutupwandaniiliwaregezwekisiasa, nahatimayekuwafanyawapotezesifazaozote. Mifanohainikama Madame INGABIRE Victoire, mwenyekitiwa FDU, mgombeakwenyeuchaguziwaraismwakawa 2010; Dr MUSHAYIDI Deogratias, mwenyekitiwa PDNnaMr Bernard NTAGANDA, mwenyekitimwanzilishiwa PS imberakuri&#8230;.Wanyarwandawanakiukubwayakujichaguliaraiswanayemutakabilakulazimishwa.
KUJENGA RWANDA MPYA NI KAZI YA WANYARWANDA WOTE
Kwamtazamohuo, Paul Kagamekamaraisnayeyenimmojawawanaotakiwakujenga Rwanda mpya.
Kuna takribanimiaka 19 wanyarwandawanazururakutokananamachafukoyaliyoikumba Rwanda yakayipelekeakutumbukiakwenyegizanenemwakawa 1994. Lakini, wakatiwotetukiwaukimbizini, serikaliya Kigali haijabadilishasiasazakezaubaguzinaukandamizajiwaupandemmojawawananchi. Hiyosiasainazuiasanawakimbiziwakinyarwandakurejea Rwanda kwahiyariyao.
Ukwerinikwambaserikaliya Kigali, hainampangowalauhiyariwakujengamazingirayamazungumzonakuwekapamojawanyarwandawote.
Kinyumechake, serikalihiyoinaendeleakuchocheamauaji, ambayoyamekuwandiyosirahayake. Ukosekanajiwasiasayakweliyakujengataifaletukwenyemaeneoyote (uchumi, utamaduni, mahusiano, uhuruwakuabudu&#8230😉, wakimbiziwotewanamashakakwenyemanenoya Paul Kagamekuhusukurejeakwao.
Kutokakwenyegazeti la Le Figaro la tarehe 24 December 2010 "Paul Kagamealijutiahadharanikuwahakuwezakuuawahutuwotewaliokimbilia DRC, naakaahidikwambaatakujakumalizananaobadaye", wakimbiziwanawezakuwanasababunzurizakujiulizamaswalikwenyehabarihiyoyakurejea.

HITIMISHO
Kwamfanowanchiambazozimepitakwenyemigogoromikubwakama Rwanda, umojawawanyarwandawakimbizi, unaaminikwambaniwakatimwafakawakuandaa mambo yajaobilakusahauyaliyopita. Lakinipia, umojahuohuo, unajuakabisakwambawapowanaumenawanawakeambaowanajuaumuhimuwakusameheyana, umuhimuwakujiunganakupendakuishipamoja. Ndiyomana, umojahuowawakimbiziungependakuhusishwakwenyekujenga Rwandampya, nchiyetu, kwakuunganishawanyarwandawotebilaubaguzi (watwa, wahutunawatutsi) nahatimayekujenganchiyenyeamaninademokrasia.

MSEMAJI WA UMOJA WA WANYARWANDA
DEOGRATIAS KAREGEYA-DENMARK
+4591703492

COMMUNAUTE DES EXILES RWANDAIS
Brazaville Dar es Salaam Cape town LondonTel.+242069728747 +255755047545 +27795382019 +447413549095
POUR UN RETOUR DIGNE DES EXILES A LA MERE PATRIE: LE RWANDA
UNE REPONSE A L'OFFRE POLITIQUE DE RETOUR AU RWANDA
 
Kikwete kamuangalia Kagame akasema nini kujibizana, you want beef, then beef it will be.

Kwanza tunawabeba kwa miongo kadhaa wenu wako kibao wanahemea kwetu huku.Tumewapa fursa ya kuchukua uraia hawajaitumia, hao wachukue.

Ki nchi chenyewe kiganjani hakijai, halafu mnataka beef na bongo.

I am not one to easily side with Kikwete, but this was a strategic way to send an OG message "don't mess with us".
 
Duuhh afadahali sasa wapatane na kumbe Nchi yao ina ardhi kubwa. Kwenu ni kwenu tu hata kama ni pangoni utaishi kwa amani na msibaguane tena ishini kwa amani. nampongeza sana
DEOGRATIAS KAREGEYA wa DENMARK wa COMMUNAUTE DES EXILES RWANDAIS Dar es Salaam +255755047545
Kwa sasa sina ubishi tena AMANI inapatikana Waafrika wenzetu kina- Koba murutongore MukUMASIMBA environmental
 
Last edited by a moderator:
Ardhi wanayo kweli Rwanda, haya kama hawajaomba hifadhi nje ya Rwanda utasikia
 
Jeshi la Polisi Tanzania, Usalama wa Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ pamoja na Viongozi wote wa Mikoa husika hakikisheni mnaendelea na msako wa kuwaondoa Wahamiaji haramu wote yaani wale wanaoishi bila Vibali. Pia zichukuliwe hatua kali za kisheria kwa wale wahamiaji haramu ambao hawakutii ule muda muafaka tuliowapa warudi kwao. Napenda kuwahakikishia ya kuwa zoezi hili halitaishia mkoani Kagera tu, bali Tanzania nzima. Serikali yenu inafahamu vema walipo hawa wahamiaji haramu hususani kutoka Rwanda. Ndugu Wananchi wa Tanzania, Serikali yetu imepeleka Batalioni nchini Congo ili kulinda amani kukabiliana na kukabiliana na waasi wanaojulikana kwa jina la m23 nchini humo.
Waasi hawa m23 wataondoka nchini DRC muda si mrefu kwa kipigo kizito watakachokipata kutoka kwa majeshi ya UN yaliyopo DRC yakiongozwa na Brigedia Jenerali James Mwakibolwa. Wakishaondoka Congo UTAPITA MSAKO WA HALI YA JUU SANA ILI KUWAONDOA WARWANDA NCHINI HUMO. Napenda kuwahakikishia ya kwamba HAKUNA NCHI YOYOTE INAYOWEZA IKATUTISHIA AMANI WATANZANIA. Tunaliamini JWTZ kwa kuwa lipo Imara sana, ndani na nje ya Tanzania.
Ni mimi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia JamiiForums. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania. Asanteni kwa Kunisikiliza.
 
asanteni sana kwa kunisikiliza...hahaha, acha bwana, JK ana muda huo kuja jf?
 
Ardhi wanayo kweli Rwanda, haya kama hawajaomba hifadhi nje ya Rwanda utasikia
Wajomba zako interahamwe ndio walikuwa wanasema ardhi haitoshi wakaanza kuua watu,Kagame anawahimiza wote mrudi kwenu muache kukaa misituni na ndoto zenu za kuwamaliza watutsi kabla malaria hazijawamaliza huko maporini.
 
Jeshi la Polisi Tanzania, Usalama wa Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ pamoja na Viongozi wote wa Mikoa husika hakikisheni mnaendelea na msako wa kuwaondoa Wahamiaji haramu wote yaani wale wanaoishi bila Vibali. Pia zichukuliwe hatua kali za kisheria kwa wale wahamiaji haramu ambao hawakutii ule muda muafaka tuliowapa warudi kwao. Napenda kuwahakikishia ya kuwa zoezi hili halitaishia mkoani Kagera tu, bali Tanzania nzima. Serikali yenu inafahamu vema walipo hawa wahamiaji haramu hususani kutoka Rwanda. Ndugu Wananchi wa Tanzania, Serikali yetu imepeleka Batalioni nchini Congo ili kulinda amani kukabiliana na kukabiliana na waasi wanaojulikana kwa jina la m23 nchini humo.
Waasi hawa m23 wataondoka nchini DRC muda si mrefu kwa kipigo kizito watakachokipata kutoka kwa majeshi ya UN yaliyopo DRC yakiongozwa na Brigedia Jenerali James Mwakibolwa. Wakishaondoka Congo UTAPITA MSAKO WA HALI YA JUU SANA ILI KUWAONDOA WARWANDA NCHINI HUMO. Napenda kuwahakikishia ya kwamba HAKUNA NCHI YOYOTE INAYOWEZA IKATUTISHIA AMANI WATANZANIA. Tunaliamini JWTZ kwa kuwa lipo Imara sana, ndani na nje ya Tanzania.
Ni mimi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia JamiiForums. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania. Asanteni kwa Kunisikiliza.
Sitashangaa kama hujawahi kutoa mguu hapo kijijini kwenu tangu uzaliwe.
 
Wajomba zako interahamwe ndio walikuwa wanasema ardhi haitoshi wakaanza kuua watu,Kagame anawahimiza wote mrudi kwenu muache kukaa misituni na ndoto zenu za kuwamaliza watutsi kabla malaria hazijawamaliza huko maporini.

Hivi Koba kweli uelewa wako ni mdogo sana,hivi unakuwa unaandika kutoka moyoni ama unaandika tu ili uonekane umeandika?Wewe kwa uelewa wako unaona kama Rwanda ni linchi likubwa sana kiasi kwamba Wanyarwanda wote walioko nje ya Rwanda wakija Rwanda haiwezi kujaa.Kwa taarifa yako Rwanda na Burundi ni vijinchi vidogo sana ndiyo maana vinawahimiza wananchi wake wazingatie uzazi wa mpango wala si kwa afya bali ni kuogopa nchi zao kuburts.
By the way mimi siyo Interahamwe ila mimi niko kinyume na Tutsi&Kagame ideologies of killings
 
Back
Top Bottom