Wimbi la hofu limewakumba wahamiaji wa mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoishi nchini Afrika Kusini baada ya maandamano makubwa ya kupinga wahamiaji haramu kuzuka jijini Pretoria, huku maandamano mengine yakitarajiwa kuendelea leo Jumatano mjini Johannesburg.
Maelfu ya wageni wameonywa kuchukua tahadhari, kufunga biashara zao na kupunguza shughuli za nje kutokana na hofu ya kushambuliwa na makundi yenye msimamo mkali wa kupinga wageni.
Tahadhari hiyo imetolewa na balozi na jumuiya za wahamiaji, ikiwemo Ghana na Nigeria, baada ya mamia ya waandamanaji kuandamana Jumanne kupitia mitaa ya Pretoria hadi Majengo ya Muungano wakitaka serikali iwafukuze wahamiaji wasio na nyaraka.
Waandaaji wa maandamano hayo wanadai wageni wamekuwa wakichukua ajira, kufanya biashara holela na kunufaika na huduma za umma, jambo lililosababisha baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni kufunga maduka yao kwa hofu ya uvamizi au vurugu.
Licha ya shinikizo hilo la wananchi, Rais Cyril Ramaphosa ameonya kuwa malalamiko kuhusu uhamiaji haramu yasitumike kuchochea chuki dhidi ya Waafrika wenzao, akisisitiza kuwa Afrika Kusini ina deni la kihistoria kwa mataifa ya Afrika yaliyoiunga mkono katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Serikali imeweka vikosi vya polisi katika hali ya tahadhari wakati maandamano hayo yakisambaa kutoka Durban hadi Gauteng, huku hofu ya mashambulizi ya kibaguzi ikiendelea kuongezeka.