Waliooa, naombeni msaada

Dah we jamaa ulikosea sana.
Kumbe yupo hivyo kabla ya ndoa? Basi ndo chaguo lako mvumilie.
Inaonekana sex sio kitu cha muhimu kwako.
Mbali na sex..nlitarajia mengi sn kuyapata kutoka kwake..kama nikienda kazini siagwi..nkiwa kazini siulizwi..nkiwa narudi siulizwi chochote..hicho ndo kimenifanya pia nichukie..AU hii ni normal kwa wake wote?
 
kaka kama ni mjamzito kuwa mpole kabisa, ni kawaida kwa wanawake wakiwa katika hali hiyo ya ujauzito kupoteza hisia kabisa ila siyo wote...hata tabia pia wanabadilika atakudhalau, Majibu siyo na kero nyingi nyingi unaweza ukaona anakudharau ila ni mabadiliko ya homoni mwilini mwake yanamuendesha
 
Mbali na sex..nlitarajia mengi sn kuyapata kutoka kwake..kama nikienda kazini siagwi..nkiwa kazini siulizwi..nkiwa narudi siulizwi chochote..hicho ndo kimenifanya pia nichukie..AU hii ni normal kwa wake wote?
Sio normal. Hayo yote ulitakiwa uyapate kabla ya ndoa. Yaani mnaishi kama walio kwenye ndoa ambao walishachokana kitambo na ndoa yao ipo juu ya mawe.

Labda tukuulize nini kilikuvutia kwake hadi ukaamua kumuoa? Nini special uliona kwake hadi ukapata msisimko kwamba huyu anafaa kuwa mke wako?
 
kaka kabla ya ujauzito hiyo tabia
 
Japo sio mwanamke ila wapo wasiopenda sex ndgu. Wapo kabisaa na ni hawapendi kwasababu zao mbalimbali, wengine wanaona wanaume ni wachafu, wengine magonjwa, wengine ndo hao wasiofeel chochote wakisex, wengine ndo huhisi maumivu tu.

Makundi yote hayo wanasex kwasababu wanaziskia story na watu kusema wanapata raha wakisex na wao wanaiga/kujaribu.
 
huruma yangu kua ana mimba yangu ndo ilinifny nivutike kumfanya awe mke wng..mengine sikuyapenda ndo maana nlimuonya kua kama anataka ndoa abadilike..akaniahidi ndo nikamuoa.
 
Ulimwomba MUNGU kabla hujajiingiza ktk mahusiano na huyo Binti?

Isijekuwa ulitekwa kwa nguvu za giza bila ya wewe kujitambua na uliposhtuka ndivyo hivyo tena ushaingia mkenge.
 
huruma yangu kua ana mimba yangu ndo ilinifny nivutike kumfanya awe mke wng..mengine sikuyapenda ndo maana nlimuonya kua kama anataka ndoa abadilike..akaniahidi ndo nikamuoa.
Duh basi endelea kupambana na hali yako mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…