Waliomteka Baba Wa Mikel Obi walijuta baada ya habari kumfikia Abramovic

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
🇳🇬🗣️ John Obi Mikel:
Baba yangu alitekwa nyara wakati nilipokuwa nikiichezea Nchi yangu Nigeria katika Kombe la Dunia la Mwaka 2018 lililopigwa nchini Urusi.

Tulikuwa tunakaribia kucheza dhidi ya Argentina.
Masaa mawili kabla ya mchezo nilipata simu kutoka kwa Ndugu yangu akisema baba yangu alitekwa.

Zamani aliwahi kutekwa nyara, ilitushangaza, lakini hii ya mara ya pili ilikuwa ya kushangaza na kustusha zaidi kwa sababu nilikuwa karibu kwenda kukiputa katika moja ya mchezo mkubwa maisha mwangu.

Sikuweza kuondoka kwenye chumba.
Sikuweza kumwambia mtu yeyote.
Nilikuwa peke yangu katika chumba kwa muda wa dakika 30 huku nikifikiria nifanye nini?

Timu nzima ya Nigeria tulikuwa kwenye maandalizi makubwa kwa maana tulikuwa karibu kuingia katika mchezo mkubwa wa maisha yetu. Tulikuwa karibu kucheza dhidi ya Lionel Messi na Argentina.

Sikuweza kumwambia Mtu yeyote katika Timu yetu kwa maana ningeweza kuwavuruga wenzangu na kuwatoa kwenye mawazo ya Mchezo.

Lakini akili ya haraka ikanijia na nikakumbuka kumpigia Simu Mwamba Roman Abramovich na kumueleza juu ya yote yaliomkuta Baba yangu.

Mwamba ni Mwamba tu, Roman aliniuliza je umeshaongea na Mtu yeyote kwa msaada?!

Nami nikamjibu hapana, na kumwambia baada ya kupokea Simu toka kwa Ndugu yangu sijaongea na Mtu yeyote zaidi yako.

Kisha Roman akaniuliza Je, unataka mimi kuwatuma watu kwenda kumuokoa Baba yako akiwa hai?!

Nilipigwa na butwaa, sikuweza ongea chochote wala kujibu lolote.

Kisha Roman akaniambia usiwe na wasiwasi juu ya hilo. Nijulishe kama unataka chaguo hilo, naweza kufanya hivyo muda wowote kuanzia hivi sasa.

Siku 4 baada ya mchezo dhidi ya Argentina, baba yangu aliachiliwa huru bila gharama yoyote, na hata waliomteka hawajajulikana mpaka Leo.

IMG_7308.jpeg
IMG_7307.jpeg
 
Hiyo ndiyo maana ya utajiri na umafia...
Usikute yeye aliwapigia tu jamaa zake ambao wapo CIA na KGB wakamwambia kesi ndogo hiyo, hiyo ndiyo maana ya connection sio konekishen sijui ya video ya nani imevuja watu waone papachu za watu halafu wajichukulie sheria mkononi.
 
Back
Top Bottom