Waliomshambulia Tundu Lissu kusomewa albadili kesho!

Status
Not open for further replies.
Huku mtaani kwangu kuna misikiti zaidi ya mitatu lkn hakuna albadiri niliyoisikia me naona clip tu ktk mitandao ya kijamii
 
Inasemekana hali ya Tundu Lissu bado ni tete bado yuko ICU.

Haruhusiwi kuongea na watu zaidi ya madaktari na mkewe.

Waliomshambulia kusomewa Albadili kesho.

Hii imekaaje?

Alibadili ni nini?

Matokeo ikisomwa ni nini?

Wakina husoma Alibadili?
Albadil hasomewi kafir. Tundu lisu ni kafir hiyo albadili mungu hataisikiliza. Kuna mtu naitwa Salman Rushdie kama kweli kuna hiyo nadhani angesomewa huyu jamaa maana aliuudhi umma mzima wa Mtume kwa kuita kitabu kitakatifu ni aya za shetani. Lakini jamaa mpaka sass anaponda maisha kishatoka mafichoni.
 
Hii ni thread maalum kujuzana hasa nini matokeo ya kilichosomwa nchi nzima baada ya swala ya ijumaa.
Tukizingatia wana JF wako dunia nzima hakika hamna litakalopita
Kwa kuwa watuhumiwa hasa bado hawajajulikana na maneno ni mengi na wajuzi wa mambo wanasema hili kombora huwa halina reverse gear,yaani mbele kwa mbele.
Tutaungana na Barafu kutoka viunga vya Toronto hasa kutupa habari za Dr Slaa,Lemutuz na Makonda so far ni wazima wa afya mpaka sasa,kutoka Nairobi hamna habari mpya sana Mbowe,Msigwa na Lema wanaendelea vizuri.PolePole na Gambo mambo yao bado yako poa.Yeriko Nyerere waliokuwa karibu naye wanasema ameenda shambani kwake kama kawaida.
Kubenea wanadai jana walipoconfirm kwamba albadri itakuwepo hali yake ilibadilika ghafla.

UPDATES ZINAKUJA KADRI TUNAVYOZIPOKEA
Mkuu wamekuunganisha huku kwenye liuzi la kimbulula
 
UBAINIFU JUU YA ALBADIRI

Ni kwa kipindi kirefu waislam na wasio kuwa waislam wanaamini kuwa "Albadir" ni Dua maalum ndani ya Uislam yenye lengo la kumuombea aliyekudhulumu nk kwa makusudio makubwa apate madhara imma kufa au kuwa kichaa nk.

Kiukweli hakuna Dua kama hii katika Uislam,hutaipata katika mafundisho(Hadith) ya Mtume Swalla llahu alayhi wasallam,si katika hadithi sahihi wala dhaifu.

Jambo hili au ushirkina huu uliopewa jina la Dua umepata umaarufu katika Nchi zetu za Afrika Mashariki hususani miji ya Pwani na mpaka unaaminika kwa baadhi ya uislam wasiotaka kujifunza dini yao katika vyanzo sahihi kiasi hata jamiii ya waislam wakiamini kweli waislam wanazo dua za namna hizi.

[HASHTAG]#Albadiri[/HASHTAG] ni nini????

Ni maombi ya kishirikina anayoomba mtu(muislam au asiye muislam) kwa lengo la kumdhuru aliyemdhulumu(au hata bila kumdhulumu) imma katika mambo kijamii,kiuchumi au kisiasa.

Maombi haya yanapelekwa kwa Majini yaende kwa muhusika kwenda kumtia ukichaa muhusika au kumvurugia mambo yake nk.

Albadiri ni kwa usahihi ni AHLUL BADR maana yake ni WATU WA BADR yaani Maswahaba walipigana Jihaad katika Viwanja Vya Badri nao walikuwa 314 wakiwa dhaifu mno na silaha duni wakawashinda Makafiri zaidi ya elfu moja waliojidhatiti mno kwa maandalizi na silaha nzito na wanyama.

Maswahaba hawa ni watukufu na wameridhiwa na ALLA hapa duniani na kesho Akhera.

[HASHTAG]#USHIRIKINA[/HASHTAG] huu umepewa jina hili kwa lengo la kuwazuga waislam ili waone kuwa hii ni Dua sahihi kama ilivyo dua zingine,na wanajifanya katika huo UCHAWI wao walioupa jina la Dua kuwa wanataja majina ya Maswahaba hawa kupitia Baraka zao wakubaliwa dua yao(Hili nalo ni makosa) hali ni uongo hawamuombi ALLAH na wanaomba Majini yao.

Washirikina hawa wanaoshrikikiana na MAJINI wote duniani ni wajanja sana na wana mbinu nyingi za kutaka kuwapeleka watu motoni.
Huwa wanamuendea Mtu kwa njia nzuri sana lakini malengo yao mwisho wa siku kuwaingiza motoni wafuasi wao.

Wanaweza kuja kwa staili kuwa tunataka huyu Kiti aswali SWALA tano,asiwe mlevi yaani wanataka awe mtu wa Ibada na ajiepushe na Maovu kisha baadae wanamzimisha katika JANGA KUBWA LA SHIRK.

Hii mbinu Baba yao Iblis ndio muasisi mkubwa...

Al araaf:21

فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ ﴿٢٠﴾
"Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie yaliyofichwa kwao ya sehemu zao za siri. Na akasema: “Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele.”



وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ﴿٢١﴾

"Naye akawaapia: “Hakika mimi kwenu nyinyi wawili ni mwenye kukunasihini kidhati.”

Haya tufanye kweli wanamwomba Allah kama wanavyodai JE HII NI NJIA SAHIHI YA KUMUOMBA ALLAH????

Mtume swalla llahu alayhi wasallam ametufundisha kuomba Dua kwa namna hii??

Je ni swahaba gani aliwahi kuomba Dua kwa kupitia Baraka za Ahlu Badr(atakayenitajiwa Swahaba mmoja tu aliyefanya haya NITAMPA MILION MOJA TASLIM)

Haifai kuomba Dua kwa kupitia Baraka za Watu hata Mitume hata kitu chochote.

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

" Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah."

Na kusema kuwa watu hawaombi wale Maswahaba bali anaombwa Allah ila wale kule kuwataja ni kutaka Baraka zao tu kujikurubisha kwa Allah huu ni USHIRIKINA(Shirq) maana huna tofauti na wale waabudu MASANAMU....Hebu wasikie mwenyewe hapa wanavyosema

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾

61. Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanavyoghilibiwa?



HAPA WANAUA KABISA.....

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾

"Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Subhaanah! Utakasifu ni Wake Na Ametukuka kwa ‘Uluwa kwa yale yote wanayomshirikisha"

Sasa hapa tofauti ipo wapi na wale waabudu MASANAMU???!!!!!!

ALLAH anasemaje juu ya yeye kuombwa....????

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖأُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖفَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦

"Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka"


Watu wanapaswa kuomba kwa kupitia majina ya Allah na Amali njema walizofanya.

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖوَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚسَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٨٠﴾
"Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda."

Halafu jiulize Dua gani inaambatana na mambo ya Sindano,wembe na Ndimu????
Kama waislam tungekuwa tunaomba Dua kwa Wembe na Ndimu msikitini si kungejaa ndimu na Wembe au tungekuwa tunaenda nayo????!

Hapa kuna kitu NYUMA YA PAZIA???
Na si kingine ni haya mambo ya uchawi kama tulivyoyabainisha huko nyuma.

NASAHA ZANGU

Waislam wajiweke mbali na hayo mambo ya sheikh yaliyopewa jina la dua na muislam hupaswi hata kufurahia kwa moyoni wanaofanya haya tuwe na msimamo wa nabii Ibrahim

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖرَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿٤﴾

4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha abadi mpaka mumuamini Allaah Pekee.” Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: “Nitakuombea maghfirah, na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia.
 
Albadil hasomewi kafir. Tundu lisu ni kafir hiyo albadili mungu hataisikiliza. Kuna mtu naitwa Salman Rushdie kama kweli kuna hiyo nadhani angesomewa huyu jamaa maana aliuudhi umma mzima wa Mtume kwa kuita kitabu kitakatifu ni aya za shetani. Lakini jamaa mpaka sass anaponda maisha kishatoka mafichoni.
OK mkuu
 
Na ni mazuzu na mazwazwa
Kabisa....wakati North Korea anajaribu Ballistics missiles zake sisi tunachoma ubani eti na kusoma sijui vitu gani eti vinasaidia kukamatwa wahalifu si ujinga ulipitiliza huo hata kichaa hawezi kufanya ujinga kama huo.
 
Kabisa....wakati North Korea anajaribu Ballistics missiles zake sisi tunachoma ubani eti na kusoma sijui vitu gani eti vinasaidia kukamatwa wahalifu si ujinga ulipitiliza huo hata kichaa hawezi kufanya ujinga kama huo.
Na wanaopiga risasi wenzao sio wajinga Mkuu?
 
cf2446de88f35ca3e45cac47ab73ccb3.jpg

Nasikia Mbeya Kishanuka huko

Naona anatafuta hata visivyotafutika.Subirini majibu muone.

Mnaogopa.subirini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom