Waliokutwa na hatia ya mauaji ya RPC Liberatus Barlow wa Mwanza wahukumiwa kifo

ticha alikuwa anamilikiwa kihalali kabisaa na mchezaji mmoja wa zamani wa yanga na pamba, ila tatizo la marehem halikuwa kwa ticha pekee yake, 'wananzengo' wengi tuu walikuwa wakimlalamikia marehen kwa hiyo tabia yake ya kuwa mega mega wake zao, ebu fikiria marehem alikuwa anaishi 'ushuani' uko mwanza mjini lakini akaja kuuliwa gizani uswazi huko tena kilometer nyingi tuu toka nyumbani kwake akiwa amewatoroka walinzi wake na mkewe wake alikuwa tayari ameisha mfukuzia kwao moshi ili apate nafasi nzuri ya kuwa gegeda akina mama wa kisukuma…….

Mnapoengea muwe nauhakika unauhakika alimtoroka mlinzi?unauhakika alimfukuza mke wake?jibu hayo maswali kwanza ndio tuendelee
 
Muganyizi nampata vizuri sana, alikuwa jamaa fulani mpole Sana na ukihitaji msaada anakusaidia. Enzi nipo shule ananiachia gheto usiku nimlindie, mizigo inaingia usiku najua ni mfanyabiashara Mana ananiambia ametoka bandarini. Nilikuwa sifatilii Sana mimi Niko bize na mambo yangu ya shule. Mwisho wa siku naambiwa kakamatwa kwa mauaji ya kamanda Barlow. Kila la kheri bro wangu Muganyizi.

Na ndio shooter wa kwenye tukio hata kumuaga baro nyamagana alikuwepo huwezi mdhania kama alikuwa panja
 
ticha alikuwa anamilikiwa kihalali kabisaa na mchezaji mmoja wa zamani wa yanga na pamba, ila tatizo la marehem halikuwa kwa ticha pekee yake, 'wananzengo' wengi tuu walikuwa wakimlalamikia marehen kwa hiyo tabia yake ya kuwa mega mega wake zao, ebu fikiria marehem alikuwa anaishi 'ushuani' uko mwanza mjini lakini akaja kuuliwa gizani uswazi huko tena kilometer nyingi tuu toka nyumbani kwake akiwa amewatoroka walinzi wake na mkewe wake alikuwa tayari ameisha mfukuzia kwao moshi ili apate nafasi nzuri ya kuwa gegeda akina mama wa kisukuma…….
hao jamaa ilikuwaje wakakamatwa,by the way vipi nani umamkubali pale Wu Tang??
 
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa, washtakiwa wanne baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow October, 2012.

Hukumu hiyo imetolewa Mwanza na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika kuwa Watuhumiwa hao wanne kati ya saba walitenda kosa hilo.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrhaman Ismail. Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Kitangiri Wilayani Ilemela Mwanza, saa 8 usiku wa kuamkia October 13,2012.
Mwenye mke alimwonya RPC
 
kila mtu ana mwisho wake,huyu kamanda alikuwa na eneo la kufugia ng'ombe wa kisasa pale Buswelu,siku akitaka kuja buswelu lazima tu apushwe kwanza la sivyo utakula mabanzi ya kutosha maana kioini hicho barabara ya kwenda Buswelu ilikuwa mbovu sana
 
Muganyizi nampata vizuri sana, alikuwa jamaa fulani mpole Sana na ukihitaji msaada anakusaidia. Enzi nipo shule ananiachia gheto usiku nimlindie, mizigo inaingia usiku najua ni mfanyabiashara Mana ananiambia ametoka bandarini. Nilikuwa sifatilii Sana mimi Niko bize na mambo yangu ya shule. Mwisho wa siku naambiwa kakamatwa kwa mauaji ya kamanda Barlow. Kila la kheri bro wangu Muganyizi.
Tutakuunganisha kwenye kesi ya msingi
 
Me kinachonisikitisha ni kesi kutumia muda mrefu sana kusikilizwa na kutoa hukumu, miaka saba mnapeleleza nini ?
Hii inawanyima haki watu wasio na hatia kuendelea kusota jela na kuharibu mfumo wa maisha yao maana hata wakiachiwa hawalipwi fidia yoyote kwa kutuhumiwa na kukaa jela. Sasa ikiwa kesi inayowahusu Polis wenyewe inachukua muda mrefu hivi, je itakuwaje kwa mimi kapuku? Na bado muda wote wa kesi ndugu wanaliwa pesa za rushwa bila mafanikio ya kesi za ndugu zao.
 
Back
Top Bottom