Waliokumbwa na mafuriko Msimbazi washikwa mkono

Apr 9, 2022
66
32
NYUMBA zaidi ya 250 zimekumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku, nakusababisha Kaya mbalimbali kuamua kuhamisha vitu vyao maeneo mengine kuhofia usalama wao.

Awali akizungumza, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala, Sabri Sharif amesema kuwa, amekubali kunyeshewa mvua kuhakikisha anawafikia Wananchi ikiwemo namna ya kutoa msaada.

"Nimefika kuwapa pole Wananchi kuwashika mkono kwa kipindi hiki huku tukiona namna ya hatua zaidi za msaada kwa waliopata mafuriko.

Lakini pia tayari nimetoa baadhi ya vyakula na vifaa kidogo ilikusaidia Kaya kadhaa ziweze kupata kula, mikate, Lakini pia Unga na baadhi ya mboga kwa Kaya kadhaa kwa leo hii",Amesema Sabri.

Aisha, baadhi ya Wananchi wamelalamikia hatua ya kifusi kilichowekwa kando ya mto Msimbazi kwa kile kinachosemekana kusababisha maji hayo kujaa kwenye nyumba zao.

Aidha, Wananchi wameomba mamlaka za serikali kufika kutoa msaada kwani vitu vyao vimezingirwa na maji Hali ambayo wameshindwa kufanya chochote hadi Sasa.
 
Waachwe, watu waliambiwa wako bondeni hawasikii na wajuaji sana tena kipindi cha kiangazi ukiwaambia mvua zinakuja hameni, watakuambia uliongea na Mungu, acha zako, waacheni wajifunze.
 
Awali akizungumza, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala, Sabri Sharif amesema kuwa, amekubali kunyeshewa mvua kuhakikisha anawafikia Wananchi ikiwemo namna ya kutoa msaada.

"Nimefika kuwapa pole Wananchi kuwashika mkono kwa kipindi hiki huku tukiona namna ya hatua zaidi za msaada kwa waliopata mafuriko.
Bifu litaanza na mbunge
 
Back
Top Bottom