Walioko kwenye ndoa pitia hapa

Walioko kwenye ndoa pitia hapa

nasi

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
47
Reaction score
20
Kwa kawaida mwanaume huhitaji kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kuliko mwanamke, ukiona mume wako anavisingizio tele ili tu asishiriki tendo hilo.

Mara leo nimechoka sana, mara kichwa kinauma, mara leo mgongo unavuta, mara joto limezidi basi hiyo ni alama tosha ya kukujuza kuwa aidha penzi lake kwako limeshuka sana kiasi cha kutolifurahia tendo hilo nawewe.

Au kuna jinsi unavyofanya naye na hapendezwi nayo au kuna sehemu anakoshiba na hana haja ya kuharibu njaa yake kwako na kama ukiona mwanamke ndio anayetoa visingizio hivi basi ujue kuna jambo au mambo hayajakaa sawa baina yenu na yanahitaji kushughulikiwa.

Kumbuka wakati wote kwamba tendo la ndoa ni mbolea ya maana sana katika kila ndoa, lisipokuwapo au lisipotolewa kwa utoshelevu husababisha mazingira hatarishi
.
 
sawa, sasa nini kifanyike...?
Mkuu Suala lako adhimu !!
Lakufanyika ni kustawisha mazingara yenu hivi :-
Mwanaume kizoeshe kumletea zawadi au pesa mkeo !!
na mwanamke ampikie msosi wa maana na atunze usafi nyumbani... (thas all) !! nasi Madame S
 
Last edited by a moderator:
Kwa kawaida mwanaume huhitaji kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kuliko mwanamke, ukiona mume wako anavisingizio tele ili tu asishiriki tendo hilo.
Mara leo nimechoka sana, mara kichwa kinauma, mara leo mgongo unavuta, mara joto limezidi basi hiyo ni alama tosha ya kukujuza kuwa aidha penzi lake kwako limeshuka sana kiasi cha kutolifurahia tendo hilo na wewe.

Mkuu hiki ulichoandika ni nadharia tu ambayo si muda wote ni sahihi. Na mara nyingi walioko nje ya ndoa ndio hudhani kwamba ukiwa kwenye ndoa basi kila mara lazima mfanye tendo la ndoa na msipofanya basi mmojawapo anachepuka. Tendo la ndoa linahitaji mazingira fulani ya utulivu wa mawazo na mwili ili kuweza kulifurahia.

Nitoe mfano hapa Dar kwa sisi tunaomka asubuhi sana kupigana na foleni, natoka nyumbani saa kumi na moja asubuhi, nikiwa nimeamka saa kumi alfajiri ili kuweza kujiandaa, nafika kazini saa mbili kasoro au saa moja na nusu asubuhi. Nafanya kazi hadi saa kumi na mbili jioni huku nikikutana na stress kibao za kazi. Natoka kazini saa moja usiku nafika nyumbani saa nne na nusu usiku na wakati mwingine saa tano usiku. Na hii ni jumatatu hadi jumamosi. Katika mazingira haya, huyo mke atakuwa ni mtu wa ajabu sana nikimweleza nimechoka na akashindwa kunielewa.
 
Back
Top Bottom