Waliokeketwa hatarini zaidi kupata maambukizi ya UKIMWI

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Imeelezwa kuwa wanawake waliokeketwa wanapojamiiana na mwathirika wa virusi vya UKIMWI (VVU) huwa katika hatari ya kupata maambukizi kwa asilimia 99 kuliko ambao hawajakeketwa.

Meneja wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na Shirika la Amref Health Africa Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN Women, Godfrey Matumu alisema vitendo vya ukeketaji ni ukatili wa kijinsia.

Akizungumza mbele ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kisangura katika kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Matumu alisema kwamba ukeketaji una athari kubwa kiafya na kisaikolojia kwa watoto wa kike wanaotendewa kwa misingi ya kutimiza hitaji la mila.

“Idadi kubwa sana hufanyiwa ukatili wa kijinsia, utafiti unabainisha kuwa mwanamke aliyekeketwa anapojamiiana na mwathirika wa virusi vya UKIMWI ana asilimia 99 ya kupata maambuzi tofauti na ambaye hajakeketwa,” alisema.

Matumu aliwataka wanafunzi kuwa na ujasiri wa kukataa vitendo vya ukeketaji kwa kuwa ni chanzo cha ndoa na mimba za utotoni zinazokatisha ndoto zao.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu, Neema Mahiri alisema kwamba watoto wengi wa kike wanakubali kukeketwa kwa kuwa hawaambiwi madhara yake.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Maria Mchala alisema kwamba wanapokea migogoro mingi ya ndoa za utotoni ikiwamo ya wazazi kuwaoza watoto kwa wazee kwa ajili ya kupata mali.

“Ofisa vijana wa wilaya, Isaack Mwakyusye alisema kata ya Kisangura ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa ukatili wa kijinsia.


Mwananchi
 
Clitoris when removed is promotional to low sexual sensational as result less vaginal lubrication when this happen friction during copulation is inevitable ,that's the fact but i n one side of coin , a genital mutilated woman experience huge vagina opening hence lowered friction in penetration ,this also reduce the chance of friction
 
Ki vipi ? Sijaelewa ,au ndo kuongeza chumvi


Clitoris when removed is proportional to low level of sexual sensations as result less vaginal lubrication when this happen friction during copulation is inevitable ,that's the fact but i n one side of coin , a genital mutilated woman experience huge vagina opening hence lowered friction in penetration ,this also reduce the chance of friction ,when no friction or less ,then the chance of HIV infection is reduced and sometimes nil ,thanks
 
kwanza wafanye utafiti kwamba kati ya jamii zinazokeketa na zisizokeketa wapi maambukizi yako juu
 
Back
Top Bottom