Walioiuza CHADEMA mwaka 2015 sasa hivi ndio wanachukua hatamu huku wakijinadi hawanunuliki, Watanzania hawajasahau

Kaka huchoki?, uchaguzi waachie chadema inawahusu wao
 
Ndiyo maana sina imani kabisa na watawala maneno asali na wapenda sifa
 
Kumbuka ccm inachukiwa sana sana na huku kulwzimisha ipendwe kwa mtutu wa bunduki ndiyo kunazidi kuwafanya watu wapandwe na ghadhabu

Mbowe kukataa kunuliwa na ccm kumefanya watu eamuamini na kumuona kuwa ndio mkombozi pekee aliyebaki Tanzania
2015 wanaccm EL,FS na Kingunge walimlipa bei gani?
 
Poor you..! Bila shaka unaugua infantile disorder
 
Ni kweli.madalali wa Chadema 2015 wakiongozwa na mbowe na genge lake la akina Tundu Lisu,Mchungaji Msigwa,Godbless Lema ,Halima Mdee nk Sasa hivi ndio wanajitia vinara wasionunulika!!!! Lowasa aliwanunua wote
 
Hivi mbona hamuongelei chama chenu ccm kimebaki cha watu watatu tu JPM, Bashiru na Polepole.
 
Umewaza mbali sana mkuu,

mimi nina swali la kuongezea.

Kama chama walikiuza,tena kwa mtu mmoja tu mwenye ukwasi na kututangazia watanzania gear ya angani.
Je wakipewa IKULU itakuwaje na tamaa zao hizo?

Na tunawaona wanavyojiuza kwa mabeberu huko EU na USA.
si watatutangazia gear ya IKULU?
 
Kama Lowasa hakushinda kwa nini kituo cha kuhesabu kilivamiwa, kompyuta kuchukuliwa na vijana kuwekwa ndani!!
Ile movu ilikuwa nzuri ni ubabe tuu wa CCM na wizi wa kura, vinginevyo MaCCM walikata pumzi, wakasaidiwa na dola!!
 
Mbona CCM mmeuza nchi,na utu wa watanzania na bado tunawachukulia poa tu, huo ushahidi wa chama kuuzwa mpelekee Pole pole ili iwe agenda yenu ya kuendelea kuwadanganya mapimbi wasiojielewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…