Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,010
- 2,604
Kaka huchoki?, uchaguzi waachie chadema inawahusu waoNdugu zangu,
Nianze tu kwa kusema Watanzania si wajinga, wanakumbuka yote yaliyotokea mwaka 2015. CHADEMA inatumia nguvu kubwa kuwanadi walioshiriki kujipatia hela kwenye siasa za mwaka 2015 huku ikiwanadi kuwa eti hao ndio ''chadema asili'' na ''hawanunuliki''. Kundi linalojinasibu kuirudisha Chadema kwenye mstari kama ile Chadema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 linaundwa na wafuatao, nitaweka kauli zao walizosema wakihalalisha ujasiriasiasa wao kwa kushibisha matumbo yao huku sasa wakijinasibu eti wao ndio wanataka ''chadema ya zamani''.
Wapo wengi ila kwa sasa timu hii ya watu sita ndio kiini cha Chadema, wao ndio wanaona ''hawanunuliki'' japo njaa zao za mwaka 2015 bado zinawaondolea uhalali kusema ''hawanunuliki.
- Freeman Mbowe; huyu anarudi, huku akisema kuwa ''CCM isituchagulie Mwenyekiti, mwaka 2015 alisikika akimsifia Lowassa na Sumaye kuwa ''hatuwezi kuacha mtu anayekuja na mamilioni ya kura ili kumridhisha mtu mmoja (Dr.Slaa), alimalizia ''Chama ni watu''. Kumbuka wale wananchi wengi wa mwaka 2015 ndio watapiga kura 2020.
- Godbless Lema; Mwaka 2015 alitumia mistari ya Biblia akitabiri ''anguko la CCM'' kwa ujio wa EL Chadema huku akikana matamshi yake aliyowahi kumtusi EL kipindi cha kampeni za Ubunge Arumeru Mashariki. Je anaushawishi kwa watanzania?
- Jacob Boniface; Huyu naweza kusema ni limbukeni wa madaraka, siku hizi ukimwita jina lake ''Jacob'' haitikia anataka umwite ''Meya''. Huyu na kundi lake walikusanyika ofisini kwa Lowassa pale Mikocheni wakimshukuru kwa kuwasaidi kushinda udiwani, umeya na ubunge Dar. alisikika akisema ''Mh.Lowassa bila wewe sisi si kitu, umetubeba kwenye uchaguzi'' akikana haya maneno lazima apate laana, je anaushawishi kwa Watanzania?
- Peter Msingwa; Huyu kipindi cha kampeni akihojiwa Channel 10 alisema '' EL ni turufu kubwa kwani kwa utafiti waliofanya waligundua ni asilimia 5 tu ya watanzania ndio humnyima kura mtu sababu ya tuhuma za ufisadi'', hivyo wao wameamua kumpa EL kijiti cha urais ili Chadema inufake. Je Msigwa anaushawishi kwa wananchi?
- John Mrema; huyu ndiye alikuwa kinara akichukua nafasi ya Mnyika aliyesusa, yeye aliambatana na EL kila alipopita akiwa na kauli mbiu yake ''kama EL, Kingunge, Sumaye wametoka CCM nani atawaweza?'' kwasasa kabaki yeye na wenzake, je Watanzania watawasamehe?
- Halima Mdee n.k
Nimalize tu kwa kusema kikundi hicho hapo juu hakiaminiki, kinanunulika na kwa sasa hawana uhalali kwa Watanzania.