Nani alikukataza kusoma ndugu. Si ndo wewe ulikuwa unawapiga walimu na kujiona mjanja pale mabinti wakikushangilia. Waache waliomudu mazingira na kujiona mafala kwa muda tu. We ujanja wako umekufanya hivyo ulivyo. Na uyaendelea kuvuta shisha na kinywa smart gin mpaka kifoMhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu
Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.
Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.
Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.