Waliochaguliwa kuandaa mpango wa maendeleo 2050 wote wanaishi Mbezi Beach au Masaki, wanalishwa kwa kodi za umma miaka yote, wana umri zaidi ya 50 yrs

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,102
Mhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu

Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.

Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.

Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.
 
Kweli tupu hii, na sijajua ni kwa nini ni academia pekee waliochaguliwa, si wangeongeza na akina wale wa upande wa pili kubalance mambo? au updande wa pili hawana wataalam Kuntu? Hizi kelele wanazitaka wao wenyewe, wasije sema hawakuambiwa humu ndani....
 
Mhe. Waziri Kitila Mkumbo ametoa majina ya watu alioteua kutengeneza mpango wa 2050. Wote walioteuliwa wana miaka 50 kwenda mbele, ni wake au watoto wa viongozi wa CCM, ni wanazuoni waliofundisha na kusoma naye chuo...........hizi siyo zama za giza ni zama za technology. Hakuna namna hawa wazee wanaweza kuweka projection za nchi kuendana na technology badala yake watakwenda kutuletea nadharia kwenye vitabu

Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa na watu wenye mafanikio kwenye jamii wakiwa Sehemu ya timu . Academia wangebaki kwenye technical team ya waandishi siyo wachakata hoja.

Tunaanza kufeli kupanga kama Ishara ya kufeli kufanikiwa...........nchi haiwezi ikapangiwa kila kitu na wakaazi wa mbezi beach inahitaji watu wa namtumbo, Kaperamsenga na Kipandaule washiriki pia.

Hawa watu wa masaki na Mbezi Beach wanawekwa kwenye mipango ya nchi ndio wanaotengeneza propaganda za utajiri kwenye umaskini. Mtu kazaliwa hadi anazeeka yupo analishwa na serikali kwa kodi za wananchi anawezaje kujua matatizo ya wananchi? Ndio hawa badala ya kuripoti uhalisia wao wanaripoti uongo na uzandiki walioandika kwenye vitabu vyao.
Ndo serikali ya CCM ilipofikia.

Inafanya mambo kama headless chicken
 
Hii inaukweli na uhakika, mtu amekulia utajirini hafu anapinga dira ya maendeleo , huo ni uhuni sana
Hakuna anayepinga dira ndugu yangu, kinachoulizwa, hivi ni ccm pekee yenye wataalam au Upinzani nao pia wapo?

Hivi hao wataalam asilimia karibu 90 wote wamesome nje ya nchi, humu ndanu hakuna? msuguano wa mawazo ndo akili yenyewe, ili dira iwe na maana, Rais angewaalika wapinzani nao wawemo kwenye dira hiyo vinginevyo nao watatengeza yao na ndio itakuwa mwanzo wa malumbano baadala ya zile R4.

Malumbano tumechoka, shirikisheni ndugu zenu watalaamu wa upande wa pili taifa lisonge mbele bila msuguano- Iweje , Mjusi, nguchiro, sungura, wote wanaishi kwenye kichuguu bila mkwaruzo ingawaje wote ni chakula cha mwenzake na sisi tushindwe na viumbe tajwa?
 
Tulitegemea kuona wafanyabiashara, wataalam wa TEHAMa
1. Mbona hawa wamo au hujamuona Rais wa Tanzania Startup association. Pia yumo Dk Neema Mduma ndio ali design mifumo ya machine learning kubashiri mabinti kuacha shule kisa ujauzito!!. So watu wa technology ni wengi humo. Pia wapo wajasiriamali mfano hapo Mgetta she's an entrepreneur pia board member Tantrade.

2. Why academicians? Dunia nzima kazi za consultancy na strategic plans hakuna watu better kuziandaa kuliko Academicians. Hawa laymen/wafanyabiashara wataitwa tu watoe maoni ila wanaoandaa draft zile have to be academicians maana wamebobea kwenye hizo mambo kwa miaka mingi.

Ambacho labda hakijakaa sawa kama ulivyosema ni balance ya wasomi vs kada zingine. Sema mpango wa taifa ni framework tu mfano watasema Huduma za afya kupitia bima ya wote. Sasa mpango wa miaka mitano mitano ndio utaeleza KIVIPI hiyo vision inatekelezeka.

4. Ila miaka yote tatizo sio uandaaji mpango ila utekelezaji. Mfano mpango wa 2015-2020 ulisema Tanzania nchi ya viwanda alafu wa 2021-25 unasema tumeshavuka kuwa nchi ya viwanda eti sasa tunafanya value addition ili kuuza nje na sio kuuza raw material kama zamani. Ni maneno ya karatasi tu ila hakuna hata kiwanda kimoja cha kueleweka hapa nchini mfano say magari, ndege, kuchenjua dhahabu n.k
 
Hiyo kamati ya kuandaa dira. Ina ma polofesa na wakubwa walewale pia ina "vijana" ila ni watoto wa wakubwa walewale. 🤣🤣🤣. Labda huyo jamaa mmoja wa startup ndio namuonaga mitandaoni.

Hayo maoni sijui watayakusanyaje? Na kama yanachambuliwa na mapolofesa hao walioshindwa miaka na miaka, je hapo kuna dira? Au ni ulaji wa kupiga hela na maposho. Utasikia bilioni miamoja na tisini na tisa nukta tisa, tisa ,moja ,nane, zimetumika kuandaa dira 🤣🤣
Hiyo Dira hatuitambui
 
Prof Semboja for years anazunguka serikalini kuandaa documents; amepewa kazi nyingi zinakosa ufanisi kwa sababu most of time yupo occupied lakini pia kwa seniority yake alipaswa akae upande wa kuwakosoa wanaochipukia.

Kwenye policy amekuwepo for years na zote alizoandaa zikifanyiwa evaluation zimefeli......upo uwezekano anadictate mchakato kwa kujua au kutokujua na hivyo ikaja sera ya Semboja na siyo sera ya nchi.

Huyu anawakilisha wengi walioteuliwa hapo. Karne hii policy formulation siyo kazi ya watawala na wasomi......wao kazi yao ibaki kuandika siyo kuratibu mchakato
 
1. Mbona hawa wamo au hujamuona Rais wa Tanzania Startup association. Pia yumo Dk Neema Mduma ndio ali design mifumo ya machine learning kubashiri mabinti kuacha shule kisa ujauzito!!. So watu wa technology ni wengi humo. Pia wapo wajasiriamali mfano hapo Mgetta she's an entrepreneur pia board member Tantrade.

2. Why academicians? Dunia nzima kazi za consultancy na strategic plans hakuna watu better kuziandaa kuliko Academicians. Hawa laymen/wafanyabiashara wataitwa tu watoe maoni ila wanaoandaa draft zile have to be academicians maana wamebobea kwenye hizo mambo kwa miaka mingi.

Ambacho labda hakijakaa sawa kama ulivyosema ni balance ya wasomi vs kada zingine. Sema mpango wa taifa ni framework tu mfano watasema Huduma za afya kupitia bima ya wote. Sasa mpango wa miaka mitano mitano ndio utaeleza KIVIPI hiyo vision inatekelezeka.

4. Ila miaka yote tatizo sio uandaaji mpango ila utekelezaji. Mfano mpango wa 2015-2020 ulisema Tanzania nchi ya viwanda alafu wa 2021-25 unasema tumeshavuka kuwa nchi ya viwanda eti sasa tunafanya value addition ili kuuza nje na sio kuuza raw material kama zamani. Ni maneno ya karatasi tu ila hakuna hata kiwanda kimoja cha kueleweka hapa nchini mfano say magari, ndege, kuchenjua dhahabu n.k
Hahaha nimecheka sana

Haha entrprinuaaa😂

Oky
 
Back
Top Bottom