Walioandamana Kumpinga Dk.ngasongwa Kushtakiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walioandamana Kumpinga Dk.ngasongwa Kushtakiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Augustoons, Mar 6, 2008.

 1. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Jamani hivi hawa ndio viongozi wetu? hawa wanawakilisha maslahi ya nani? ndugu wadau,hebu tuangalie uhalali wa haya mambo

  na George Maziku  WANANCHI walioandamana wilayani Ulanga, mkoani Morogoro kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumwacha Dk. Juma Ngasongwa katika uteuzi mpya wa Baraza la Mawaziri alioufanya hivi karibuni, wameingia matatani na wanaweza kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa, Tanzania Daima imegundua.
  Katika hali ya kushangaza na inayoashiria kuwa suala hilo lina shinikizo la kisiasa, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Dk. Rajabu Rutengwe na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo Suleiman Magoto, ndio wanaoshika bango la kutaka wananchi hao washitakiwe.

  “Tumeamua kuwakamata na kuwafikisha mahakani watu wote walioandamana siku hiyo kwa sababu maandamano yao hayakuwa na kibali,” alisema mkuu huyo wa wilaya alipozungumza na gazeti hili juzi kupitia simu yake ya kiganjani.

  Pia mwandishi wa habari wa gazeti lililoripoti kuhusu maandamano hayo (si Tanzania Daima) anatafutwa na viongozi hao wa serikali na CCM ili aunganishwe na wananchi hao kujibu mashitaka yanayowakabili.

  Dk. Rutengwe anamlalamikia mwandishi wa gazeti lililoandika habari ya maandamano hayo kwa kile alichodai kuwa kwanza mwandishi hakuwa na kibali cha viongozi wa wilaya hiyo cha kumruhusu kuripoti habari hiyo, pili habari yenyewe ni ya kuchochea chuki.

  “Huyu mwandishi kwanza ni mchochezi, anaandika habari za kuchonganisha wananchi na viongozi wao, na isitoshe hakupata kibali chetu kama viongozi wa wilaya kumruhusu kuandika habari hiyo, hayo ni makosa makubwa”, alisisitiza Dk. Rutengwe.

  Siku mbili tu baada ya Rais Kikwete kutangaza baraza jipya la mawaziri, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, ambapo aliwatupa nje baadhi ya mawaziri waliokuwa katika baraza la kwanza akiwemo Dk. Ngasongwa, gazeti moja la kila siku liliripoti kuwa wananchi wa tarafa za Malinyi na Mtimbira wilayani humo, waliandamana kumpongeza Rais Kikwete kwa kutomteua Dk. Ngasongwa katika baraza hilo.

  Naye mwenyekiti wa CCM wilayani humo, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa uongozi wa chama hicho wilayani Ulanga ulikuwa umekasirishwa mno na kitendo cha wananchi hao kuandamana kwa kumkejeli Dk. Ngasongwa, ambaye ni mmoja wa wabunge wawili wa CCM wilayani humo.

  “Tumekubaliana na DC ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya yetu kuhakikisha watu wote walioandamana, pamoja na mwandishi aliyeandika habari hiyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani haraka.

  “Si uungwana hata kidogo watu kushangilia kuanguka kwa mwenzao. Ngasongwa bado ni mbunge, kitendo cha kuandamana kumpongeza rais na kumkejeli mbunge ni kosa, ni lazima wahusika watuambie wamepata wapi utamaduni huo,” alisisitiza Magoto.

  Lakini wananchi walioshiriki maandamano hayo, walipoongea na gazeti hili kwa njia ya simu za kiganjani, kwa nyakati tofauti na kwa sharti la kutotajwa, walisema hawakufanya kosa lolote kwa kuandamana kumpongeza rais wao kwa kuteua baraza zuri la mawaziri.

  Pia walisema hawakutenda kosa lolote kwa kuonyesha hisia zao dhidi ya mbunge wao, ambaye walidai hajatekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2005, na kwamba kama watakamatwa na kushitakiwa kwa kitendo hicho basi huo ni udikteta wa hali ya juu.

  “Hii ni demokrasia gani? Hivi kweli hata tukitaka kumpongeza rais kwa kazi nzuri lazima tuombe kibali? Huyu DC ni wa kizazi kipi? Mbona anataka kubana uhuru wa binadamu?” alihoji mmoja wa watu walioshiriki maandamano hayo ambaye aliliambia gazeti hili kuwa huenda yeye akawa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo.

  Hata hivyo, baadhi ya watu walioshiriki maandamano hayo wameapa kupambana na kwamba wapo tayari kufunga safari kwenda Dar es Salaam kuonana na Rais Kikwete, ili wamfikishie kilio chao kuhusu manyayaso waliyodai kuyapata kutoka kwa viongozi wao wa wilaya kutokana na kitendo chao cha kuandamana kumuunga mkono.
   
 2. K

  Kasana JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2008
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hawa viongozi wetu, yaelekea watakuwa wameshinikizwa na huyo 'aliyekejeliwa'.
  Wakati wanandamana hawakuwaona? kwa nini FFU hawakuwatimua au kuwarushia mabomu kama yale ya mwembechai kama hawakufuata sheria.

  vikaragosi na kuzomea na kwenyewe si kukejeli?

  Hawa viongozi wanafikiri wananchi bado wako enzi zile za kutojua haki zao.

  Viongozi wa ulanga it is too late. Wanajua wanachokifanya, wanatumia haki yao ya kidemokrasia.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Unajua kama hawa jamaa wa Ulanga wangeandamana bila kibali kushangilia ujio wa "masah" Bush, wasingeingia matatani!

  This tells you how our political structure is completely flawed. Hivi DC na DPC wamekaa kuangalia ni sheria gani ilivunjwa wakaweka vikao kucha kuchwa na kisha kufikia uamuzi wa kufanya utekelezaji wa haraka namna hii?

  I wish they could hev spend tume like this for development projects for Wananchi and not witchhunt!
   
 4. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa design hii ya kukamata watu bila mpangilio na kuwasweka ndani wamerithi enzi za ukiritimba na udikteta wa Nyerere.Hawataki kuambiwa ukweli na hawaelewi kero za wananchi.Hii ni sifa kubwa ya Mwalimu.Aliwasweka ndani mpaka wakazeekea huko...bila kuwafungulia mashtaka.Sasa kasumba hii itakwisha lini?
   
 5. D

  Dotori JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huku ndio kulewa madaraka. Tangu lini kuwa na furaha ni kosa.
   
 6. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiki ni kituko ambacho siamini kama kinaweza kufanywa na kiongozi wa serikali ambaye ni Dr. kwanza ni dokta wa kitu gani huyu bwana? nadhani hapa ndipo Kikwete anapopaswa kuona jinsi alivyo na viongozi mataahira. Yaani rais kafanya kazi nzuri, wananchi wanampongeza anatokea taahira mmoja na kuwakamata; kosa kumpongeza rais kwa kazi nzuri. Hii nchi hii? Sijui!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Jamani mwenye simu ya huyo Mkuu wa Wilaya naomba pleaase..
   
 8. R

  Ras-nungwi Member

  #8
  Mar 6, 2008
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ni Dr. (PhD) wa mama lishe.... eh nimesahau ni Dr. wa lishe bora
   
 9. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kuna haja wakuu wa wilaya wote nchini kupigwa msasa maana ya utawala bora ni nini,kwa kweli mwenzenu sina imani nao kabisa hawa jamaa,yaani huwa hawajui wanachofanya na kazi zao kule wilayani ni almost hazipo.Halafu wanavyojifanyaga watemi,nilimuona mkuu wa wilaya moja inaitwa kongwa alikuwa anaenda kutembelea vijiji mbona magari yote yalisimamishwa na alikuwa na msafara kama wa rais,nilicheka sana,nikasema ungejua hapa dar tunawaona wa kawaiiiiiiiiiiiiiiida hata msingempisha.Uongozi wao ndio hivyo wa kutishia tishia tu na umwinyi,hiki cheo kinafaa kifutwe,zaidi za ukada wa chama hawana kingine,tena wa sasa hivi wengi wao shule hazimo.
   
 10. S

  Siao Member

  #10
  Mar 7, 2008
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hao viongozi wa hiyo wilaya lazima akili yao ni ya chekecheke..! Hawa kwani hawakwenda Ngurudoto? lakini afadhali hata hawa kuliko wale waliokwenda ngurudoto....!

  Hata balozi wetu sio hivi...!!
   
 11. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hii ishu inanikumbusha kesi ya delegates wa FL, na MI........if you dont play by the rules................!!
   
 12. F

  FDR Jr JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2008
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji kaka yangu mtafute Absolom Kibanda Mhariri wa MT_Daima atakusaidia kumpata huyu Mzaramo wa bagamoyo Dkt Rutengwe, kwa ufupi hii ni vita dhidi ya Dkt Ngasongwa iliyoanza NEC 2007 na sasa jamaa wa mwananchi wakiendeleza kazi hiyo ingawaje hatujii who is behind this game.

  Dkt Ngasongwa tangu amepoteza nafasi ya uwaziri ndio leo hii asubuhi ameenda Malinyi ktk shughuli za kijimbo na haya maneno ya mkuu wa wilaya hayana chochote cha kumsaidia mbunge wake bali kumuangamiza, anataka aonekane kuwa amekerwa na amemlalamikia hivyo yeye anachukuwa hatua!!!!Uhuni huu!!Ukweli hakukuwa maandamano yoyote Malinyi wala Mtimbira yaliyofanywa na watu wa huko na yule kijana Mshamu aliyenukuliwa ktk Mwananchi ameshangazwa sana na yeye kuhusishwa na taarifa za uongo,ktk downfall kuna watu wenye roho nzito hufurahia na binadamu husononeka lakini wote wana haki sawa; ktk haya yote Dkt Rutengwe anajua anachokifanya ila tatizo CCM wameamua kulichunguza kichama na anajua itakapobainishwa nani wamehusika ktk kupotosha ngoma itafika juu ambako hataki ifike ndio maana kaja na kisa cha mahakama, tangu lini maandamano ya kumpongeza rais kumnyima mtu uwaziri yamekwenda mahakamani wana JF? Huu ni uhuni wa mkuu wa wilaya na wenziwe huko mkoani Morogoro.

  Huyu Mheshimiwa ameamua kuwa " Yake macho na Masikio wenye midomo waseme ila yeye ametulia"
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Kumbe bado tuna wakuu wa wilaya wenye mawazo mgando hadi leo?
  Yaani mwandishi wa habari lazima aombe kibali kuripoti habari kutoka wilayani? mbona mie ndio naisikia habari hii leo?
  Kazi kweli kweli!
   
 14. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  "Huyu mwandishi kwanza ni mchochezi, anaandika habari za kuchonganisha wananchi na viongozi wao, na isitoshe hakupata kibali chetu kama viongozi wa wilaya kumruhusu kuandika habari hiyo, hayo ni makosa makubwa”, alisisitiza Dk. Ruteng"


  Naye mwenyekiti wa CCM wilayani humo, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa uongozi wa chama hicho wilayani Ulanga ulikuwa umekasirishwa mno na kitendo cha wananchi hao kuandamana kwa kumkejeli Dk. Ngasongwa, ambaye ni mmoja wa wabunge wawili wa CCM wilayani humo.

  “Tumekubaliana na DC ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya yetu kuhakikisha watu wote walioandamana, pamoja na mwandishi aliyeandika habari hiyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani haraka.

  “Si uungwana hata kidogo watu kushangilia kuanguka kwa mwenzao. Ngasongwa bado ni mbunge, kitendo cha kuandamana kumpongeza rais na kumkejeli mbunge ni kosa, ni lazima wahusika watuambie wamepata wapi utamaduni huo,” alisisitiza Magoto.
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Namshauri mkuu wa wilaya ya Monduli nae afuate mfano wa huyu Dr Rutengwe ( whatever his name is ) awakamate na kuwafikisha mahakamni wale walioandaa maandamano ya kumpokea fisadi Lowasa kule Monduli.
   
 16. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  MWANAKIJIJI naomba ukipata namba ya huyo DC nipatie na mimi.
   
Loading...