Walioacha nyayo za kale waliwezaje kutembea kwenye uji wa Volcano wa moto?

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Kuna baadhi ya rekodi za historia nahisi hazijakaa sawa,
au inawezekana labda mimi ndio nina kichwa kigumu kuelewa lakini naamini kutakuwa na wataalamu wa kulifafanua hili jambo vizuri,

Utata wangu upo kwenye ugunduzi wa nyayo za watu wa kale ambazo wataalamu wanasema kwamba hizo nyayo zimetokea (zimebakia) baada ya kutokea volcano kisha hao watu kukatiza juu ya uji uji/ majivu ya volcano...
Sasa kama tunavyojua kitendo cha watu hao kuacha nyayo inamaanisha kwamba walikuwa wanatembea peku,
Sasa swali ni je,
hivi kuna kiumbe ambaye anaweza kuhimili na kukatiza(kwa madaha) juu ya uji wenye moto wa volcano??
Hao watu walioacha nyayo walikuwa na miguu yenye ugumu wa namna gani isiyohisi maumivu?
-
Sitaki thread iwe ndefu,
aliyeelewa ashushe nondo.... Karibuni
 
Nilivyoona hedin nikaja mbio kwa kujua ni kuhusu wanawake, hahahaha kumbe leo uko kihistoria zaidi
 
Tazama picha hii Volcanic ash inavyosumbua majivu haya huwa hayaunguzi hupoa haraka
2313510-3x2-940x627.jpg
 
Ukitaka ujue kiwango cha juu kbsa cha uongo wa binadamu, basi fuatilia historia
Asikuambie mtu MABABU zetu walijaaliwa uongo sana, na ukijitia kumpinga anakutishia nyie kizazi cha nyoka mtapata laaana
 
Haswa huwa ni mvua,halafu yanakuwa tope zito,hata leo ukiwa arusha mvua zikinyesha bado mabaki ya majivu ya mlima meru utayaona.
Kwa jinsi yalivyokuwa malaini(majivu) nadhani yakinyeshewa na mvua lazima yatapoteza umbo lake la asili kabla ya kuanza kuganyiana, ukitaka kuamini kakanyage cement alafu mwagia maji kwajuu
 
Back
Top Bottom