Walio nyuma ya mgomo wa madaktari ni hawa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walio nyuma ya mgomo wa madaktari ni hawa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rugo, Jul 2, 2012.

 1. r

  rugo Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, wahusika wakuu katika kuchochea mgomo wa madaktari nchini ni wanasiasa (WABUNGE). Nasema ni wabunge kutokana na urafi na ubinafsi wao unaotokana na kujiongezea mishahara na posho kila mara huku watumishi wa umma ambao ndio wanafanya kazi kubwa katika ujenzi wa taifa wakiambulia mishahara kiduchu na mazingira magumu ya kazi. Nasema hawa waishiwa ndo chanzo kikuu cha mgomo huu kwa sababu, hebu angalia, mgomo wa mwezi wa pili mwaka huu ulikua baada ya taarifa kuvuja kuwa waishiwa hawa wamejiongezea posho na mshahara. Angalia mgomo unaoedelea sasa nao ukiangalia umekua baada ya taarifa kuvuja kuwa waishiwa mjengoni wamejiongezea tena mshahara kwa kazi ya kusinzia na kuzomea wanaopinga uozo kwa hoja. nawasilisha.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  inasikitisha sana,tuwapige mawe nini?
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Wanatafuta mchawi wakati wachawi wapo wanaonekana waziwazi
   
 4. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nashauri wabunge wawe na maximum qualification of Form 4.Tu.
  Kwani hawa wenye PHD,Masters and Madegrees wameshindwa kutumia elimu yao kuendesha Taifa hili,badala yake wanatumia hayo makwalifications kutuibia na kutesa watanzania.

  wasomi wote wasiwe wabunge,na kuwa Waziri asiwe mbunge,wabunge watuwakilishe wananchi Tu,Raisi achague mawaziri mtaani.Wawe wasomi ili watekeleze matakwa ya wabunge wetu wa Form $.

  What is the point Mtu na PHD yake anaenda kusinzia Bungeni.
   
 5. O

  Original JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Lakini madaktari wana akili ya kitoto. Mwenzako akipata kwani ni lazima na wewe upate?. Na kama kuna ulazima wa wewe pia kupata ndiyo uweke maisha ya watanzania hatarini?. Udoctor ni wito na walikula kiapo kuifanya kazi hiyo. Kwa kugoma kwao ni sawa na uuaji inatakiwa tuwafungulie kesi ya uuaji wapuuzi wakubwa madaktari wa hapa Tanzania.
   
 6. M

  MTENGE Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchawi mkubwa ni Serikali yenyewe, kwa matumizi yasiyo ya lazima, kama kununua mashangingi mafano tume ya kuratibu katiba , safari ambazo sio muhimu na convoy kubwa, matumizi makubwa ya sherehe kama miaka 50 ya uhuru, tume zisizo na tija, posho kwa viongozi kuwa kubwa sana mfano wajumbe wa kamati ya kuratibu katiba kila siku 450,000/ kwa miezi yote 18 wakiwa kazini
   
 7. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Pumbaaaaaaaaaaa
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wabunge ukiangalia mishahara yao including allowances sio chini ya million 5, why? mbunge na daktari yupi ni more important kwenye jamii, alafu cha ajabu wanazidi kuongeza mikoa,wilaya,majimbo kwa hiyo idadi iya wabunge itazidi kuongezeka, wanajinufaisha wao kwanza.
   
 9. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu, unaowazungumzia ni wabunge wa nchi gani? Au labda wewe current news zinakupita kushoto sana! Wabunge wetu wa Bunge tukufu la JMT ni juzi tu wameongezwa mishahara hadi milioni 10 kwa mwezi, wewe unazungumzia milioni 5 za wapi??/
   
 10. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  MTENGE nakubaliana nawe kwa 100% kuwa mchawi mkuu ni serikali yenyewe. Mifano ya huo uchawi wake ni mingi mno mfano serikali inanunua mashangingi kwa viongozi wote kuanzia waziri mpaka mkuu wa wilaya achilia mbali kwa ajili ya kurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali kisha anatokea mjinga mmoja kwa tabasamu kuuuuubwa eti anazindua bajaji ambazo zimenunuliwa ili wananchi watumie kama ambulance!

  Pesa za matumizi yasiyo na tija zipo lakini za kununulia vitanda walao hata vya wodi za wajawazito na watoto hakuna!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  usiku wake alikuwa anaimba nyimbo za mipasho za chama chao na akaishia kupumzika na lulu, what do u expect????
   
 12. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kama ni rahisi kiasi hicho mbona wewe hujaitikia huo "wito"!
   
 13. n

  ngokowalwa Senior Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inategemea unaliangalia kutokea kona ipi. Kwa wananchi Dakitari ni muhimu kwa sababu kutoka kwao wanapata huduma za afya ambazo zinawagusa moja kwa moja. Kwa serikali Bunge ni muhimu maana ndilo linapitisha/bariki mafungu na pia likiwa kinyume serikali inatambua linaweza kuipelekea kwenye kurudia uchaguzi kitu ambacho kwetu hapa serikali itahakikisha hakitokei kwa kuhakikisha chombo hiki hakina malalamiko ya kimaslahi - lol
   
 14. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Ilifaa wabunge wapokee milioni moja na nusu.
   
 15. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Tena wanasiasa walivyokuwa punguani huwa wanajidai kuhoji kwenye porojo tu lakini ikifikia suala la kuongezewa anasa zao kama posho na mengineyo wote wanakuwa wamoja.Yaani itaniwia vigumu sana kurudisha imani na siasa uchwara za bongo.
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Wabunge wamezidi kujenga tabaka ndani ya nchi yetu
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii nchi inakoelekea tutagawana kila mtu chake maana madai ya wananchi kwa serikali ni mengi kana kwamba ikilipa itafilisika
   
 18. M

  Miranda Michael Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 19. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Serikali ijipange upya kwenye hili la mishahara kwa ngazi zote za wafanyakazi.
   
 20. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,401
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mpuuzi ni wewe mwenyewe ambae unabwabwaja hovyo.Wengekuwa na akili ya kitoto ungekuwa unawapeleka mkeo/watoto wako wakawatibu.Mtu mzima ovyo.
   
Loading...