Walio na Tamaa Utawajua

Walio na Tamaa Utawajua

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Habari zenu marafiki zangu

Awali ya yote nimeonelea niseme jambo hili ambalo limenishangaza na tena
kuniogopesha na zaidi ya yote limenifanya nianze kuwawaogopa wale
ambao maisha yao siku zote wanaishi kwa tamaa mbaya, sisemi kuwa
mtu asitamani kitu wala asitamani mtu la hasha nasema wengine wamevuka
mipaka yao mpaka wanamtenda Mungu dhambi kwa tamaa zao wenyewe
huku wakivutwa na zile roho zidangannyazo, na fikra zao zimejaaa uovu
mwingi sana.

Inashangaza sana kwanini mwanadamu anakuwa hana hofu ya Mungu,
wala haoni kuwa kuna Mungu aaonaye sirini kwa yale maovu anayomtenda
jamani kwaniini tunakuwa wanyama kiasi hicho? wewe una familia yako na
na mke wako unaanza kumtamani mke wa rafiki/ndugu yako hivyo? kwa
nini tunazoelea kuishi maisha ya dhambi, hiivi hamjui ya kuwa mshahara wa
dhambi ni mauti. Hebu ninikuu hapa : "Lakini kila mmoja hujaribiwa na TAMAA
zake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa, halafu ile Tamaa ikiisha
kuchukua mimba huzaa dhambi na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti"
hiyo inapatikana katika kitabu cha Yakobo 1:14
. Na vilevile ninukuu hapa:
Lakini zikimbie TAMAA za ujanani ukafuate haki na imani na upendo na amani
pamoja na hofu kwa wamwitao Bwana kwa mioyo safi."
mwisho wa kunu
kuu.

Ndugu zangu kwanini tunawashwa na Tamaa mbaya mpaka inatufanya
tumtende Mungu dhambi kiasi hichi kwanini unakuwa na tamaa ya kuwaza
kumgegeda mke wa rafikio, kuwaza kupokonya mali walizochuma wenzako,
kwanini tunakuwa mafisadi hata kwa nchi yetu wenyewe, tunaua watu kwa
ushirikina wa kutaka kutajirika haraka (shortcut), kwanini tunakuwa wakatili
jamani, hivi hatujui kuwa tutatoa hesabu ya mambo yetu tuliyofanya hapa
duniani iwe ni mazuri au mabaya? Pls marafiki Tamaa ni mbaya na inasababisha
mauti kwako na unaukosa ufalme wa Mungu.

copy: Mentor, Nicas Mtei, Paloma, The secretary, amu, watu8,
Bujibuji, Jiwe Linaloishi, Asprin, charminglady, FirstLady,
Passion Lady, Lady doctor, Bishanga, Mtambuzi, Excellent,
Kipaji Halisi, figganigga, manoah, Arushaone, Erickb52,
Ruttashobolwa, Mwita Maranya, Mjeda, Madame B, Smile
kisukari, Mwali, Preta, Chimbuvu, mathematics, stevoh,
Donn, Kaizer, KakaKiiza, Mr. rocky, Filipo, Mamndenyi,
Zion Daughter, Heaven on earth, @Fp, Elli59, lara 1, mwaJ,
jouneGwalu, Ben Saanane, Lady Na marafiki wengine karibuni

ciao
 
Last edited by a moderator:
mi huwa najisemehe hata Mungu akiamua assess watu wa kwenda mbinguni kwa kutumia amri moja tu ya usizini, mbinguni wataingia watoto tu, labda na mimi kwa upande wa wanaume, teh teh!
 
Laiti kusingekua na tamaa, maisha yangekuaje? Mimi nadhani suala kubwa hapa nikukumbuka kutubu kila saa na kila wakati, kila unapoona umekosea jaribu kuwa mnyenyekevu na kukubali toba. Hio ishu ya kutamaniana hio mmhh, mie ni muathirika sana wa hio but I always keep my mind straight. Sitaki eti nikishafanya ndio niseme "aaah nimefanya nini sas?"
 
kwani umeona dhambi kubwa ndo hiyo hakuna dhambi kubwa wala ndogo best zote ni dhambi na machukizo mbele za Mungu hivyo jitahidi sana usiishawishike na tamaa za ujanani au tamaa zako mwenyewe
mi huwa najisemehe hata Mungu akiamua assess watu wa kwenda mbinguni kwa kutumia amri moja tu ya usizini, mbinguni wataingia watoto tu, labda na mimi kwa upande wa wanaume, teh teh!
 
hapa umelonga mwana bigup ila tamaa zipo nzuri na mbaya laikini wanadamu wanakuwa upande mmoja tu wa mabaya na mema
Laiti kusingekua na tamaa, maisha yangekuaje? Mimi nadhani suala kubwa hapa nikukumbuka kutubu kila saa na kila wakati, kila unapoona umekosea jaribu kuwa mnyenyekevu na kukubali toba. Hio ishu ya kutamaniana hio mmhh, mie ni muathirika sana wa hio but I always keep my mind straight. Sitaki eti nikishafanya ndio niseme "aaah nimefanya nini sas?"
 
"Lakini kila mmoja hujaribiwa na TAMAA
zake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa, halafu ile Tamaa ikiisha
kuchukua mimba huzaa dhambi na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti"

umenikumbusha kwaya ya Bulyanhulu aisee, kuna wimbo wao mmoja wa kitambo sana una hicho kiitikio!

Unaipata hiyo nyimbo, nayoisema!!
 
Daaah naona kama nashindwa kuandika
nimepata kigugumizi
nitarudi tena hapa.
 
i love my principles.maumbea hayanihusu.Dhambi kwa maskini kumutamani Zahra White tajiri poa nitamutamani pia
 
Last edited by a moderator:
nimeipata hiyo wimbo unaousema best na nimeukumbuka nikifika home inabidi niusikilize
umenikumbusha kwaya ya Bulyanhulu aisee, kuna wimbo wao mmoja wa kitambo sana una hicho kiitikio!

Unaipata hiyo nyimbo, nayoisema!!
 
hee kumbe wewe uko studio - Kinondoni au siyo?
umenikumbusha kwaya ya Bulyanhulu aisee, kuna wimbo wao mmoja wa kitambo sana una hicho kiitikio!

Unaipata hiyo nyimbo, nayoisema!!
 
Hayo hayakuanza leo, kama historia inaonyesha hata Mfalme Daudi alimtamani mke wa huria. Wajua, kama wake wangekuwa wanyimi nadhani wengi wangeacha haka ka.. 'Mwana FA alisema, ukigongewa na wewe tafuta mnyonge wako...
 
kwani umeona dhambi kubwa ndo hiyo hakuna dhambi kubwa wala ndogo best zote ni dhambi na machukizo mbele za Mungu hivyo jitahidi sana usiishawishike na tamaa za ujanani au tamaa zako mwenyewe

maana yangu siyo bhana, namaanisha uzinzi ni dhambi inayowashinda wengi
 
lakini ni TAMAA inayokupelekea kufanya dhambi, wee unajua mwisho wa mfalme wa Daudi ulikuwaje pale alipoingia tamaa ya kumgegeda mke wa Huria, si alifanya dhambi ingine ya mauaji kwa kumuua Huria ili afiche uthibitisho wake, na mwisho wake si uanaujua best, mara nyingi tamaa mbaya hupelekea mauti hivyo nachosema hapo ni ile tamaa mbaya best nielewe
Hayo hayakuanza leo, kama historia inaonyesha hata Mfalme Daudi alimtamani mke wa huria. Wajua, kama wake wangekuwa wanyimi nadhani wengi wangeacha haka ka.. 'Mwana FA alisema, ukigongewa na wewe tafuta mnyonge wako...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom