Walinzi nane na wengine 12 wafikishwa Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,557
1594815537261.png

WALINZI nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo shtaka la wizi na utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh bilioni mbili mali ya NMB benki.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na

Wakili wa Serikali, Faraja Ngukah imewataja washtakiwa watano ambao ni ndugu kuwa ni Manjestus Mselema (44), Bernadetha (45) ambaye ni mama wa nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes (29) Hotelia, Oswald Mselema (49) na Olaph Mselema (35) ambapo wote ni walinzi.

Wengine ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor (39) na Sylidion Odil (42), Tulipo Mwamuzi (40) ambaye ni dereva, Grace Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal International Ltd, Godwin (52) Fundi Mwashi na Anold Erio (25), Florah Mwita (25) mfanyabiashara na Tispo Mwasakieni (27) maarufu Ronic Kinyozi na mkazi wa Kawe.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, wakili Ngukah amedai, katika tarehe tofauti mwaka 2020, maeneo ya Dar es Salaam washitakiwa Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na Odil walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu ili kufanya kosa la wizi.

Inadaiwa kuwa, Juni 8, 2020 huko maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya NMB Benki

Katika shtaka la tatu imedaiwa Juni 8,2020 huko katika maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa walijipatia Sh 2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.

PIA SOMA:
= > Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB
 
Kama upelelezi haujakamilika kwa nini mmewakamata? Hata hivyo hayo mazuzu yalitakiwa yapigwe risasi hadhalani hadi yafe.
 
Hawa ni wapumbavu kabisa wacha wasulubiwe walishindwa kuziacha zipoe kwanza
Unahuzunisha sana na kukasirisha sana.

Lakini tusisahau hawa walinzi wengi shule ndogo na njaa kali sana. Wanalinda billions of money mshahara laki 2, mtu wa hivyo ataacha milioni 20 zikae ndani tu zipoe kweli?

Kuna wale wenzao wa waliiba wakaenda kununua vitanda, makochi, sofa sets, makabati, ist, viwanja na kujenga hata mwezi haujaisha.

Ukiangalia cases za hawa wezi wote wanakimbilia kununua furniture za ndani, gari, viwanja na nyumba haraka haraka hata wiki 2 hazijaisha. Hawa wote wamejaa njaa tupu.

Tusiwalaumu sana, kwa akili zao wako sahihi.

Bank au security companies hawawezi kuajiri kazi ya ulinzi watu wenye akili kubwa na wasomi maana wanajua mtacheza deal very smart, mtakula hela na hata mkikamatwa kesi itakosa ushahidi mtaachiwa kula hela.
 
WALINZI nane wa Kampuni ya Ulinzi ya Security Group ya Afrika (SGA) Tanzania Ltd na wenzao 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo shtaka la wizi na utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh bilioni mbili mali ya NMB benki.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na

Wakili wa Serikali, Faraja Ngukah imewataja washtakiwa watano ambao ni ndugu kuwa ni Manjestus Mselema (44), Bernadetha (45) ambaye ni mama wa nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes (29) Hotelia, Oswald Mselema (49) na Olaph Mselema (35) ambapo wote ni walinzi.

Wengine ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor (39) na Sylidion Odil (42), Tulipo Mwamuzi (40) ambaye ni dereva, Grace Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal International Ltd, Godwin (52) Fundi Mwashi na Anold Erio (25), Florah Mwita (25) mfanyabiashara na Tispo Mwasakieni (27) maarufu Ronic Kinyozi na mkazi wa Kawe.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, wakili Ngukah amedai, katika tarehe tofauti mwaka 2020, maeneo ya Dar es Salaam washitakiwa Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na Odil walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu ili kufanya kosa la wizi.

Inadaiwa kuwa, Juni 8, 2020 huko maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya NMB Benki

Katika shtaka la tatu imedaiwa Juni 8,2020 huko katika maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa walijipatia Sh 2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana.

PIA SOMA:
= > Dar: Polisi wakamata watu 32 kwa wizi wa Bil 2.082, ndani ya benki ya NMB
Hawa walinzi binafsi wengi ni mawenge hawana ufahamu wowote wa wizi,issue kama hizo zinasukwa mapema! Wamsome mtu kama Hashpappi alivyokuwa anawaliza watu!! Mpunga kama huo 2B halafu watu zaidi ya 12 mtagawanaje? Sasa 200m+ ndio zikuweke mashakani na kupotea?
 
Mashtaka ya serikali yetu bana, watu wameiba lakini mwendesha mashataka anataka kunyumbua kosa moja yawe makosa kumi. Ni upumbavi tu na akili za kikoloni.
 
Back
Top Bottom