Walindwe: Umuhimu wa WHISTLEBLOWERS Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walindwe: Umuhimu wa WHISTLEBLOWERS Tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Indume Yene, Dec 10, 2008.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tumekuwa tukiona na kusikia matukio mbalimbali nchini kama vile skendo ya EPA, Meremeta, Deep Green Finance na hata sakata mpya kati ya Mh. Masha na Bw. Mengi. Naamini Mh. Slaa alipata msaada kutoka kwa whistleblower(s) kwa njia moja au nyingine alipotoboa siri ya majina ya watu pamoja na makampuni yaliyojihusisha wizi huo. Na mpaka leo hiyo inabaki siri yake Slaa na Whistleblower(s). Pamoja na hayo kuna issues nyingi ambazo zimeibuliwa na whistleblowers na imekuwa ni faida kwa serikali na wananchi. Mfano tumesikia pesa hizo ambazo zilizochotwa kwa udanganyifu kutoka BOT zilipaswa zirudishwe serikalini na kutumika kwa ajili ya maendeleo ya kilimo. Sina hakika kama zimeshapelekwa katika mfuko huo ila ninachojua ni kuwa Rais Kikwete alitoa amri kuwa hizo pesa zipelekwe kwenye huo mfuko kwa ajili ya maendeleo ya kilimo.

  Kuhusu sakata ya Mh. Masha na Mengi, nimesoma katika gazeti la Mtanzania Daima kuwa sasa serikali inamtafuta kwa udi na uvumba mtu aliyetoa hiyo siri ya kikao hicho kwa Bw. Mengi. Kama ni kweli serikali imeamua kufanya hivyo maana yake ni kuwa inakiri kuwa kulikuwa na kikao cha ngazi ya juu (Usalama) na wakajadili hilo suala la kumchezea faulo Bw. Mengi.
  Mie siamini hata chembe kama hatua ya kumfilisi Bw. Mengi ingekuwa na faida kwa usalama wa taifa. Zaidi ingeleta matatizo ya kiuchumi kwa wananchi ambao wameajiriwa na makampuni yaliyo chini ya himaya ya Bw. Mengi.

  Kutokana na huyu Whistleblower:-
  i/. Uonevu kwa raia unaoendeshwa na baadhi ya viongozi wa serikali wajulikana. Viongozi kutumia vyeo vyao kuwakandamiza raia.

  ii/. Wananchi wamesaidiwa ku-keep kazi zao katika makampuni yaliyo chini ya Himaya ya Bw. Mengi. Watu wengepoteza kazi kama Mengi angefilisiwa.

  iii/. Wanafamilia ya wafanyakazi wa Mengi wangeathirika kwa njia moja au nyingine kama vile watoto wao wengekosa ada za shule. Na kama wangekosa ada maanayake wangekosa hata elimu.

  iv/. Mashule wanayohudhuria hao wanafamilia vilevile wangeathirika kiuchumi kwa kukosa hayo mapato (Ada).

  v/. Serikali ingekosa mapato ambayo yangetokana kodi inayolipwa na makampuni ya Bw. Mengi

  vi/. Whistleblower amedhihirisha kuwa kuna baadhi ya viongozi hata wa kitaifa wana-support ufisadi pamoja na kwamba Mh. Kikwete kaanza kupeleka VIDAGAA mbele ya sheria.
  Mengine wanajamvi mnaweza kuongezea hapa.

  Hivyo basi ni muhimu kuwalinda hawa watu (Whistleblowers) kwa manufaa ya Taifa. Na kama kweli serikali iko katika mkakati huu wa kumtafuta kiongozi ambaye alikosekana katika kikao hicho cha kumhujumu Bw. Mengi, kwa manufaa ya UMMA tafadhali serikali isimamishe mpango huu.
  Huo utumbo wa kumkandamiza Mzalendo kisa vyombo vyake vinapiga vita UFISADI hauwezi kukubalika mbele ya Umma. Tuongeze juhudi kwa kuibana serikali kuhakikisha inatii sheria na katiba, vilevile kuhakikisha inawapeleka wahusika wote kwa njia moja au nyingine katika Ufisadi mbele ya sheria.

  Mchango wa maoni unakaribishwa.
   
Loading...