Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,054
Nimepata taarifa toka kwa wadau ambao walihudhuria kikao hicho kilichokuwa chini ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Masasi, kuwa walimu zaidi za 50 kutoka shule 10 wilayani humo waliitwa katika ukumbi wa shule ya wasichana Masas ili kushinikizwa kwa kilichosemwa kuwa WANAAZIMWA hivyo siyo uhamisho hivyo hawana stahiki zozote za kulipwa.
Zoezi hilo lilihudhuriwa na maafisa wa TAKUKURU ngazi ya wilaya, maafisa wa jeshi la police, wakaguzi wa elimu na idara ya TSD. Mmoja wa walimu hao amesema kwamba, sifa zilizotumika kuteua walimu hao ni idadi ya vipindi kwa kila mwalimu jambo ambalo halijazingatiwa kwani walimu wenye vipindi vitatu wamebaki makazini na wale wenye vipindi vingi kama somo la kiingereza ambao wengi wao wana vipindi hadi 30 ndio ambao wamechukuliwa.
Mmoja wa walimu hao ameeleza pia mvutano ambao ulitawala kikao hicho ambacho kiukweli inaonesha wakuu wa shule wametumia chansi hiyo kuwaondoa wale wote waliohoji utawala.
Hii ndiyo Tanzania ya sasa yule great thinker anayehoji hoji mambo ya msingi anachukuliwa kama adui. Na yasemekana Halmashauri hiyo haijawahi kufanya vizuri hata ktk mitihani ya ngazi ya mkoa wa mtwara kutokana na plans nyingi za idara ya elimu kuwa hovyo.
My take: Hii mikoa ya kusini inatakiwa iangaliwe kwa ukaribu sana hasa katika elimu. Hivi mwl wa sekondari aliyesomea vitu tofauti kabisa na vya shule ya msingi atawezaje kufundisha level ambayo hata masomo yake yanatofautiana?
Naamini tutasikia sarakasi nyingi sana za viongozi wetu.