Walimu watoboa mahusiano ya mwenzao, rpc barlow | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu watoboa mahusiano ya mwenzao, rpc barlow

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]
  Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana wamevunja ukimya na kueleza kile kinachodaiwa ni mahusiano kati ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, na mwalimu mwenzao, Dororth Moses.


  Wakizungumza na NIPASHE shuleni hapo jana, pia walielezea kusikitishwa kwao na jinsi tukio hilo la mauaji ya RPC lilivyotokea mbele ya mwalimu mwenzao, Doroth Moses aliyeuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi eneo la Kitangiri, jijini Mwanza.


  Mwalimu Doroth ndiye aliyekuwa na RPC Barlow ndani ya gari wakati watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walipowavamia na kumuua kwa kumpiga risasi Kamanda huyo.


  Katika mahojiano hayo Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Mary Ngalula, alisema wanamuonea huruma mwalimu mwenzao kutokana na kushuhudia tukio hilo la kutisha.


  Alisema wanamsikitikia kwa sababu jamii imeanza kumfikiria vibaya kwa kudhani anahusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.


  “Tunamuonea huruma mwalimu mwenzetu kutokana na maneno tunayoyasikia, lakini sisi tuko pamoja naye kwa sababu tunamfahamu ni mtu safi, na hivi tunajiandaa kwenda kumuona na kumtia moyo ili amudu kuilea familia yake kwani ni mjane,” alisema.


  Mwalimu Baraka Magafu alisema tofauti na hisia za baadhi ya watu kuhusu uhusiano wa Mwalimu Doroth na Kamanda Barlow, wao (walimu) wanafahamu kuwa ni watu wa kabila moja wanaotoka kijiji kimoja huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.


  Alibainisha kuwa Mwalimu Doroth amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (Wachaga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.


  “Ukifuatilia mwenendo wa tukio lote, utaona kwamba kilichotokea ni bahati mbaya na kingeweza kumtokea yeyote, kwani Barlow alikuwa akimsindikiza Mwalimu Doroth nyumbani kwake, na hata baada ya tukio, alipowapigia simu wenzao waliokuwa nao kwenye kikao walikuwa ndipo na wao wanafika majumbani mwao,” alisema.


  Aliongeza kwamba katika mazingira kama hayo ni makosa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Mwalimu Doroth kama ambavyo baadhi ya watu wameanza kuvumisha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.


  Wakati huo huo, majonzi, simanzi na kauli za kulipa kisasi ni miongoni mwa mambo yaliyogubika shughuli ya kuuaga mwili wa Barlow.


  Mwili wa Barlow uliagwa na wakazi wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, katika shughuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jana.


  Baada ya shughuli ya kuagwa mwili wa Barlow, ulisafirishwa baadaye jana jioni kwa ndege kuelekea jijini Dar es Salaam kabla ya leo kusafirishwa kwenda kijijini kwake Vunjo, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

  Chanzo:Nipashe

   
 2. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  screaming headline utumbo mtupu nipashechoka mbaya
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  absolutely. i agree with u!
   
 4. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mbona habar nyepesi sana? sensationalism hii!!
   
 5. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,245
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Naacha kusoma magazeti!
   
 6. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nipashe wikienda..udaku mtupu..tupa kule..!!
   
 7. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sikumbuki mara ya mwisho kusoma magazeti ya numbani ilikuwa lini. Huwa nayapitiapitia humu mtandaoni.
   
 8. Ghiti Milimo

  Ghiti Milimo JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 60
  So and I!
   
 9. controler

  controler JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya maelezo wakayatoe polisi yatasaidia wakati wa uchunguzi waache kutupigia kelele! Gademit
   
 10. L

  Luushu JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 593
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Pole familia ya marehemu,pole mwalimu kwani nijuavyo utasota ingawa huna kesi ya kujibu
   
 11. l

  leekud Member

  #11
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kazi wanayo ya kuchunguza la mwangosi bado linasumbua. la Mbagala limeenza na hili lina hitaji uchunguzi. Ila kwa nini hakuna anayesema kwa nini alitumia gari binafsi na ni usiku wakati yupo titled kutumia dereva.
   
 12. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanafiki hawa. Nani anajua mahusiano ya ndani. Kwani ile kitu wanasimuliana?
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Very predictable. Mwalimu mkuu angesema anajua dorothy anatembea na marehemu mbona tungemshangaa!
   
 14. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...suala la uhusiano wa kimapenzi kati ya mme/mke wa mtu ni jambo la siri sana kati ya watu wawili,sioni sababu ya hao waalimu kuwa wasemaji wa mwalimu Doroth,kama walikuwa na uhusiano wa kimapenzi au la,ni marehem na Doroth wanaojua ukweli...hizo stori za eti wana mfaham mwalimu Doroth ni mtu safi hazina mashiko,kwani mtu safi ndo hana hisia za mapenzi?...Mwalimu Doroth na Kamanda
  Barlow, wao (walimu)
  wanafahamu kuwa ni watu wa
  kabila moja wanaotoka kijiji
  kimoja huko Vunjo mkoani
  Kilimanjaro,kama hawa watu waliafahamiana tangu huko kijijini kwa Vunjo,kwa nini hao walimu wanataka kutuaminisha kwamba watu wanaofahamiana si raisi kuwa wapenzi?...
   
 15. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  just like shigogo papers.headline compared to body.utumbo mtupu.
   
 16. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Nimeacha bia yangu nakuja mbio kumbe utumbo mtupu!!!!!!!!
   
Loading...