Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimeipa serikali mwezi mmoja kuanzia jana, kuwalipa Sh13 bilioni wanazodai walimu vinginevyo itatangaza mgogoro utakaosababisha walimu kugoma nchi nzima.Hatua hiyo inatokana na kikao cha dharura cha baraza la taifa la CWT, kilichofanyika wiki hii mkoani Morogoro ambacho kilijadili matatizo ya walimu. Rais wa CWT, Gratian Mkoba akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, alisema fedha hizo ni madeni yanatokana na malimbikizo ya mishahara na madai mengine.Miongoni mwa matatizo makubwa yaliyojadiliwa ni malimbikizo ya madeni ya walimu yanayozidi kuongezeka siku hadi siku, alisema Mkoba.
Mkoba alisema madai mengine ni ya walimu waliopandishwa madaraja lakini hawajarekebishiwa mishahara yao kuanzia tarehe ya kupandishwa.Madai mengine alisema yanawahusu walimu waliopandishwa madaraja na kurekebishiwa mishahara yao lakini hawajalipwa fedha za malimbikizo yao kuanzia siku walipopandishwa. Aliongeza kuwa madai mengine wanayodai ni ya walimu ambao mishahara yao haikutolewa kwa wakati na hivyo kuwa na malimbikizo ya mishahara ambayo haijatolewa kipindi cha nyuma. Kama nilivyotaja matatizo hayo ya walimu, kama hayatakuwa yamepatiwa ufumbuzi ifikapo Julai 31 mwaka huu, CWT kitatangaza mgogoro dhidi ya serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, alisema Mkoba.
Ikiwa walimu watafikia uamuzi wa kugoma, upo uwzekano mkubwa wa kuathiri mitihani ya taifa ya darasa la saba ambao hufanyika kati ya mwezi Agosti na Septemba, na ule wa kidato cha nne ambao hufanyika kati ya mwezi Septemba na Oktoba kila mwaka.
Walimu ndio wasimamizi wakuu wa mitahi hiyo ya kitaifa ambayo kwa darasa la saba hutumika kupatikana kwa wananfunzi wa kuingia kidato cha kwanza, wakati ule wa kidato cha nne hutumika kupata wananfunzi wa kujiunga na kidato cha tano.
Matatizo mengine
Aidha Mkoba alisema tatizo jingine ambalo linakikabili chama hicho ni baadhi ya walimu kutopandishwa madaraja licha ya kustahili kama miongozo inavyosema. Hivi sasa lipo tatizo kubwa la walimu walioajiriwa mwaka 2007 au kabla yake ambao hawana matatizo ya kiutumishi lakini hadi sasa hawajapandishwa madaraja, alisema Mkoba. Aidha, Mkoba alisema sababu nyingine iliyosababisha kufikia aumuzi huo ni kutokana na waraka wenye kumbukumbu namba A/AC44/45/01/84 wa Desemba 2009 ambao unawashusha walimu vyeo.Walimu hawa baada ya kumaliza masomo ya shahada ya kwanza, waraka huo unawataka kuanza kazi kwa vyeo vya daraja la D wakati walikwishalipitia kabla hawajaenda vyuoni, alisema Mkoba.
Mkoba alisema walimu wengi walioathirika na waraka huo ni wale ambao kimuundo walikuwa walimu au maafisa elimu wasaidizi ambao wamefanya kazi muda mrefu. Tunaona kwamba haki ya walimu inazidi kupuuzwa siku hadi siku licha ya mchango wao mkubwa wanaoutoa katika jamii, sasa tunaona umefika wakati wa kuchukua hatua kama serikali itaendelea kupuuzwa, alisema Mkoba Serikali ya awamu ya nne imekuwa ikijikuta ikiingia kwenye mgogoro na walimu mara kwa mara kwa kile kinachoelezwa kuwa serikali inapuuza sekta hiyo. Mara kadhaa serikali imechukua hatua za kuwalipa walimu malimbikizo lakini inaishia kueleza kwamba baadhi ya madai ni ya udanganyifu jambo ambalo bado limekuwa likiendelea kujenga uhasama baina yao. Wakati wakilipwa malimbikizo yao miaka miwili iliyopita, baadhi ya walimu walilalamika kwamba walikuta viwango vya malimbikizo yao vikiwa vimepunguzwa na kulazimishwa kusaini ili wachukue kiwango walichandikiwa.
Gazeti hili liliwahi kumnukuu Mkoba mwaka 2009 akilalamika kwaba fedha ambazo zilitolewa kwa ajili ya kulipa madai ya walimu zilikuwa Sh32 bilioni, lakini hazikutumika zote na badala yake zilipindishwa na kulipwa tofauti na madai halisi ya walimu. Alifafanua kuwa Sh18 bilioni zilizotakiwa kutolewa kwa ajili ya malipo ya walimu wa sekondari, hazikutolewa kabisa.Kutokana na hali hiyo, uvumilivu wa walimu walio chini ya katibu mkuu umekwisha," alisema wakati akisisitiza walimu kuchukua hatua ya kugoma. Alielezea madai ya wakati huo 2009 kuwa licha ya baadhi ya walimu kulipwa na kupewa barua za kupandishwa madaraja, kulipwa malimbikizo ya mishahara na madeni mengine, mpango huo kwa walimu wa sekondari haukwenda vizuri kutokana na mishahara mingi kuwa haijarekebishwa na malimbikizo yake bado yalikuwa hayajalipwa.
CWT na serikali
Tamko la kusudio la walimu kuchukua hatua dhidi ya kutolipwa haki zao na Serikali limekuja baada ya kuwepo kwa kimya cha muda mrefu kuhusu madai yao hayo tangu mwishoni mwa mwaka 2009.Tishio la kuwemo mgomo mkubwa wa walimu lilitolewa maraya mwisho Novemba 2009, mwaka ambao uligubikwa na vita ya maneno baina ya CWT na serikali, huku kukiwa na matishio mengi ya walimu kugoma. Kadhalika Oktoba 2008 kulikuwa na tishio la walimu kugoma kutokana na kuwepo kwa matatizo ya muda mrefu ya walimu, lakini mgomo huo ulizimwa na taarifa ya aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Jumanne Maghembe ambaye alieleza jinsi Serikali ilivyokuwa ikishughulikia matatizo hayo.
Mwananchi