Walimu Wapya Waandamana Manispaa Arusha; Polisi Wawazingira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu Wapya Waandamana Manispaa Arusha; Polisi Wawazingira

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MsandoAlberto, Feb 1, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Walimu wapya leo hii wameandamana hadi ofisi za Manispaa Arusha kudai malipo yao. Taarifa zilizopo ni kwamba malipo hayo yamechelewa kulipwa kwa sababu Serikali kuu haina fedha hivyo ikaiomba Halmashauri ya Manispaa Arusha iwalipe. Kutokana na Halmashauri ya Manispaa kutokuwa na fedha ikaamua kuwalipa nusu ya malipo yao jambo ambalo walimu hao wamelipinga.

  Huu ni uzembe na unyanyasaji. Hizi kelele za serikali kukuza elimu ni siasa. Huwezi ukawa na matokeo mabaya ya mitihani halafu bado unaendelea kunyanyasa walimu!

  Malipo ya Dowans ni haki kulipwa haraka lakini ya walimu masikini ambao wanajitolea jasho na damu kufundisha watoto masikini wa kitanzania hawana haki ya kulipwa mapema!

  Wanakula nini? Wanalala wapi walimu hawa? Wanafikaje kwenye vituo vyao vya kazi?

  Haya sio mambo ya kuvumiliwa hata kidogo. Walimu wasiachwe pekee yao kama yatima! Wanaharakati wawasimamie haki zao, vyama vya siasa viwapiganie!
   
 2. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mh.Diwani, serikali hii ya kishikijali wanayopeana kiawara awara ni vigumu wao kuona na kutambua matatizo yanayoukabili sekta nzima ya elimu.Ifike mahala sasa watz tuige ya Tunisia na Misri tuingie mitaani mpaka kieleweke.
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Mishara ya Ma DC vp huwa inachelewa pia,
   
 4. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Wameajiriwa kwa shinikizo. Hela zitatoka wapi wakati wanakwiba kila kitu? Na bado.
   
 5. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  acha tu hata sisi huku shinyanga manispaa hatujalipwa eti hela hazijatoka hazina na eti halmashauri haina fungu tumeahidiwa kesho na sisi kesho tusipopewa kesho hela zote mtaskia tu bifu aisee tunaishi kwa shida kwa wasamaria wema na hatujaanza kufundisha wakat shule hazina walimu hadi tulipwe kama hawana hela walituajiri ya nini? Na kutuwaisha vituon wengine tunatoka mbali jaman wanaharakati tusaidieni coz CWT hawana msaada tunaombeen plz coz tunaadhirika na tuko ktk nchi yetu
   
 6. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndo ghrama ya kuchakachua kura na kufanya mikutano ya kampeni kama sherehe za kufuru za wafalme. Na ile sheria ya gharama za uchaguzi vipi..... haitekelezeki au ilikuwa CRAAAAAP?
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  mbona land cruiser V8 zinakula mitaa full kiyoyozi mpka jumamosi na jumapili?

  hizo hela wanatoa wapi washindwe za kulipa walimu? mshahara wenyewe wa mwalimu laki tatu unafika?:angry:
   
 8. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  inashangaza sana!huu ni upumbavu mkubwa kabisa,si walikuwa wanajua kuwa walipaswa kuajiri watumishi wapya,sasa kwa nini hawakutenga fedha kuwezesha hili?serikali kuu haina fedha,mbona wamenunua ma V8,mbona wanaharakisha malipo ya dowans?hivi hivyo ndo vipaumbele vya taifa hili!Safari za nje kila kukicha halafu...aaargh!
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  CCM wameiharibu Tanzania beyond weird imaginations! Sijawahi ona Serikali dhaifu, katili, kipofu kama hii ya Kikwete. Ole wao wanaodhani ni suala la udini! Walimu ni watumishi wa umma, mazingira yao ya kazi si mazuri na wengi wao vipato ni vidogo sana....sasa Serikali (maana ya Hazina) waseme hela za walipa kodi ziko wapi mpaka kadhia hii ya walimu tuisikie huku.

  Ni wazi si salama kusubiri hadi 2015, hapa katikati lazima kieleweke na kuwepo mabadiliko ya uongozi Tz.
   
 10. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 632
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  tatizo la walimu ni kuwa hapa mnapiga kelele ila mlisaidia sana kwenye uchakachuaji wa kura. Na kama hamkushiriki 2015 watawahonga msaidie kuchakachua tena. VUMILIENI TU!
   
 11. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ndio maana matokeo ya F4 Zero inaongaza kwa wingi; kama mwalimu hana hela ya kula, hana uhakika na mahali pa kulala
  anawezaje kuconcetrate kwenye kufundisha ukizingatia kwa utaratibu wa Serikali mtu huyo hajaingia kwenye payroll kwa sababu ni ajira mpya
  na hata pata mshara mpaka baada ya miezi 3-4.
  Sina uhakika kama walimu wanaposho yoyote. Tukishirikiana pamoja tunaweza kuifanya Tanzania kuwa nchi yetu.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Walimu nao ni wanaharakati mkuu, sema tu viongozi wao wanawatosa
   
Loading...