Walimu wanawake CWT Kiteto walilia nafasi za uongozi

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Walimu wanawake CWT Kiteto walilia nafasi za uongozi

Na, MOHAMED HAMAD-KITETO.

Mkakati wa kuongeza idadi ya wanawake kushika nafasi za uongozi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, umeanza kutekelezwa na Chama cha Walimu Kiteto (CWT) kitengo cha wanawake.

Wawakilishi wa Chama Cha Walimu Kiteto wako 105, kati yao wanawake ni 21, walimu wakuu ni 87 wanawake 9, wakuu wa shule Sekondari 17 wanawake 3, Maafisa elimu Kata 23 wanawake 5.

Mwenyekiti wa kitengo cha wanawake (CWT) Kiteto, Agnes Lyatuu akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto alisema moja ya sababu ya uchache huo ni walimu wanawake kutojua maadili sheria na haki mbalimbali za walimu wanawake.

Kutojua sheria ya ndoa na mirathi, Afya na magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa akina mama, maadili ya viongozi na misingi ya uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi.

Katiba ya Chama cha walimu toleo la sita ya mwaka 2014, inatambua uwepo wa Idara ya jinsia na walimu wanawake mahali pakazi ambayo inaongoza kufanya mambo yanayowahusu.

Akizungumza na walimu wanawake wa (CWT) Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magesa alisema, kati ya Walimu 1054 walimu 38 ndio viongozi walimu wanawake sawa na 3% hali ambayo alisema hata yeye anatakiwa kuwa upande wa walimu wanawake kuwasemea.

“Kwa hili mimi niseme tu nitawaunga mkono upande wenu, sitokuwa mwanamke ila nitawaunga mkono tu..ili tuweze kusukuma gurudumu hili, kuna baadhi ya wanawake wa mfano hapa ila hawana sauti kutokaa na uchache wao sasa waungwe mkono na wanawake wenzao”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema idadi ya walimu viongozi wanawake inatakiwa kuongezeka kutokana na changamoto za ubakaji watoto zilizopo, hivyo jitihada za kuongeza wigo wa uongozi ziongezeke ili kukabiliana na vitendo hivyo.

Kwa upande wa waalimu wanawake ambao ni viongozi walisema watahakikisha idadi ya walimu kuwa viongozi inaongezeka kwa kuwahamasi waweze kuomba nafasi za kugombea na hata uteuzi.

Mwisho.
 
Back
Top Bottom