Walimu wanavyoibiwa na CWT & PSPF

Kwani ni lazima kisheria kujiunga na CWT?
 
Kumbe wewe ni mwalimu? Si ulisema unaishi Kenya?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
Kwani kuishi Kenya ndio sababu ya kuacha kuzungumzia unyonyaji unaofanywa sehemu nyingine?
kwani ukizungumzia changamoto na unyonyaji dhidi ya waalimu ni lazima uwe mwalimu?
 
Kwani kuishi Kenya ndio sababu ya kuacha kuzungumzia unyonyaji unaofanywa sehemu nyingine?
kwani ukizungumzia changamoto na unyonyaji dhidi ya waalimu ni lazima uwe mwalimu?
Mkuu umeona akili za ccm zilivyo pumba,yaani FaizaFoxy anaishi kwa kukariri mnooo,
mtu kuzungumzia ufisadi kwenye sekta fulani basi lazima na wewe uwe muhusika,

Ritz nae ndio zeroooooo kabisa kichwani
 
Mkuu umeona akili za ccm zilivyo pumba,yaani FaizaFoxy anaishi kwa kukariri mnooo,
mtu kuzungumzia ufisadi kwenye sekta fulani basi lazima na wewe uwe muhusika,

Ritz nae ndio zeroooooo kabisa kichwani

Amma post namba moja hujaisoma vizuri amma huelewi unachokisoma.

Rudia kusoma post namba moja, para ya pili, sentensi ya kwanza.

Kisha njoo ueleze ulichokielewa.
 
Walimu wa Tanzania sio wa kuonea huruma....kwanza ni wajinga sanaaa ....hawajui kudai haki zao.....
 
Walimu wenyew hawajitambui,wanapaswa kuungana na kujadil hlo suala bt wao kila cku ni kulia lia kuhuxu ugumu wa maisha
 

Matatizo ya waalimu yanaanzia kwenye ngazi ya chini kabisa mashuleni, walimu wakuu na wakuu wa shule wamegeuka miungu watu na kwa utawala huu nihatari zaidi kwa mwalimu kwani mkuu wa shule anaweza kumuandikia taarifa mbaya kwa Afisa Elimu ikawa kesi na matatizo makubwa.

Maafisa elimu wengi ni vilaza na wanawaogopa sana walimu wanaojielewa hivyo ukionekana unaleta ujuaji wa kila siku utatengenezewa kesi zisizoisha kila siku na faili litaharibika, wakati huo DED na DC hawatakutetea hata kidogo utabigwa ban la nguvu ukitoa mguu kituo cha kazi taarifa ilishafika hadi kwa waziri mkuu kuwa kuna mwalimu ameenda sokoni bila kuaga, na mshahara utafungwa muda huohuo.

Waalimu ndio wanaocheleweshewa hata kupanda madaraja ya mishahara na wengine wanakuwa nyuma hata kama ulianza mwaka mmoja na wengine utajikuta daraja lako liko nyuma na ukienda kwa afisa utumishi utaambulia matusi na kejeli zakijinga sana, utaonekana kama hukustahili hata kuitwa mwalimu kwani walimu wenzio wanamatatizo kama yako na wametulia ila wewe unaleta kimbelembele. Walimu wengi ni WANAFIKI wakubwa sana, kupikiana majungu kwa wakuu wa shule na maafisa elimu na wakurugenzi. utakuta mwalimu hampendi mwenzie kisa anapiga sana ngeli kuliko yeye. sasa huyu atakubali kuweka kunji la pamoja???

TAHOSSA ndio liumoja lingine lakijinga sanab katika kada ya ualimu. mm niliwahi kuwauliza hivi nyinyi tahossa mnashindwa kuwa na hata stationary yakuchapa na kutoa kopi mitihani yenu wenyewe kila siku mnapeleka tenda kwa watu binafsi, nikaja kustuka zile stationaries nizao wenyewe. TAHOSSA wakikutana wanaongelea walimu wakorofi katika mashule yao na jinsi yakuwadhibiti na wanapeleka mapendekezo kwa maafisa elimu kuwa umetuletea walimu wajorofi sana, mwalimu anakuwa yupo chini ya uangalizi wamajungu na fitna bila kujua. basi ni kero kila kukicha.

Mimi niliacha ualimu baada yakuvimbiana na kiafisa elimu kimoja hivi huko maporini nikamwambia kwaheri, hakuamini nikarudi nikafunga virago vyangu safari hadi kesho huu i mwaka wa 5 sasa. walimu msiwe wanyonge hao jamaa wanaowaendesha mkipata nafasi mnakunja ngumi, unamtoa meno 3 alafu unatafuta laki 5 za kesi.

Kuna kichama kingine chakipumbavu sana kinaitwa TSD, yaaaaaaani duuuuuuuuu walimu ni SHIIIIIIIIIIIIIIDA, ukiwaona hawa TSD ni vibabu flani vikoloni kishenzi yaani vimekaa pale kusubiri mwalimu ateleze apewe barua za nidhamu sijui ujinga gani, hawa wote ni wakoloni wanao waandama walimu na walimu hawana pakutokea masikini ya MUNGU. wamekuwa wanyonge sana, mara mkuu washule, akigeuka huku anakuta cwt, hajakaa sawa MEK, hajapinduka upande mwingine tsd, huku kuna madiwani nao wanawaandama walimu hatari. WALIMU SIO KAZI, UKITAKA UMASIKINI JIINGIZE HUKO
 
Dili kwako wewe si ndiyo kila kitu Kenya mara nipo Mombasa kwa mume wangu mara nipo Nairobi wakwe zangu yaani ueleweki.
Karibu kenya mkuu ,hapa ndio kimbilio la dada zenu wa rombo
 
[QUOTi, post: 15555850, member: 269031"]Cwt ni genge la wahuni wanaokula kiulaini kupitia shida za walimu,mara 100 wangekua wanatatua shida za walimu,cwt ndani ya mwaka mzma ndani ya wilaya 1 hutatua shida ya mwalimu 1 au wawl;wanatatua matatzo kwa sampling;hela wanayochota ni kubwa kulinganisha na huduma anayopata mwl toka kwao;walimu tupambane kuanzisha vyama vya kututetea viwe vingi,Inawezekana Tukishikama..[/QUOTE]
kweli umesema.mimi mwenyewe ni mwl sasa ni mwaka wakumi nababuliwa nahawa jamaa.cwt nizaidi ya bomu la atomic.chama hiki sio cha hiari nikulazimishana tu
 
Mkuu dangadunguri hao maafisa elimu wengi wala hawana hata ngazi ya degree,pia wakijua wewe ni ukawa watakuandama sana
 
Mkuu dangadunguri hao maafisa elimu wengi wala hawana hata ngazi ya degree,pia wakijua wewe ni ukawa watakuandama sana

Kaka ni hatari sana, Afisa Elimu anakasirika akiona walimu wamejaa kwenye ofisi yake utafikiri nyumbani kwake. Sisi wakati tunaripoti walitukagua wakagundua kuwa walimu wenye shahada tulikuwa wengi kuliko wenye stashahada, walisikika wanasema mwaka huu kazi tunayo. kumbe wao walitaka kuzipiga pesa zetu za kujikimu na garama za usafiri. na vichwa vingi pale vilitoka huu ukanda wa pwani maneno kama chiriku na wengi walitoka vyuo vilivyozoea vurugu na makunji. Jamaa ili kutupunguza nguvu wakatupangia vituo harakaharaka.

Tugawana namba za simu tukawa tunawasiliana ni siku gani yakukutana kwa afsa elimu atoe pesa zetu. ilichukua wiki 2 kila siku tunapanda kwenda kwake na kumbuka kuna wengine walipangiwa vituo 120km kutoka halmashauri, wao walichukua vyumba gest ikawa hakuliki wala hakukaliki.

Tukazama kuzitafuta namba za waziri mkuu, tukamtwangia tukampa makavu kila kitu kuhusu pesa zetu, hadi kufika saa nane list ya walimu wote tunaaodai na pesa zetu ilikuwa tayari, watu waliondoka na 1.5m na wengine 2m. Jamaa anagawa hundi amevimba kama kifutu. tukabeba mpunga wetu tukatambaa.

Hatari zaidi ya kada hii walimu wanaoajiriwa sasa ni vitoto kabisa yani havijitambui wakifika site ni mademu na ulabu. na vyuo wanavyotoka ndio shida kabisa hakuna kugoma wala kusononeka, hajui hata aanzie wapi hata kupiga mbinja/minja hajui.
 
Nafikiri wanaweza kuamua na kuwa na chama vya kikanda au mkoa kinachotakiwa ni idadi ya wanachama kwa ajili ya kuanzisha chama kingine. Haya aamkeni kuanzia huko mikoani mvunje hili genge la wahuni!
 
Nasikia tanzania teachers association wameamua kufikishia magufuli
 
Ualimu ni wito jamani

Hayo mengine ni kama anasa tu
 
Kichwa cha Habari hakiendani na maudhui ya Habari yako,

Hukusema ni kwa jinsi gani PSPF inawanyonya walimu,

Aidha, kujiunga na Chama cha wafanyakazi sio lazma, ni hiyari, unaweza kuomba kujitoa na utatolewa.
 
walimu wakiacha majungu nakuchukiana wao kwa wao itasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…