Walimu walipwe kama maofisa wa BoT na TRA, tatizo la walimu litakoma mara moja!

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Wengi wanakimbilia ajira BOT na TRA. Wengine TAKUKURU na JWTZ, kinachowapeleka kwa wingi ni mishahara minono.

Leo taifa linakabiliwa na uchache wa walimu hasa wa masomo ya Hisabati na Sayansi. Najiuliza kama kuna nia ya dhati ya kumaliza tatizo hili, maana tiba yake ni rahisi kuongeza mishahara iwe kama ya taasisi nilizozitaja hapo juu.
 
Haitawezekana mkuu. Nchi haiwezi kupata fedha za kutosha kuwalipa walimu mishahara kama ya taasisi ulizotaja kwani wao (WALIMU) ni wengi sana ukilinganisha na idadi ya watumishi wengine wa umma. Hata hivyo serikali inaweza kuboresha mapato yao ya mshahara kwa kurudisha ile asilimia 50 (Posho ya kufundisha) iliyokuwa inatolewa zamani na kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwamo kuwajengea nyumba za kuishi shuleni au kuwapa posho ya pango, kuwapa usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kwenda na kurudi kazini, kuwalipa stahili zao kwa wakati NK.
 
hivi walimu ni wachache kuliko bot na tra??

tra sizan kama ina staffs 4000 nchi nzima na bot sizan kama ina staff 3000 nchi nzima..

ila walimu nina imani wapo zaidi ya elfu hamsini ( 50,000) nchi nzima
 
Haitawezekana mkuu. Nchi haiwezi kupata fedha za kutosha kuwalipa walimu mishahara kama ya taasisi ulizotaja kwani wao (WALIMU) ni wengi sana ukilinganisha na idadi ya watumishi wengine wa umma. Hata hivyo serikali inaweza kuboresha mapato yao ya mshahara kwa kurudisha ile asilimia 50 (Posho ya kufundisha) iliyokuwa inatolewa zamani na kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwamo kuwajengea nyumba za kuishi shuleni au kuwapa posho ya pango, kuwapa usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kwenda na kurudi kazini, kuwalipa stahili zao kwa wakati NK.
Japan walimu wanalipwa vizuri kuliko kada nyingine zote, kwa nn Tanzania isiwezekane. Sema nchi yetu haijatoa kipaumbele kwenye elimu
 
akiwa anaongea siku ya wafanyakazi tarehe 1 mei mwaka huu Magufuli alisema kwa idadi ya watumishi hewa iliyokuwepo na pesa iliyokuwa wakilipwa, ikigawiwa kwa wafanyakazi waliopo kila mfanyakazi atapata mshahara ambao ni kuanzia 1 million na kuendelea.

kama mtumishi wa umma nilimwelewa sana!
nasubiri julai 23 nione kama na yeye ni walewale au sio.
 
wangekua walimu wanafundisha ningesapoti but walimu wa bongo ni chenga hata class hawaonekani ,,itakua vizuri mishahara ikakatwa tu ipungue zaidi..
 
Ungeanza kuwataka walimu wasome sana kama wenzao wa BOT na TRA ningekuelewa. Enzi zangu nasoma wale jamaa waliofeli peke yao ndio walienda kwenye ualimu. Yaani division three zisizo na combination pamoja na division four. Wale tuliopata one na two tulisonga mbele. Sasa ikitokea hawa failures wakalipwa kuliko wale waliofaulu nani atabuni mipango ya kuipatia nchi mapato kama tunaamua kuwapa kipaumbele hao?
 
Haitawezekana mkuu. Nchi haiwezi kupata fedha za kutosha kuwalipa walimu mishahara kama ya taasisi ulizotaja kwani wao (WALIMU) ni wengi sana ukilinganisha na idadi ya watumishi wengine wa umma. Hata hivyo serikali inaweza kuboresha mapato yao ya mshahara kwa kurudisha ile asilimia 50 (Posho ya kufundisha) iliyokuwa inatolewa zamani na kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwamo kuwajengea nyumba za kuishi shuleni au kuwapa posho ya pango, kuwapa usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kwenda na kurudi kazini, kuwalipa stahili zao kwa wakati NK.
kuhusu pikipiki huwatakii mema walimu
 
Ungeanza kuwataka walimu wasome sana kama wenzao wa BOT na TRA ningekuelewa. Enzi zangu nasoma wale jamaa waliofeli peke yao ndio walienda kwenye ualimu. Yaani division three zisizo na combination pamoja na division four. Wale tuliopata one na two tulisonga mbele. Sasa ikitokea hawa failures wakalipwa kuliko wale waliofaulu nani atabuni mipango ya kuipatia nchi mapato kama tunaamua kuwapa kipaumbele hao?
ULIFUNDISHWA NA FAILURES UKAPATA DIVISION ONE ! HILI NALO NI MAAJABU YA DUNIA.
 
Tafadhali msipoteze nguvu na muda kutupigania walimu.
Walimu tunajipigania wenyewe na tumelianza hili siku nyingi.

Aluta continua.
Tutaeleweka tu.
 
Wengi wanakimbilia ajira BOT na TRA. Wengine TAKUKURU na JWTZ, kinachowapeleka kwa wingi ni mishahara minono.

Leo taifa linakabiliwa na uchache wa walimu hasa wa masomo ya Hisabati na Sayansi. Najiuliza kama kuna nia ya dhati ya kumaliza tatizo hili, maana tiba yake ni rahisi kuongeza mishahara iwe kama ya taasisi nilizozitaja hapo juu.
Kun kazi zingine kutokana na mazingira yake ukiongeza tu mshahara watu wataacha hio kazi baada ya mwaka au miaka miwili , wataenda kufanya biashaa zao .. Kama ualimu na uaskari...
Kaka hujasoma economics ee?
 
Ungeanza kuwataka walimu wasome sana kama wenzao wa BOT na TRA ningekuelewa. Enzi zangu nasoma wale jamaa waliofeli peke yao ndio walienda kwenye ualimu. Yaani division three zisizo na combination pamoja na division four. Wale tuliopata one na two tulisonga mbele. Sasa ikitokea hawa failures wakalipwa kuliko wale waliofaulu nani atabuni mipango ya kuipatia nchi mapato kama tunaamua kuwapa kipaumbele hao?
hiyo zamani sana, sasa ivi nimeona one kali sana zinasoma BAED na BED...hii yote sababu ya bodi a.k.a HESLB huku three na two zikienda kusoma hizo course unazosema za waliofaulu.
 
Back
Top Bottom