Walimu waliojiendeleza kwenye TEHAMA

macarina

Senior Member
Jan 24, 2016
143
55
Kuna walimu ambao katika kujiendeleza kielimu wamesomea ujuzi au fani ambazo ni tofauti na ualimu ikiwa ni pamoja na waliosomea IT.
Hapa ninamaanisha kwamba mwalimu aliajiriwa akiwa na elimu ya ualimu ngazi ya chetu au diploma. Mwaka 2005 mwishoni walimu waliambiwa kwa kuwa technolojia inakua haraka watahitajika wataalamu wa IT katika kila sekta hivyo walimu wenye ujuzi huo pia watahitajika kwa wingi.
Wapo walimu ambao walienda vyuoni kusoma IT na wengi zaidi walijiunga masomo hayo katika chuo cha IFM.
Walipohitimu wakarudi katika vituo vyao vya kazi na huko walikabidhiwa kufundisha somo la TEHAMA na kwa wale ambao Shule zao zina computer Labs wakakabidhiwa kumamia na kufanya kazi zote zinazohusiana na IT.
Chakushangaza walipopeleka kwa waajiri vyeti na degree walizopata kwa kusoma kozi hiyo waliambiwa kwamba havitambuliki kwa kuwa kozi waliosomea ni nje ya ualimu.
Na mpaka sasa wakipita maafisa mashuleni wanasisitiza somo la TEHAMA lifundishwe na wale wataalamu wa IT. Na hawajapata nyongeza yoyote kwenye Mishahara na hata viwango vyao vya elimu. Mishahara ya walimu hao bado ni ile ya certificate kwa walioajiriwa wakiwa na certificate na Mishahara ya diploma kwa walioajiriwa wakiwa na diploma.
Je. Huu siyo wizi unaofanywa na serikali dhidi ya walimu hao?
Na je. Walimu hao wanafanya kazi kwa moyo mkunjufu huku wakijua kuwa ujuzi wao wanautumia kwa kutoa sadaka ya kulazimishwa?
Kuna mmoja alijaribu kufuatilia ili abadilishwe na kupelekwa kitengo cha IT mahali pengine. Alipomuona Afisa utumishi wa will ya yao amuelekeze cha kufanya alimjibu "sina cha kukusaidia zaidi ya kukuambia nenda kakae na shida yako"
Je. Ni vema tuendelee na utaratibu huu? Na kama tu naendelea nao. Je. Serikali itawasaidiaje walimu hao?
Kama hawatasaidiwa je. Rais wetu atakubali walimu hao wakikataa kufanya kazi hizo ambazo wamekuwa wanafanya kwa kuibiwa ujuzi bila malipo?

Naomba mawazo yenu zaidi wadau. Maana hili linanigusa maana mmoja wa wahanga hao ni mdogo wangu. Na ndo amekuwa anapika mrejesho toka kwa walimu wenzake aliosoma nao IFM.
 
Da pole, labda atafute halmashauri yenye hitaji la elim yake ahamie huko na abadili na ajira
 
hilo suala litakuwa linakuhusu wewe, kwanza serikali haionei mtu bali inafata kanuni na sheria za ajira, cha kukushauri rudi chuoni kafanye PDDE ni mwaka mmoja then rudi kituoni kwako na daraja utapandishwa wakikuzingua rudi hapa jukwaani kwa hatua zaidi
 
In reality kujiendeleza ktk Kazi inatakiwa uwe mahili kwenye kuzielewa taratibu za Kazi yako na sheria ndogo ndogo. Ukisema hivyo kuna MTU ataenda kusoma sociology halafu atarudi na kuleta kauli za hii fani hats shuleni inahitajika. Ujanja ulikuwa ungesoma education na teaching subject ingekuwa IT na hesabu au na somo jingine ila usome bachelor ya IT laah hiko cheti pamba sebuleni. Ila chukua wazo la PGDE fasta kabla hawajabadili mtazamo maana hii nchi ni kama unga wa ngano Mara andazi mara mkate heeeee!!! chapati hamad skonzo yalaah kababu. Haieleweki in short wanaweza kisema hawajui PGDE ndo nn
 
G'HOMELE. Uzi haujauliza utaje unamuhusu nani. Changia kulingana na kilichotelezwa. Ila nashukuru kwa kuwa mmoja wa wachangiaji.
 
Back
Top Bottom