Ushauri kwa wanaotarajia kuanza kusoma program za Ualimu 2024

kekule benzene

JF-Expert Member
Sep 28, 2016
1,363
3,337
Leo 13/07/2024 matokeo ya kidato cha sita yametoka na ufaulu ni 99.43%

Nawapongeza waliofaulu, lakini pia nawaasa kuwa makini sana katika kuchagua program za kusoma, maana matokeo mazuri ya kidato Cha nne na sita hayatokuwa na maana sana endapo ukifeli kuchagua program ya kusoma chuo.

Kwa upande wangu leo napenda kuwashauri wanaofikiria kwenda kusomea ualimu.

Kwa mazingira ya sasa yalivyo ni vema kutochagua program ya ualimu, ni heri uchague program nyinginezo kwa sababu

1. Watu walikuwa wanachagua ualimu kwa ajili ya kupata mkopo kwa urahisi ila kwa sasa unaweza ukachaguliwa ualimu na mkopo ukakosa vizuri tu.

2. Watu walikuwa wanasoma ualimu kwa ajili ya kupata ajira kwa urahisi ila kwa sasa walimu wamejaa mtaani hawana ajira wanaishia kujitolea huku wakilipwa posho ya 50k hadi 200k kwa mwezi (degree holder?)

NB: hata serikali ikiajiri kila mwaka, haina uwezo wa kuajiri walimu wa degree wote wa UDOM na DUCE ( UDOM pekee Ina uwezo wa kutoa walimu wa degree zaidi ya 3500 kwa mwaka), na kumbuka takribani ya nusu ya vyuo Vikuu vya Tanzania vinatoa program ya ualimu.

3. Mshahara duni na mazingira duni ya walimu
Haihitaji maelekezo mengi، ualimu ndio kazi isiyokuwa na allowance yoyote na mshahara unakuta ni 750k gross kwa anayeanza kazi (degree) huku take home ikiwa ni kwenye 500k kwa mtu mwenye mkopo HESLB

Pia ukiwa mwalimu unajihakikishia kufanya kazi vijijini (interior) ambapo sometimes hata huduma za msingi ni shida

4. Watu walikuwa wanasoma ualimu kwa sababu ya ufaulu mdogo (japo si sahihi 100%)
  • kwa sasa Kuna watu wengi ambao wanapata division one na two wanaenda kusoma education hali ya kuwa wangeweza kusoma program nyinginezo
  • cutting point za education na program nyinginezo karibu zote (isipokuwa chache)

5. Pia ni kazi ambayo hadi wasiosoma wanakudharau, unaweza kukuta hadi diwani/mwenyekiti wa kijiji ambaye ni std 7 failure anawafokea walimu, ila huwezi kukuta anaenda kuwafokea madaktari, manesi nk

Pia mwalimu ana maboss 20 kidogo

SWALI
KWA NINI UCHAGUE KOZI AMBAYO AJIRA SHIDA, MSHAHARA MDOGO, MAZINGIRA YA KAZI MAGUMU, ?

Kwa kuwa program zote zina Shida ya ajira ni bora uchague program ambayo ukipambana na kufanikiwa kupata ajira angalau unapata ahueni ya kimaisha.

Ndugu zangu wa CBG na PCB ambao mnategemea kwenda kusoma education kwa masomo ya Chemistry na biology au chemistry na geography msijidanganye kuwa mnaenda kusoma sayansi hivyo ajira zipo nyingi, hao watu wa CB na BG wapo kibao mtaani na hawana hata matumaIni

Mnaotegemea kusoma arts😂😂 mwaka Jana kwenye maombi ya ualimu wa degree baadhi ya masomo hayakuwekwa kabisa

MWISHO
Ukweli wa mambo, ajira ni changamoto kwa kila program hivyo

1. Jitahidi kuchagua program ambayo unaweza kujiajiri baada ya kumaliza chuo

2. Usilazimishe kusoma degree, mfano umesoma CBG badala ya kuforce kusoma degree programs zisizoeleweka, bora ukasome program ya afya, nk

3. Usichague program usiyoifahamu au usiyoipenda ili ujaze machaguo matano, itakukost.

4. Usijifanye ujuaji, waulize waliomaliza vyuo Wana mengi sana ya kuwashauri.

Mjumbe hauwawi

WALIMU WENZANGU NAOMBA MNISAMEHE

Pia soma
 
Kifupi waombaji nenda kaangal8e digrii ngumu zenye watu wachache vyuoni za sayansi angalia miaka may be mitatu iliyopita degree gani ngumu enrolment ni ya watu wachache

Sio unaomba sijui business administration, sijui law nk angalia degree ipi wanafunzi wengi wanaitoroka sababu ya ugumu nenda huko

Hizo degree za mdebwebo kila toto la Mama Bishoo linakimbilia huko

Vinginevyo ujiandae kusoma masters hadi PhD na kuwa registered as a proffesinal ili kutoboa kiajira ukichagua degree rahisi Kimbilio la kila toto la Mama lipenda mdebwedo digrii rahisi
 
Ualimu Kwa hapa Tanzania ni hovyo Sana,kwasasa kupata ajira tu ni majanga,ukisoma ualimu uwe mjanja janja uombe programm mbalimbali nje ta nchi ukapambane na changamoto zingine.
 
Madogo Mliosoma comb za Art nendeni mkasome kozi za ustawi wa jamii na Maendeleo, msitishwe kuwa ajira hamna, hapana ajira zipo.

watu wanastaafu, wanaacha kazi, wanafukuzwa, wanakufa na wanaacha nafasi wazi.

Mwigulu Nchemba hatakama akiingiza ukoo wake mzima kwenye nafasi za utumishi hawezi kumaliza nafasi zote. Na sio kwamba kila ndugu yake atakuwa na qualification ya kukaa kwenye nafasi hiyo, kunawengine watakuwa wanawaza biashara.

na unatakiwa kujua Mwigulu Nchemba hiyo nafasi hatakaa milele hata ww unaweza kukaa.

Ajira zipo madogo, achaneni na ualimu mi huwa naiita course ya kimaskini
 
Kifupi waombaji nenda kaangal8e digrii ngumu zenye watu wachache vyuoni za sayansi angalia miaka may be mitatu iliyopita degree gani ngumu enrolment ni ya watu wachache

Sio unaomba sijui business administration, sijui law nk angalia degree ipi wanafunzi wengi wanaitoroka sababu ya ugumu nenda huko

Hizo degree za mdebwebo kila toto la Mama Bishoo linakimbilia huko

Vinginevyo ujiandae kusoma masters hadi PhD na kuwa registered as a proffesinal ili kutoboa kiajira ukichagua degree rahisi Kimbilio la kila toto la Mama lipenda mdebwedo digrii rahisi
Hakuna sifa ya kusoma vitu vigumu. Zipo course ngumu mtu anasoma halafu mwisho wa siku anasanda tu mtaani.
 
Sahihi kabisa,
Mfano Kuna nina radiki yangu kasoma UDOM (MD) miaka 5 +1 intern

Mume wake kasoma UDOM (BCOM) miaka 3

Mume wake kaajiriwa sehemu ambayo mshahara wake (+ allowance) ni zaidi ya mara 3 ya mke wake ambaye amesoma kozi ngumu na kwa muda mrefu
 
Leo 13/07/2024 matokeo ya kidato cha sita yametoka na ufaulu ni 99.43%

Nawapongeza waliofaulu, lakini pia nawaasa kuwa makini sana katika kuchagua program za kusoma, maana matokeo mazuri ya kidato Cha nne na sita hayatokuwa na maana sana endapo ukifeli kuchagua program ya kusoma chuo.

Kwa upande wangu leo napenda kuwashauri wanaofikiria kwenda kusomea ualimu.

Kwa mazingira ya sasa yalivyo ni vema kutochagua program ya ualimu, ni heri uchague program nyinginezo kwa sababu

1. Watu walikuwa wanachagua ualimu kwa ajili ya kupata mkopo kwa urahisi ila kwa sasa unaweza ukachaguliwa ualimu na mkopo ukakosa vizuri tu.

2. Watu walikuwa wanasoma ualimu kwa ajili ya kupata ajira kwa urahisi ila kwa sasa walimu wamejaa mtaani hawana ajira wanaishia kujitolea huku wakilipwa posho ya 50k hadi 200k kwa mwezi (degree holder?)

NB : hata serikali ikiajiri kila mwaka, haina uwezo wa kuajiri walimu wa degree wote wa UDOM na DUCE ( UDOM pekee Ina uwezo wa kutoa walimu wa degree zaidi ya 3500 kwa mwaka), na kumbuka takribani ya nusu ya vyuo Vikuu vya Tanzania vinatoa program ya ualimu.

3. Mshahara duni na mazingira duni ya walimu
Haihitaji maelekezo mengi، ualimu ndio kazi isiyokuwa na allowance yoyote na mshahara unakuta ni 750k gross kwa anayeanza kazi (degree) huku take home ikiwa ni kwenye 500k kwa mtu mwenye mkopo HESLB

Pia ukiwa mwalimu unajihakikishia kufanya kazi vijijini (interior) ambapo sometimes hata huduma za msingi ni shida

4. Watu walikuwa wanasoma ualimu kwa sababu ya ufaulu mdogo (japo si sahihi 100%)

  • kwa sasa Kuna watu wengi ambao wanapata division one na two wanaenda kusoma education hali ya kuwa wangeweza kusoma program nyinginezo
  • cutting point za education na program nyinginezo karibu zote (isipokuwa chache)

5. Pia ni kazi ambayo hadi wasiosoma wanakudharau, unaweza kukuta hadi diwani/mwenyekiti wa kijiji ambaye ni std 7 failure anawafokea walimu, ila huwezi kukuta anaenda kuwafokea madaktari, manesi nk

Pia mwalimu ana maboss 20 kidogo

SWALI
KWA NINI UCHAGUE KOZI AMBAYO AJIRA SHIDA , MSHAHARA MDOGO, MAZINGIRA YA KAZI MAGUMU, ?

Kwa kuwa program zote zina Shida ya ajira ni bora uchague program ambayo ukipambana na kufanikiwa kupata ajira angalau unapata ahueni ya kimaisha.

Ndugu zangu wa CBG na PCB ambao mnategemea kwenda kusoma education kwa masomo ya Chemistry na biology au chemistry na geography msijidanganye kuwa mnaenda kusoma sayansi hivyo ajira zipo nyingi, hao watu wa CB na BG wapo kibao mtaani na hawana hata matumaIni

Mnaotegemea kusoma arts😂😂 mwaka Jana kwenye maombi ya ualimu wa degree baadhi ya masomo hayakuwekwa kabisa

MWISHO
Ukweli wa mambo, ajira ni changamoto kwa kila program hivyo

1. Jitahidi kuchagua program ambayo unaweza kujiajiri baada ya kumaliza chuo

2. Usilazimishe kusoma degree, mfano umesoma CBG badala ya kuforce kusoma degree programs zisizoeleweka, bora ukasome program ya afya, nk

3. Usichague program usiyoifahamu au usiyoipenda ili ujaze machaguo matano, itakukost.

4. Usijifanye ujuaji, waulize waliomaliza vyuo Wana mengi sana ya kuwashauri.

Mjumbe hauwawi

WALIMU WENZANGU NAOMBA MNISAMEHE
Upande wangu bora VETA kuliko Ualimu...Mafundi wa Mitambo kama Grader, Excavator na mitambo yabdizain iyo ina uhitaji sana wa mafundi hasa mafund umeme wa iyo mitambo vijana kasomeeni iyo kuliko ualimu ambao hata ukipata ajira mazingira n magumi mno
 
Madogo Mliosoma comb za Art nendeni mkasome kozi za ustawi wa jamii na Maendeleo, msitishwe kuwa ajira hamna, hapana ajira zipo.

watu wanastaafu, wanaacha kazi, wanafukuzwa, wanakufa na wanaacha nafasi wazi.

Mwigulu Nchemba hatakama akiingiza ukoo wake mzima kwenye nafasi za utumishi hawezi kumaliza nafasi zote. Na sio kwamba kila ndugu yake atakuwa na qualification ya kukaa kwenye nafasi hiyo, kunawengine watakuwa wanawaza biashara.

na unatakiwa kujua Mwigulu Nchemba hiyo nafasi hatakaa milele hata ww unaweza kukaa.

Ajira zipo madogo, achaneni na ualimu mi huwa naiita course ya kimaskini
Umeongea sahihi ila kusema ajira zipo hapo lazima iwekwe maelekezo

Yes, ajira zipo ila za kupambania

Mtu asome awe competent, pia wajue kwa sasa interview ndio habari ya mjini

Huna connection, basi interview inakuhusu, written, oral and practicals
 
Upande wangu bora VETA kuliko Ualimu...Mafundi wa Mitambo kama Grader, Excavator na mitambo yabdizain iyo ina uhitaji sana wa mafundi hasa mafund umeme wa iyo mitambo vijana kasomeeni iyo kuliko ualimu ambao hata ukipata ajira mazingira n magumi mno
Exactly

Sio bora, ni bora mara 10,000😂
 
Sahihi kabisa,
Mfano Kuna nina radiki yangu kasoma UDOM (MD) miaka 5 +1 intern

Mume wake kasoma UDOM (BCOM) miaka 3

Mume wake kaajiriwa sehemu ambayo mshahara wake (+ allowance) ni zaidi ya mara 3 ya mke wake ambaye amesoma kozi ngumu na kwa muda mrefu
Tatizo mara ingine mtu haekewi career path
Ukisoma udaktari lengo sio kuishia MD unatakiwa kusonga mbele kusoma kuwa specialist au kwenda masters sio tu kuishia MD na kwenda kuolewa au kukaa ukisubiri ajira

Au mtu anamaliza degree ya uhasibu anaanza kuzurura kutafuta kazi anatakiwa asome awe certified Accountant sio kuzurura tu na kadigrii kake ohh natafuta ajira vigumu kupata
 
Upande wangu bora VETA kuliko Ualimu...Mafundi wa Mitambo kama Grader, Excavator na mitambo yabdizain iyo ina uhitaji sana wa mafundi hasa mafund umeme wa iyo mitambo vijana kasomeeni iyo kuliko ualimu ambao hata ukipata ajira mazingira n magumi mno
Umeongea ukweli kabisa,japo wazazi wengi wanaona VETA mizinguo kutokana na kuwa na fikra kuwa watoto wao wasome ili waajiriwe, VETA kuna kozi ka za barabara,ufundi AC,ufundi wa majenereta,injini za dizeli n.k....
 
Back
Top Bottom