Walimu Wajipanga Kuvamia Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu Wajipanga Kuvamia Ikulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, May 16, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CHAMA Cha Walimu Tanzania [CWT] kimetishia kuweka kambi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwezi huu, kwa walimu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam endapo hawatapatiwa madai na malimbizo wanayodai kwa muda mrefu.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki kwa walimu kote nchini na wametishia kuweka kambi kwa Kikwete ili kuweza kushinikiza kupatiwa madai yao wanayodai.

  Hatua hiyo ilitangazwa jana na Katibu wa Chama hicho, Bw. Ezekiel Oluoch kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

  Oluoch alisema kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu endapo Serikali kupitia Wizara husika endapo haitaweza kulipa madeni hayo basi watakwenda Ikulu kwa Rais Kikwete ili awatunze hadi hapo watakapopatiwa madai yao.

  Alisema kuwa kwa wale walimu ambao wapo mikoani ametoa agizo kwa walimu hao waende kutia kambi kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya zao hadi hapo watakapolipwa madai yao.

  Mbali na kutangaza kuchukua hatua hiyo chama hicho kimechukua uamuzi wa kuishitaki Serikali kwenye Shirika la Kazi Duniani [ILO], Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

  Pia chama hicho kimeishitaki Serikali kwenye Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Spika wake Samweli Sitta na kwenye Shirikisho la Wafanyakazi [TUCTA] kwa kuwa chama hicho kinaamini taasisi hizo zina uwezo wa kuishinikiza Serikali kulipa madeni hayo kwa wakati.

  Alisema madai ya walimu yamekuwa yakishindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na walianza kudai toka mwaka jana lakini majibu yanayotolewa ni urasimu wa Serikali ndio tatizo.

  Alisema awali walishakutana na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu lakini hakuna ufumbuzi wa uhakika kuhusu madai hayo na kupelekea walimu kuchoshwa na hali hiyo.

  CWT imekuwa kwenye malumbano na mvutano na Serikali kudai madeni yao hadi kufikia hatua ya kugoma nchi nzima, lakini Serikali iliweza kukimbilia Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kuomba kufunga mgomo huo usiendelee.

  “Sasa kwa kuwa walishafunga mgomo huo na walimu wakabaki hawana cha kufanya sasa uamuzi watakaouchukua utakuwa ni muafaka” alisema

  Kutokana na malalamiko hayo ya mara kwa mara ya walimu, baadhi ya walimu hasa wale wa shahada wameamua kuacha kazi na kukimbilia kwenye shule binafsi kwa kuwa huko wanalipwa mishahara kwa wakati.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2007050&&Cat=1
   
 2. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Hao nao wapumzike tu wale chaki, hawana jipya. kila siku wanatishia Nyau tu halafu they dont do the real Thing! Wafanyakazi woote wa Tanzania ni waoga. hawajui kabisa kuwa tawala nyingi dhalimu duniani ziliangushwa na nguvu ya wafanyakazi. Either they go for the real thing or just keep their peace!!
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  May 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  BabaDesi, hili tatizo la walimu, ni tatizo letu sote Watanzania. Raiya wengi wanafikiria kuwa matatizo kama haya ya walimu hayawahusu. Wanashindwa kutambua kuwa huu ni sawa na mtego wa panya, wanaingia waliomo na wasio kuwemo. Elimu ya Watz ikushuka kutokana na walimu kukosa hari na miundo mbinu ya kufundisha, watakao athirika ni watoto wetu.

  Leo hii kule Mkoani Arusha tunaambiwa kuwa 80% ya wanafunzi wa kidato cha tatu hawajui kusoma na kuandika...! Hii si tu inashangaza bari inatia kichefu chefu. Hawa vijana wamebakiza mwaka mmoja tu kumaliza elimu ya sekondari. Je Taifa litegemee tija gani kutoka kwa mabaro baro hawa....!? Au ndio wataishia Melerani?

  Hapa wizara ya Elimu, imechukuwa hatua gani kukabiliana na tatizo hili, au ndio wanaachiwa wakuu wa wilaya na maofisa elimu wa kata!?
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Walimu hawa utawaona mwakani watakavyokuwa bega kwa bega kuichagua CCM chama kilicholewa madaraka na kukumbatia wezi wa mali za umma na kutowajali wananchi wake wanaoendelea kuogelea kwenye dimbwi la umaskini ndani ya nchi yao iliyojaa kila namna ya utajiri. Kama wana uchungu na maovu ya CCM mwakani waiipe kura. Na kwale walioko vijijini wawawelimishe na wananchi wengine.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  May 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tatizo lingine la hao walimu wetu nao wamejaa ubinafsi, wakishapewa fulana , vitenge na pesa kidogo wanasahau wajibu wao...! Wanafikiria kuwa ualimu wao unaishia madarasani tu, wanashindwa kuelewa kuwa ukishakuwa mwalimu basi ujue kuwa wewe ndio kioo cha jamii. Wanatakiwa waonyeshe mfano kwa taifa kuwa wao si watu wa kuchezewa tena.
   
 6. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wewe jamaa umetulia saana , nadhani chaki zinawaathiri woa sijui ni ujinga ? Nadhani ni ujinga maana ujinga ndio hadui yetu mojawapo, kwanza wengi mafukara wakutupwa wakati wao ni waajiliwaliwa wa serikali lakini mmh ! Hawafanyi maendeleo yoyote matokeo yake unakuta anakuwa mlevii, au anatembea na wanafunzi hamna kingine shida ndio zimefanya wawe hivyo.
  Poleni mmefulia hamtoweza kubadilisha mambo!
  Ushauri kwa walimu naomba watulie tu! Hawana jipya hao.
  Wameshindwa kujijengea misingi mapema yakuishinikiza serikali iwafanyie kima cha chini japo jiwe 3 tu lakini hakuna.
  Nawahurumia wanateseka mno sijui wanabajet vp?
   
 7. Y

  YesSir Senior Member

  #7
  May 17, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  60,000 is just too little
   
 8. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Acha uongo ! 60,000? Siamini ,sasa viongozi wao huwa wanafikilianini kuhusu hii kitu?
  Ila ndo maana matoto ya sikuhizi ni majinga, sidhani kama mtu anaweza kuthamini kazi ambayo haimsaidii.
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,796
  Likes Received: 1,044
  Trophy Points: 280
  he kwani hawajalipwa tu! si niliwasikia maafisa elimu kwenye mkutano mkuu wao pale morogoro kuwa ofisi zao hazina pesa kwa kuwa zimepelekwa kulipa madeni ya walimu?
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  May 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kaka maneno yako si barabara, sikutegemea kwa mtu kama wewe kutamka hayo ulio tamka. Hao walimu unao waita hivyo ndio hao hao walio kutoa kutoka kwenye kutokujua na kukufikisha hapo, kiasi ya kwamba nawe leo unaonekana mtu.
  Hisingekuwa jitihada zao za kukufundisha kusoma na kuandika, leo hii ungekuwa wapi?
  Hiyo misingi unayoitaja ni hipi ambayo wameshindwa kujijengea!?

  Unapowacheka na kuwaona kuwa hamnazo, hatakaye kuja kuhathirika zaidi ni nani kama si mtoto yule utakaye mpeleka kufundishwa na mwalimu huyo huyo unaye mcheka leo kwa kuwa na mshahara mdogo. Je unafikiri hiyo mitahala ya shule ataitekeleza vipi na hali yake kiuchumi ni duni?

  Usije kushangaa mtoto wako ukamkuta mitaani anauza ubuyu na kashata za mwalimu kipindi cha masomo...!?

  Tujifunze Watz kusaidiana na kujaliana ili tuweze kukomboana kifikra na kimawazo... ili tulijenge taifa letu ambalo kila kukicha elimu inazidi kudidimia.
   
 11. Y

  YesSir Senior Member

  #11
  May 18, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari ndio hiyo ndugu yangu
   
Loading...