Walimu waahidi makubwa - Lazima kitaeleweka

Duh! Kali kweli kweli.Nzuri lakini,maana bila Mwalimu tusingekuwa na Rais,Wabunge,Wanasiasa,Madaktari,Wahasibu na Walimu wenyewe.Sasa sijui yupi muhimu,Daktari au Mwalimu?Nisaidieni
Wote ni muhimu.Manake bila daktari labda huyo mwalimu asingezaliwa salama au hata baada ya
kuzaliwa angeugua na kufa.Sidhani kama kuna mtu anaweza kufikia umri wa kuwa mwalim ambaye
hajawahi ugua hata mara moja.
 
hao watoto wakijakuwa vibaka na kukaba watu sijui hasara inakua kwa ccm au jamii nzima kwa ujumla akiwemo mwalimu.
Ndo maana nasema watanzania tuna akili za kijinga sana.ni upuuzi huu unaweza kukuta tanzania peke yake.

kiwalo na liwe.....!
 
tutapambana mpaka tone la mwisho. je hawajui walimu ni sawa na ngombe wa maziwa. ukimchukiza kidogo tu hupati maziwa. pole yao wanafunzi yaani wataishi kupata division iv na 0.
Naomba kuuliza, waalimu wa private shule wamegoma? kama hawajagoma nasikitikia sana watoto wetu sisi ambao tunawategemea hao walimu waliogoma.
hii vita tujue kabisa ni ya kwetu sisi na si serikali, nakumbuka mgomo wa madakitari, tulioumia wengi ni sisi ambao tunategemea hospitali za serikali. wenzetu walipoumwa walienda kutibiwa hata nje ya nchi, na kwenye shule itakuwa hivyo hivyo, watoto wetu watapata zero, watoto wao hawataathirika. Inauma sana
 
3x3=33 WELL DONE,ha ha ha ha ha
be confident on it, we are supporting you walimu.

Umekosea mkuu hiyo hesabu. Ni kwamba 3x3=333. Yaani tatu mara tatu unapata tatu tatu (i.e. 3 3 3). Tehetehetehetehetehete
 
Hiyo ni silaha ya maangamizi duh. Nadhani wanatakiwa watokee watu na busara zao kama kina Salim Ahmed Salimu wawashauri viongozi wetu namna ya kutatua migogoro. Hivi tutakuwa na taifa gani la watumishi walioigomea kazi yao? Hii ni hatari sana kwa mtu anaeangalia mbali walau miaka 10
 
Lazima kitaeleweka!

Viva walimu

attachment.php



Source Habari leo

Hawa ni waalimu hivyo unaweza kufikiri wanachofanya madaktari. Wao hawatumii chaki na ubao wanatumia mwili wako na wangu

Kuna haja ya kuomba Mahakama waingilie kati waaandao monitoring ya hawa waalimu wasitufanyie mchezo. Lazima wafundishe na work plan zao ziwe approved na Chief Justice.

Pia daktari akikuandikia sindano iwe approved na RC au DC pia akikunyima sindano ajieleze

We must be joking
 
Wewe mwl wa upe unaonekana kuwa na jazba. Kamwe waalimu hawataweza kuwa wamoja hata siku moja. Halafu unaongea ovyo ovyo tu bila ya kujua unachosema. Wakaguzi wa elimu pamoja na kuwa ni waalimu lakini wanaishi dunia tofauti na waalimu wala chaki.

Wale kila mwaka wanazungukia mashule na wanalipwa posho nzuri tu.wao kila mwaka ni mavuno tu. Swala la hela kwa ajili ya maendeleo yao binafsi kama kujenga nyumba si issue.

Kwa hiyo mwalimu OMONTO WA HENE wewe kufa ki vyako tu usitafute wa kwenda naye kaburini.

TWIZAMALLYA ninatamani kuendeleza malumbano na wewe, ila nimeogopa kitu kimoja tu: watu watashindwa kututofautisha! Lakini kwa kuwa kufundisha ni kazi yangu na ni taaluma ambayo mimi ni mgenzi kwayo, nitachukua muda mchache kukufundisha. Suala la kuamua kuyaelewa mafundisho yangu nitaliacha kwako binafsi kama ambavyo nimekuwa nikiwakokota mbuzi wangu hadi kwenye mto na kuwaachia maamuzi kamili juu ya kunywa maji. Wakaguzi wa Shule wapo katika ngazi tatu nchini mwetu. Wapo Wizarani, wapo katika kila Kanda na wengine wapo wilayani. Wale wa Kanda hufanya ukaguzi maalum mara moja moja hasa kwa shule za sekondari kwa kuwa raslimali wapewazo haziwapi uwezo wa kukagua mara nyingi kwa shule zote. Wale walioko wilayani wanawajibika kukagua shule za msingi katika wilaya husika lakini 'trend' inaonesha wakaguzi hawa hukaa tu ofisini mwao kama wanafunzi wa darasa lisilo na mwalimu na muda wa kazi uishapo hutawanyika hima. Hawana kazi ya kufanya kwa sababu hawana usafiri, viandikwa na viandikio, achilia mbali posho za kujikimu! Ikitokea mwanya fulani wakaguzi wa shule wakapewa fursa ya kubadilisha kitengo cha kufanyia kazi, nikudokeze tu, wote watakimbia fasta!! Kwa hiyo hoja uliyoitoa hapa kwamba wakaguzi wao ni 'full posho', siyo tu kwamba ni hoja mufilisi, bali ndiyo hoja imewasaidia wanajamvi kukujua jinsi ulivyo mbu mbu mbu wa kitengo hiki. Ila nakushauri usitahayari, maana ninaamini utanishukuru kwa kukuelimisha bila kukudai malipo yoyote. Karibu kwa maswali, mchango au nyongeza yoyote yenye tija, hasa kwa upande wako!
 
Jamani hamuelewi? Mbona mkulu ameweka wazi kuwa haya matatizo yatashughulikiwa na watawala wajao wa awamu ya tano!!! Yeye amemaliza. Sasa hivi serikali ya JMT iko kwenye gear ya auto-pilot!!!
 
Bado ninaamini walimu wana akili timamu na wanajua nafasi yao katika Taifa. Kwavile serikali ikiwa na shida hukimbilia walimu (kuandikisha wapiga kura etc) lakini kwenye madai yao wanaonekana hamnazo, basi wasikubali kuwa 'spare tyre'. Waingie ulingoni tuone nani mshindi. Wasipotoshe watoto wetu kwavile hawana kosa bali wawaelimishe jinsi serikali na chama chake vinavyokumbatia mafisadi na kuwadharau walalahoi. Hili somo la uraia likifanyika vizuri haswa sekondari, miaka mitano tu ijayo walimu watavuna. Wakati wa kupanda ni sasa kwasababu waliyemtegemea amewatelekeza. Mwenye masikio na asikie neno hili mzawa awaambia walimu.
 
So madaktari wataendelea kuua.
Walimu watafundisha kwa kumislead.
Huu utamaduni unaojengeka ni wakijinga sana.
Hivi wanadhani wanamkomoa nani?AU SEREKALI?
Kwa akili zao wanadhani huyo serikali ninani?

Utamaduni unaojengwa na serikali yako ndo una akili eeh! Hii nchi imeanza kufuata utaratibu wa LIWALO NA LIWE,ngoja twende hivihivi ndo tutaheshimiana
 
hao watoto wakijakuwa vibaka na kukaba watu sijui hasara inakua kwa ccm au jamii nzima kwa ujumla akiwemo mwalimu.
Ndo maana nasema watanzania tuna akili za kijinga sana.ni upuuzi huu unaweza kukuta tanzania peke yake.


Mkuu (Elungata) tutake radhi Watanzania. Matusi yako ya rejareja ya kuwajumuisha Watanzania wote ni ya kutudhalilisha bila sababu. Ingefaa angalau ungejisemea mwenyewe kuwa na akili hizo. Akili hizo ni zako peke yako kwa ujumla wetu Watanzania wala hazituhusu.
 
Kitaeleweka tu kwa walimu, vinginevyo darasani itakuwa hivi:
a) 1 + 3 = 13
b) 73 - 3 = 7
c) 3 x 3 = 33
d) 7 x 2 = 77
physics kila formula itakuwa reciprocal. Hyo ndo plan B kwa walimu wa science.
Sipat picha kwa wana history, 'Binadam wa kwanza alikuwa NYERERE.english nako,you took my pen,tooknt you?
:D chezea walimu sie wewe
 
Back
Top Bottom