Walimu wa secondary kwenda msingi serikali inakwepa nini

Walimu wa secondary kwenda msingi serikali inakwepa nini

Huu ni ujinga wa hali ya juu.walimu wa secondary amejifunza kufundisha huko na si msingi
 
Acha waende maana walimu wa art wamekuwa wengi mno , unakuta darasa moja mfano kidato cha pili history wanafundisha walimu wawili , unakuta walimu wanashinda hawana kazi wanapiga majungu tu chini yamiti ...asante serikali kwa kuliona hili.
Shuleni kwako, lakini shule za secondary za vijijini hali ni tofauti na unachokizungumza.
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu.walimu wa secondary amejifunza kufundisha huko na si msingi

Cha ajabu sijaona! Wale mashuhuda wa mpango wa Universal Primary Education (UPE) watakumbuka kuwa shule ziliwahi kuwa na walimu wasiokuwa walimu kitaaluma na walipata on-the-job training! Wengi wao hata hawakuwa na elimu zaidi ya elimu ya msingi. Kama hao waliweza kufanya kazi ya ualimu huku wakipata on-the-job training, kitu gani kitamfanya mwalimu wa secondary, ambaye kitaaluma ni mwalimu, ashindwe?
 
Mwajiri ndie anaejua ma gap na jinsi gani ayazibe ili kuleta tija ktk kazi. Work load zao ni ndogo mno tofauti na mishahara mikubwa wanayopata. Mzalendo wa kweli hawezi kulaumu wala kulalamika.
 
Mwajiri ndie anaejua ma gap na jinsi gani ayazibe ili kuleta tija ktk kazi. Work load zao ni ndogo mno tofauti na mishahara mikubwa wanayopata. Mzalendo wa kweli hawezi kulaumu wala kulalamika.
kwa mfano mkurugenzi anawork load gan kubwa kulinganisha na maslahi/marupurupu na stahiki anazopewa ikiwemo nyumba maji umeme bure usafiri n.k ukilinganisha na mshahara wa mwalimu laki tano alipie vyote hivyo kwenye hiyo hiyo laki tano..!
 
Mwongo mkubwa, ukienda nchi za watu chekechea anafundishwa na degree holder siyo certificate, primary hadi secondary pia ni degree holder na PhD,
Umemuita mwenzako muongo ila wewe umeandika usichokijua.

Wenzetu wanazo level tofauti za elimu ya ualimu zinazofungamana na specialization. Wanayo bachelor degree in early childhood, bachelor in primary education na bachelor kwa jili ya secondary education.

Hoja ni kwamba huyu mwenye bachelor ya secondary education umempa mafunzo gani ili akidhi mahitaji ya primary education..?
 
ni aina fulani ya kuchezea rasilimali watu
 
Nawaza tu, hao walimu wakuu wenye certificate afu unaletewa surbodinate mwalimu wa shahada.
Sasa hivi huwezi kupewa ukuu ukiwa na cert mkuu,wqliokuwepo wanaisha hivyo then experience nayo inamata
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mwongo mkubwa, ukienda nchi za watu chekechea anafundishwa na degree holder siyo certificate, primary hadi secondary pia ni degree holder na PhD,
Usikurupuke tu kujibu kwakuwa unaweza kuandika mkuu,jamaa ana point ya msingi kusema vile kwani hata unalolisema lipo lakini halipo kama unavyofikiria wewe,
Ni kweli kabisa nchi zilizoendelea kuna watu wana degree,na hizo PhD na wanafundisha chekechea lakini hizo degree zao ni za eneo husika kwa mfano kuna walimu wenye shahada ya elimu ya awali,na msingi kila mmoja anafundisha katka eneo lake na sio mtu ana shahada ya elimu ya msingi akafundishe elimu ya awali BIG NO
 
Duuuuu!, Educational psychology mnayosoma chuoni inawahusu tu watoto Wa miaka 15(Wa sekondari)?
 
Walimu acheni kulia lia, nyie muda wote ni kulialia tu, psychology mlikuwa mnasoma nn, tunataka tuone hizo implications kwenye field ya elimu, mfano, Piaget's stages of child development ambazo zipo nne , sensorimotal stage, preoperational stage, concrete stage na formal operational stage zinaonesha kabisa mtoto Wa umri Fulani anaweza kusoma kitu gani na kwa namna gani, na wengine tulikuwa walimu acheni kudanganya umma kwamba hamuwezi kufundisha s/msingi, labda km siku hizi hamsomi psychology
 
Ni kwamba MTU anasoma degree ( law, business, arts, science, Engineering etc.) Baada ya degree ya kwanza anasoma certificate kwa miezi miwili au mitatu anaenda fundisha either primary or secondary,
Ujanja ujanja kama huu,hauwez kusaidia.Ndomana,elimu yetu inakosa thaman,kila kiongoz anataka kuja na mifumo yake,na mifumo mingine haina tija kabisa.
 
Nadhani serikali haina vipaumbele kwasasa.
Elimu bure inatusumbua sana kwani serikali ilijiingiza kichwa kichwa.

Serikali imeweka matumizi makubwa kwenye siasa kwa lengo la kupambana na upinzani.
Upinzani unaonekana kama ndio kikwazo kikubwa kwa sasa.

Siamini kama kuna walimu wengi hadi kuzidi kwa sekondari labda mijini, na kama wapo wa ziada kwanini wasiwahamishie shule za pembezoni palipo na upungufu?
Ukipinga unaonekana mpinzani
 
Naamini wote sisi ni wazima

Jana nmeona tangazo linatembea lihusulo uhamisho wa walimu wa secondary wa sanaa kwenda kufundisha shule ya msingi kwa lengo la kufidia upungufu wa walimu uliopo shule za msingi.

Nmejikuta napata maswali
Je ni kwamba serikali haina pesa ya kuajiri walimu wengine au inaongeza ufanisi katika kazi na ni kwa namna gani sasa .
Mtaani kuna walimu tokea2015 je hawa hatima yao ni nini?

Kiufanisi litakuaje hili?

Je hawa walimu wataokwenda shule za msingi wataweza kuendana na kasi ya huko
Tafadhali tuwekee hilo tangazo au tupe source (chanzo chako) ili tuone kipi haswa kimeandikwa, tujadili kwa umakini zaidi na sio hisia zetu. Kwa sasa nitahifadhi maneno.
 
Acha waende maana walimu wa art wamekuwa wengi mno , unakuta darasa moja mfano kidato cha pili history wanafundisha walimu wawili , unakuta walimu wanashinda hawana kazi wanapiga majungu tu chini yamiti ...asante serikali kwa kuliona hili.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Serikali imeangalia idadi ya walim,haijaanglia uwiano wa darasa na idadi ya wanafunzi.
Wanafunzi 90 wanasoma darasa moja hapo wakiingia walim wawili utasema "Walim ni wengi",Uwiano wa serikali darasa moja watoto 40-45 tu.
Lakini kuna shule hadi watoto 100 wanasomea daraaa moja
 
Cha ajabu sijaona! Wale mashuhuda wa mpango wa Universal Primary Education (UPE) watakumbuka kuwa shule ziliwahi kuwa na walimu wasiokuwa walimu kitaaluma na walipata on-the-job training! Wengi wao hata hawakuwa na elimu zaidi ya elimu ya msingi. Kama hao waliweza kufanya kazi ya ualimu huku wakipata on-the-job training, kitu gani kitamfanya mwalimu wa secondary, ambaye kitaaluma ni mwalimu, ashindwe?
Kwa Tanzania,mwalim anaweza kuanza kazi had anaataafu asipate mafunzo ya aina yeyote yale akiwa kazini,labda ya kusimamia mitihan ya taifa kama atapendekezwa
 
Back
Top Bottom