Walimu wa Msingi na Sekondari Pitieni hapa .

Walimu wa Msingi na Sekondari Pitieni hapa .

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Mwalimi anapaswa kumfundisha mwanafunzi kwa kuzingatia nyanja kuu tatu ambazo ni;
1). Maarifa(cognitive) (2). Stadi(psychomotor) na (3). Mwelekeo(Affective).
Kwa maana nyingine, mtoto anapaswa kulelewa kwa kuzingatia makuzi ya kiakili, kimwili, na kiroho/jamii. Watoto wa Siku hizi wanalelewa kiakili na kimwili. Wameachwa kulelewa katika nyanja ya mwelekeo(kijamii au kiroho) kuanzia kwenye familia na jamii. Omari(2006), katika kitabu chake cha elimu ya saikolojia kwa walimu(Educational psychology for teachers) ametaja changamoto zinazowakabili wanafunzi kuwa ni matatizo ya kijamii, taaluma, afya, matatizo ya kupevuka. Akitaja matatizo katika kipindi cha kupevuka anataja hasira, ngono na mambo yahusuyo jinsia zao(sexuality), msongo wa mawazo na kujiua. Hayo yote yanapaswa kushughulikiwa. Yapo yale yanayohitaji motisha na vichokoo, na mengine yanahitaji adhabu(James Watson na ujenzi tabia, behaviourism). Chagua nadharia sahihi kulingana na wakati na mazingira. Walimu nao wanahitaji ushauri nasaha.
 
Kwa huu mfumo wetu wa elimu, na namna walimu tunavyochukuliwa na jamii, namna elimu ya ualimu "navyogawiwa" yaaani inatolewa kama alternative ya mtu kupata chuo cha kusoma, huku hakuta akisi hizo domains mkuu,

Mana mpaka tujenge mtoto inabidi tuakisi muelekeo wa jamii, elimu inabadilika kutokana na mahitaji ya jamii, tazama tulipofikia leo ni uwekezaji mbovu wa u katika mitaala ya elimu, shida nimoja tuu ni :Teachers' education inatolewa, haifundishiwi😕😕
 
Back
Top Bottom