Walimu wa mazoezi kero katika mahusiano

Kwa sasa na mimi ni mwalimu wa mazoezi, nimefungua fitness centre mtaani, wadada jitokezeni kwa wingi!
 
duh.... yametokea ila inataka moyo kweli kushudia jinsi walimu hawa wamazoezi jinsi wanavyowafanyisha mazoezi hawa wake, na dada zetu.
mimi nimeamua kumpiga stop wife... mazoezi ni hapa hapa home....

Umefunga mjadala.

Kati ya vitu ambavyo wanawake wengi hawapendi ni kushikwa na mwanaume yeyote tu sehemu kadhaa za mwili kama miguu, mapaja, nyonga, mabega na makalio. Baada ya kufanya aerobics huwa wanamaliza na kitu zinaitwa "stretching". Wanalala chini na kujipanua. Mwalimu anakuja kuwasaidia ili wafanye hiyo stretching inavotakikana na kwa sababu ya ugumu wake, ndipo walimu hawa wenye mikono yenye nguvu huweza kuwashika akina dada sehemu ambazo kumbe hushikwa na wapenzi wao!! Ni hapo wanadada huanza kuwaamini waalimu na hata kulinganisha ushikaji wa nyenzo kati ya mwalimu na mpenzi!!

Mwanamke yeyote anayejiheshimu humpenda mwanaume kimapenzi baada ya kumwamini. Ni uaminifu huu kwa mwalimu na contact za kimwili ndio husababisha hisia za kimapenzi.

Gynasium nyingi zimetengenezwa na faragha kwa wanawake hivo kama mwalimu anamtaka mdada, si jambo gumu kwani hiyo kumshika ******, mapaja na miguu na kumkunja itafanyika mwanamke akiamini haonekani na ni sehemu ya mazoezi. Ni hapo mdada ataanza kupenda baadhi ya mikunjo na kuitamani.

Lakini sehemu kubwa ya ufedhuli, hufanywa na kukosa uaminifu. Si kwa mwalimu tu, bali hata kwa mwanafunzi.
 


I will be right back soon!!
 

Mkuu uwezowako wa kufikiri, kuchambua mambo ni mkubwa, nimependa mchango wako. Asante!
 

Hawa walimu mnalaumu bure tu. Akikuomba mzigo ukikataa atakuua?
 
Glory umesema vyema!
Utawalaumu waalimu wa gym, waosha miguu na wapaka kucha rangi, wauza mitumba na handbags, wauza nyama, wauza genge na taxi drivers?

Mkuu Gagurito, kwanza gym sehemu ya kubadilishia nguo ina ya wanawake na wanaume, na kuna mabafu pia. Na huko nimeshuhudia wanawake wasio na tatizo na privacy yao wanavyojiachia na kukaa utupu. M'baba hawezi kuchungulia manake rolling eyes zitamletea makengeza. Isitoshe mwalimu hawezi kupata privacy hiyo ya kubanjuka na mteja kwenye bafu sio la wanawake wala wanaume unless ni same sex nae!

Nimejifunza hii, mwanamke awe mzuri ama mbaya, atatakwa kila aendapo. Na mtakaji anaangalia response. Usilaumu gym, laumu mkeo. Kama ambavyo mie silaumu kona bar, namlaumu la'aziz wangu
 

Hivi issue hapa ni wake za watu kutoka nje ya ndoa au huyo mwalimu kuwapa dose? Kwa taarifa yako wanawake pia uvutiwa na physique ya mwanaume hasa kifua cha haja na zile six pack, kama mwalimu yuko hivi na waume zao wamevimbiana kama chatu kameza mbuzi unategemea nini kitokee!

Pia una uhakika kuwa wanawake hao wote wameolewa au ndio wale wafanyabiashara wa Dubai na China?
 
Ahh kama ndo hivyo inabidi nimuondoe mpenzi wangu kwenye ile GYM...... ,maana anaipenda kweli na akiwa anenda huko anajipodoa sana sijui kama atakuwa kasalimika.
 
sio hawa tu mkuu, kuna waalimu wa tuisheni, wafanyakazi wa ndani wa kiume, ni mlolongo mrefu..tatizo ni nini?? tamaa kwa wenza na pia ugumu wa maisha..hawa jamaa wanakaa kimitego sana kwani wanajua kuwa kumpata mwanamke mwenye uwezo ndio utakuwa mwanzo wamaisha mazuri..huwaga nawasikia sana wakizungumza maneno kama hayo..kwahiyo wao ndio huwa wa kwanza kuweka mitego kwa mtu wanayemuona kuwa atawatoa kwenye matatizo yao
 
S
Sisi walimj was mazoezi tuna pata changa moto nyingi sana lakini kama MTU hutambui mile unacho kifanya hakika lazima kuharibu kazi yako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…