Walimu wa Kenya wapata nyongeza kubwa yamishahara..!!!

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843


Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya asili mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa kwa wiki tatu sasa.


Kutokana na maafikiano hayo kati ya serikali na chama cha walimu nchini KNUT, sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu.
Hatua hiyo sasa itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na upili za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni.
Vyama vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali kuwalipa walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja.
Awali serikali ya Kenya ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali kulipwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu.
Mwalimu wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi 39.000.
Serikali ya Kenya imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa zaidi ya walimu 250,000 ambao walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi.
 
nadhani hii itawasaidia waalimu wa Tanzania kujua kuwa mkiamua kukomaa hata muuaji huwa anashindwa. thumb up to Kenyan teachers, Tanzania bado twakuna nazi tu, tukitishwa kidogo tu, tunapiga magoti na kuomba samahani, yaani badala sisi ndo tuombwe samahani, sie ndo tunaomba samahani. MAAJABU!!! halafu linakurupuka dubwana moja kule mbeya limelewa u-dc wa kupewa, linawakashfu waalimu, mbaya zaidi waalimu kimya tu utadhani hawana akili timamu hata za kujua tu kuwa tunatukanwa. Tunayemuomba samahani mwenyewe fisadi, muongo, mwizi na m-binafsi wa kutupwa!!!!.
 
Walimu hawapo kimya mkuu....we huoni wanaoingia Secondary bila kujua kusoma na kuandika wanaongezeka? And thats how they are delivering their message!
 
Back
Top Bottom