Walimu wa English Medium Schools mnawatumia Vibaya Wanafunzi

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Mtoto wangu ana Umri wa miaka 5 sasa anasoma shule moja ya English Medium. Mbali na ada ya mwaka kiwa tsh 3,000,000. Kuna udambwi dambwi mwingi sana mpaka sasa nachoka kwa usumbufu.

Kila baada ya miezi miwili kuna picnic hii mzazi nachangia tsh 70,000/ akienda huko anapigwa picha akija nazo kesho yake picha moja anaambiwa ni tsh 2,000. Anaweza kuja nazo hata 10.

Kila baada ya week mbili wanakuwa na class party hii anatakiwa aende na juice za box 3 na chips something au sausages. Au any dry food but siyo wali,ugali au ndizi za kupikwa.

Mtoto wangu ile juice ya box hata moja tu hamalizi. Sasa box tatu nawaza anaenda kuoga kabisa?nmekuwa nafanya hivyo lakini leo nikawaza na kusema ni kweli uchumi umebana. Lakini why wao waamue kutuchuna wazazi?

Jamani mkila na kipofu msishike mkono...mnafikia hatua mpaka wazazi mnatushtua sasa. Ilitakiwa mnapotaka kutupiga mumeweke hata gaps.siyo mnafuliliza mpaka nasi akili inakaa sawa.

Haya ni matumizi mabaya ya wanafunzi kwani kuna siku mtamisi pilau kuku na mtataka kila mtoto alete pilau kuku. Hizo juice za box kila mtoto akileta 3 si mwisho mnaweza fungua maduka ya vinywaji?

Aaahh! jamani taratibu wandugu muwe na huruma, ubaya inakuwa ngumu kumnyima Junior pesa maana kesho yake wenzake wakimsimulia atakuwa mpweke.naye tu hawez kubali kukosa.

Walimu wanawaambia nendeni mkadai msikubali.ukikosa shauri yako...mtoto akija hasikii la mwadhini wala la mnadi swala.anataka pesa...walimu muwe na huruma. Kuna siku ntaaamua kuwajia shule halafu mnione mimi mbaya.watu tushachanganyikiwa nyie mnatuletea mambo ya kifala...

Haya mimi nmeweka hili kama angalizo next time tutakuja kueleweshana kwa vitendo kama sijamwasha mtu mbata na kumtaka anioneshe jinsi ambavyo mtoto wangu alimaliza juice tatu za box.
 
Back
Top Bottom